Monday, December 14, 2015

Tizama Jinsi DC Makonda Alivyoamuru Mbunge Kubenea atiwe mbaroni

SAED KUBENEA MBARONI KWA AMRI YA MKUU WA WIYALA YA KINONDONI PAUL MAKONDA 

Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) amekamatwa na polisi eneo la viwanda (EPZA) Mabibo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.Tukio hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda cha nguo cha TOOKU ambao walimpigia Mbunge wao aende kutatua mgogoro huo.

Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana, akakutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya Kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9. 

Ilipofika saa 10:30 Makonda alikuja na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.

Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko kesho na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na waziri wa Afya wanawake, jinsia na watoto.

Alimzuia Mbunge asihutubie kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, Kubenea alisema ni vema aseme neno, Kubenea akaanza kumdhihaki Makonda aliyeamuru Mkutano ufungwe na akaamrisha Kubenea akamatwe mara moja kwa lugha chafu kwa Mkuu wa Wilaya. Katika tukio hilo Mwandishi wa habari wa Star Tv aliyekuwa anarekodi tukio hilo alinyang’anywa camera na Polisi.

Mwandishi wa habari habari wa MwanaHALISI Josephat Isango alijaribu kumsaidia mwenzake ili arejeshewe Camera lakini Polisi wa kituo cha Magomeni walimtisha, na kumtaka kuondoka haraka huku wakiondoka na aliyenyang’anywa camera.
 

No comments: