Friday, January 30, 2015

LEMA,LISU,ESTER BULAYA WALIPUKA BUNGENI,NI UFISADI WA KUTISHA,SOMA KAULI ZAO HAPA


YANAYOJIRI BUNGENI: NATAMANI KWENYE AMRI ZA MUNGU IONGEZWE YA 11 ISEMAYO 'USIWE CCM' - KASEMA LEMA

Wabunge wanaendelea kuchangia taarifa za Kamati za Hesabu za Serikali PAC na LAAC zinazoonesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma

Lema: Haiwezekani kila siku tukija humu tunazungumzia wizi tu, inatakiwa tuzungumzie mipango ya maendeleo ya wananchi sio kila siku wizi wizi wizi unaosababishwa na CCM.

Lema: Kama ningeweza kupendekeza pia kwenye Amri Kumi za Mungu, ningependekeza iongezwe amri ya 11 inayosema 'USIWE CCM'

Lema: Katika mazingira kama haya, nathubutu kusema 'My Country is like a Getho' mambo hayaendeshwi kwa utaratibu kabisa

Esther Bulaya: "Yani watu wanagawana posho Bilion 9, na wanafunzi wanasoma kwa shida halafu mnataka tuwapigie makofi haiwezekani"

Esther Bulaya: "Hatuwezi kila siku tunakuja hapa majibu yaleyale kila siku wizi wizi wizi, haiwezekani, hawa watu washughulikiwe"

Lissu: "Kinachotufikisha hapa ni Rais kushindwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuwawajibisha watendaji wake"

Lissu: "Tunachotakiwa kufanya hapa ni kuanza na hawa mawaziri tulionao humu ndani, tukubaliane kuwawajibisha"

SIKIO LA KUFA,TIZAMA HICHI WALICHOTANGAZA VIJANA WA CUF TENA

Pichani ni ,Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa
Chama cha Wananchi CUF-JUVICUF,Hamidu Bobali,
Akizungumza na Waandishi wa
Habari leo,jijini Dar es Salaam
NAKAROLI VINSENT

JUMUIYA ya Vijana  ya chama cha Wananchi CUF-JUVICUF  wametangaza kuanzisha maandamano makubwa ya kulaani vitendo wanachodai  ni vya ukiukwaji wa Haki za Binadamu  kilichofanywa na Serikali   ya Chama cha Mapinduzi CCM,cha kumpiga Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba na wanachama wao, walipokuwa kwenye maandamo.
        
 Kauli hiyo JUVICUF imekuja siku moja wakati  Bunge likiwa  limefunga Mjadala ulioibuliwa  na Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia juu ya kupigwa mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba,na Bunge kufikia maamuzi ya pamoja kuiachia mahakama kutoa hukumu.
        
 Akitangaza Maandamano hayo leo Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF-JUVICUF,Hamidu Bobali,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema chama hicho kimepokea kwa masikitiko makubwa uongo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani nchi Mathias Chikawe wakati alipokuwa akitoa taarifa Bungeni.
    
 “Tunasikitisha sana juu ya kauli iliyotolewa na waziri Chikawe ndani ya Bunge jana kwa kuweka uwongo mwingi kwenye taarifa yake kwa kumsingizia profesa wetu kwamba alikiuka sheria, sio kweli  kwani profesa alikuwa sahihi,na ndio maana tunaandaa maandamano sisi Vijana wa Chama hicho ili kulaani vitendo vya kinyama na vya kuwapiga viongozi wetu na wanachama chetu”alisema Bobali.
         
Bobali alibainisha kuwa Jumuiya ya hiyo vijana kufuatia matukio hayo wanamtaka Rais Jakaya kikwete kuomba Radhi watanzania juu ya matukio hayo ya kupigwa na kudhalilishwa pamoja kuvuliwa kwa viongozi wetu na jeshi la polisi.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa Makini
           Aidha,Jumuiya hiyo alimtaka Waziri wa mambo ya Ndani,Mathias Chikawe,pamoja Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu kujiuzulu kwenye Nafasi zao kutokana kitendo chao cha kudanganya Umma kwa kusema Maandamano hayo yalikuwa hayana kibali.


Vilevile,Mwenyekiti huyo wa Vijana alisema Tarehe ya Maandamano itatangazwa mda wowote kuanzia sasa na kuwataka wananchama hao kuwa na subira kuwaachia viongozi wa chama hicho

Thursday, January 29, 2015

TIZAMA REPORT NZIMA YA SAKATA LA LIPUMBA LEO,CUF WAJA JUU,MJADALA BUNGENI WAJADILIWA.


NA KAROLI VINSENT

SIKU moja kupita  baada Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba kupandishwa mahakamani kwa kile kinachodaiwa kushawishi wanachama wa chama  hicho kuandamana na kupelekea jeshi hilo kutumia nguvu katika maeneo ya Mtongani wilaya ya temeke Jijiji Dar es Salaam.
          
Nacho Chama cha Wananchi CUF,kimeibuka na kulivaa jeshi la polisi nchini na kusema jeshi hilo linatumiwa na chama cha mapinduzi CCM,ili kudhoofisha upinzani nchi.
     
     Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf ,Juma Duni Haji,Wakati wa Mkutano na  waandishi wa Habari ili kuzungumzia kitendo alichofanyiwa mwenyekiti wa chama hicho cha kupigwa na polisi,ambapo Bwana haji alisema Chama hicho kinalaani vikali kile alichodai ni hujuma wanachofanyiwa na polisi Kuzoofisha upinzani nchini.
        
 “Cuf-tunalaani kitendo hicho cha jeshi la polisi nchini kutumika kisiasa kuzuia shuguli halali za vyama vya upinzani nchini na kuwaruhusu ccm kufanya wanavyotaka bila kubughudhiwa na vyombo vya dola wala kisingizia vya sababu za kintelijinsia”
        
 “Kumkamata mwenyekiti wetu wa taifa,kumdhalilisha pasipo kuwepo kwa maandamano ambayo CUF na viongozi wake walishakubaliana kutofanya”alisema Bwana Haji. 
        
 Bwana Haji aliongeza kuwa licha ya kulaani kupigwa kwa mwenyekiti wao pia wanalaani kupigwa hata kupigwa wananchama wao ambao wanadai walikuwa hawana kosa lolote.
        
 Aida,Bwana Haji alibainisha kuwa hata hoja wanayoisema jeshi la Polisi kwamba chama hicho kilidharau magizo ya jeshi la Polisi,kuendelea na maandamano hayo kwa kusema sio kweli kwani chama hicho kilifuata maagizo yote.

        
Vilevile,Bwana Haji alilitaka jeshi la polisi kuacha kutumika na chama cha  mapinduzi CCM kwani wanachokifanya hakikubaliki na chama hicho kitachoka na kuongeza kuwa kuchoka huko kutapelekea Taifa kutotawalika na amani ya nchi itakuwa imevurugika
      
 Bungeni Mjadala uliendelea Hivi.

MICHEZO24--TFF YAHADHARISHA MGOGORO WA ZFA KORTINI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)l imepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo tena kortini kwa kesi dhidi ya uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), jambo ambalo linaweza kuathiri ushiriki wa timu za Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na Kombe la Shirikisho.

Mwishoni mwa mwaka jana, TFF ilihadharisha juu ya masuala ya mpira wa miguu kupelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.

Kutokana na hali hiyo, TFF iliiandikia barua ZFA kutaka mgogoro huo uondolewe kortini na yenyewe kuridhia kuwa tayari kupeleka ujumbe Zanzibar ili ukutane na pande zinazohusika.

Pia TFF ilisema timu za Tanzania Bara zisingeruhusiwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 iwapo kesi hiyo ingeendelea kuwepo kortini na kutaka iondolewe bila masharti yoyote.

ZFA iliithibitishia TFF kuwa kesi hiyo imeondolewa kortini bila masharti, hivyo timu za Tanzania Bara kuruhusiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ni muhimu suala hilo likashughulikiwa haraka ili kutohatarisha ushiriki wa timu za KMKM na Polisi kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

BINTI WA MIAKA 22 ASHINDA MILIONI 100 ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544

LHRC NAO WATOA KAULI KUHUSU SAKATA LA KUPIGWA KWA LIPUMBA,SOMA HAPA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu  Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizngumza na wahabari mapema leo
Sakata la kupigwa na kudhalilishwa kwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa IBRAHIMU LIPUMBA katika maandamano ya chama hicho juzi huko Temeke limeendelea kulaaniwa kila kona ambapo leo kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC wameibuka na kauli ya kulaani kitendo hicho na kusema ni kitendo cha kinyama na kinachoididimiza democrasia ya Tanzania.
            
 Akizungumza na wanahabari katika mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili mapungufu ya katiba pendekezwa na sheria ya kura ya maoni Mkurugeni mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria na katiba ya Tanzania na maandamano ni haki ya kila mtanzania hivyo kitendo kinachofanywa na polisi kujaribu kuwanyamazisha watanzania kwa kuzuia maandamano ambayo ni ya amani ni kitendo kibaya na kisipopigwa marufuku kitalipekeka taifa la Tanzania mahali ambapo sio pazuri.

Mwanasheria kutoka LHRC  HAROLD SUNGUSIA akizungumza katika mkutano huo ambao unafanyika katika ukumbi wa ubungo plaza jijini DAR ES SALAAM
  Katika mdahalo huo ambao umehudhuriwa na baadhi ya wanahaharakati wa kuitafuta katiba akiwemo aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba HAMFREY POLEPOLE na   wadau wengine wameendelea kupinga kwa kasi mchakato wa kupata katiba kuendelea kwa kile ambacho wanadai ni kukosa uhalali wa kisiasa na mapungufu mengi ambayo yapo katika sheria ya kura ya maoni ambayo itasimamia mchakato huo

Wednesday, January 28, 2015

MICHEZO24--HIVI NDIVYO SIMBA ALIVYONYONYOLEWA TAIFA JIONI HII

CHOLLO AKOSA PENALTI DAKIKA YA MWISHO, SIMBA SC YALALA 2-1 KWA MBEYA CITY

BEKI Nassor Masoud ‘Chollo’ amekosa penalti dakika ya mwisho, Simba SC ikilala 2-1 mbele ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Chollo alipiga penalti hiyo ikagonga mwamba wa juu dakika ya 90+3 baada ya beki Yussuf Abdallah kumchezea rafu kiungo Jonas Mkude kwenye boksi.

Chollo alifanya kosa hilo, Simba SC ikitoka kufungwa bao la pili kwa penalti pia na Yussuf Abdallah baada ya kipa Peter Manyika kumshika miguu Raphael Daudi dakika ya pili 90+2.  

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambua wa Shinyanga aliyesaidiwa na Anold Bugado wa Singida na Yahya Ali wa Mara, hadi mapumziko tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

BAADA YA ZITTO KABWE KUGOMA KUSOMA TAARIFA YA PAC BUNGENI ATOA SABABU

https://zittokabwe.files.wordpress.com/2012/04/zkwasanii2.jpgZitto Kabwe- "Kwanini sikwenda kusoma taarifa ya PAC leo nilipoitwa na Spika? Jibu rahisi kabisa, siwezi kuona madhila na uvunjifu mkubwa wa HAKI za binaadamu nikaendelea na mambo kama hakuna lililotokea. Kitendo cha polisi kutumia nguvu, kupiga raia hovyo na kumdhalilisha Kiongozi wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote".

MADIWANI WA MANISPAA YA TEMEKE WAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Madiwani wa Manispaa ya Temeke wakikagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa maabara ya shule za sekondari na barabara
 Madiwani wa manispaa ya Temeke wamefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo ujenzi wa maabara,  afya na miundombinu ya barabara mbalimbali katika manispaa hiyo ya temeke.

Ziara hiyo ambayo ina lengo la kujiridhisha na utendaji na maendeleo yanayoendelea katika kutekeleza ahadi za serikali imefanyika kwa mafanikio makubwa na kutoa fursa kwa madiwani hao kukagua na kuona wenyewe kasi ya maendeleo katika manispaa yao ya temeke.
Hapa kuna picha kadhaa kuhusi ziara hiyo

DRFA YAWAOMBA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU KUJITOKEZA KWA WINGI MICHEZO YA TAIFA CUP

2
Uongozi wa chama  cha soka mkoa wa Dar es salaam,DRFA,umewaomba,mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya kandanda,kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam zinazoshiriki ligi kuu,Daraja la kwanza na michuano ya taifa Cup wanawake ,ili kutoa hamasa kwa wachezaji.
Leo (januari 28) kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi kuu kwa timu ya Simba ya Dar es salaam dhidi ya Mbeya City ya Mbeya,mchezo ambao utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini.
Itakumbukwa kwamba katika mechi mbili za ligi msimu uliopita,Simba na Mbeya City hakuna aliyefanikiwa kumfunga mwenzake,na kujikuta wakiambulia sare ya 1-1 kule uwanja wa Sokoine,na ule wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa taifa nao kwenda sare ya 1-1.

SINTOFAHAMU BUNGENI MUDA HUU,KISA NI LIPUMBA


          Kufwatia sakata la mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF  profesa  Ibrahim lipumba Jana kukakamwa na kupigwa katika maandamano ya chama chake huko temeke sakata hilo limetua bungeni asubuhi hii na kusababisha bunge kahirishwa kutokana na wabunge wa upinzani kuwasilisha hoja ya kuahirisha shughuli za bunge.kujadadili jambo la dharura lililojitokeza.

           Akiwasilisha hoja hiyo mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI JAMES MBATIA ameliomba bunge kutoka na uzito wa jambo hilo na ukizingatia heshima aliyo mayo lipumba na kitendo alichofanyiwa paMoja na kutii amri ya polisi ni kitendo cha kihuni na hakivumilki hivyo bunge lijadili jambo hilo.

Mheshimiwa MBATIA amesema kuwa  Lipumba ni mwenyekiti wa chama ambacho kina wabunge zaidi ya 30 huku bungeni,lipumba ni mwenyekiti wa chama ambacho kinashiriki serikali ya umoja wa kitaifa huko zanzibar,haiwezekani atendendewe kitendo kama kile kilichotokea jana,naomba mwongozo wako spika ili tusitishe mambo ya leo na tujadili jambo hili ambalo ni kubwa na haliwezi kufumbiwa macho
.
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo wabunge wa upinzani walisimama ishara ya kuunga hoja mkono hapo ndipo spika makinda alipowataka wakae na swala hilo litapatiwa majibu na serikali hapo kesho.

Baada ya majibu hayo wabunge wa upinzani hawakuridhika na wakaendelea kusimama hadi spika akaamua kulisitisha bunge hadi SAA kumi Leo.


Tuesday, January 27, 2015

HOFU YATANDA MBAGALA,LIPUMBA AKAMATWA,NI MAANDAMANO YA CUF

HABARI zilizotufikia mda huu zinasema Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam limetumia nguvu kwa  kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchama cha Wananchi CUF waliokuwa kwenye maandamo wilaya ya Temeke .
Na kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi waandamizi wa chama cha Wananchi CUF,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba,huku wananchi wa maeneo hayo wakiishi kwa hofu kubwa sana.

Akithibitisha kukamatwa viongozi hao pamoja na kuvunjwa kwa maandamano .Afisa Habari wa chama cha Cuf ,Bwana Silas  alipoongea na mtandao huu  amesema waalianza maandamano ya Amani katika Viwanja vya temeke na kwenda mbagala , ambapo maandamano hayo yaliokuwa na lengo la kumbukumbu ya mauaji ya wanachama wao yaliofanyika  TAREHE 26 januari mwaka  2001 huko Zanzibari na Tanzania Bara,
     

HOJA YA KUWAPIMA AFYA WAGOMBEA URAIS YAANZA KUSHIKIWA BANGO,JUKATA NAO WASEMA YAO

Mwenyekiti wa jukwaa la kitiba nchini (JUKATA) Deus Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi leo
NA KAROLI VINSENT


  HUKU zikiwa zimebaki miezi michache tu,kabla ya kipenge akijapulizwa ili kuashiria Kampeni za Uchaguzi wa Mwaka 2015 kuanza,Nao Jukwaa La Katiba nchini JUKATA,limeibuka na kusema Serikali iwapime afya wagombea wa urais kabla ya hawajaenda kwa wananchi ili kuliokoa Taifa  lisiingie kwenye matatizo ya kufa marais  kama yalioikumba nchi Jirani ya Zambia,Ambao wao waliitisha uchaguzi Mkuu baada ya kufariki Michael Chilufya Satta
   
            Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa jukwaa la kitiba nchini (JUKATA) Deus Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambao uliitishwa mahususi kuzungumzia hali ya uchaguzi uliomalizika nchini Zambia ambapo Jukwaa hilo la Katiba liliwakilisha  mwavuli wa asasi za kiraia 184,waliokuwa nchini Zambia wakiangalia mwenendo wa uchaguzi huo,ambapo pamoja na Mambo mengine Kibamba-
           Alisema kuna haja ya watu wanaojitokeza katika nafasi ya kuwania Urais wakapimwa afya zao mapema kabla hawajaruhusiwa kugombea nafasi ya Urais.

TIZAMA VIJANA WA CHADEMA WALICHOKIFANYA HUKO MUFINDI KASKAZINI

WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa ali
yekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI
 Makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la mufindi kasikazini
WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwahutubia wananchi wa jimbo la mufindi kusini ambako anatarajia kugombea ubunge kupitia Chadema.

BOMU LINGINE KULIPULIWA BUNGENI,NI BAADA YA LILE LA ESCROW

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)  itawasha moto upya bungeni wakati itakaposoma ripoti maalumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikitarajiwa kuibua kashfa tatu nzito ikiwamo ya misamaha ya kodi.
Kashfa nyingine zinazotarajiwa kuibuliwa kesho ni, ufisadi katika gharama za ujenzi wa jengo la watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na uuzaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe zilisema kuwa, tayari kamati hiyo imepokea ripoti ya ukaguzi huo ambayo inaonyesha ufisadi wa kutisha katika maeneo hayo matatu na mengineyo.
Masuala hayo matatu pia yaliibuka wakati wa vikao vya kamati za Bunge vilivyomalizika Dar es Salaam wiki iliyopita, huku bodi ya korosho ikibanwa kuhusu nyumba yake aliyouziwa Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Silvestry Koka.

USIKOSE HII KUTOKA DAR ES SALAAM LEO

Aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni aziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizungumza na wadau mbalimbali walojitikeza katika afla hiyo ya kutafuta fedha za kuendesha mkutano huo utakao fanyika mapema mwezi wa tatu
 Taasisi ya kimataifa ya uhudumiaji wa bidhaa na uchukuzi wa bidhaa CILT yani THE CHARTERD INSTITUTE OF LOGISTIC AND TRANSPORT Tawi la Tanzania imeandaa mkutano mkubwa nchini ambao utafanyika katika mkoa wa arusha tarehe 3 na 4 mwezi wa tatu mkutano wenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kujadili changamoto mbalimbli katika secta hiyo.
Mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE MAKUKE akizungumza kuhusu mkutano huo na taasisi hiyo inavyofanya kazi. 
 Mkutano huo ambao utafanyika katika hoteli ya mount meru jijini arusha una mipango pia ya kuwakutanisha wanataaluma wa maswala ya uchukuzi na usafirishaji wa bidhaa ili kubadilishana uzoefu katika taluma hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupata chai yenye lengo la kuchangisha fedha ambazo zitasaidia katika kuendesha mutano huo aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikian wa Africa mashariki MH HARSON MWAKYEMBE amesema kuwa Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa kama huu ni fursa ya kipekee ambayo nchi inatakiwa kujivunia na kuitumia kujitangaza kimataifa.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza.
 Amesema kuwa mkutano huo utawasaidia hasa vijana ambao wanasoma maswala haya kukutana na wazoefu katika fani hiyo na kubadilishana uzoefu jambo ambalo litawajengea uzoefu katika kazi zao pindi watakapoingia katika fani.
Aidha mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE MAKUKE anesema kuwa kwa sasa katika secta ya usafirishaj wa bidha nchini kumekuwa na watu ambao amewaita makanjanja ambao wamekuwa hawana weledi katika kazi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi jambo ambalo amesema kuwa linafaa kupigwa vita mara moja.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza katika hafla hiyo amewataka watanzania hususani wadau wa secta hiyo kujitoa katika kuufadhili mkutano huo kwani una manufaa makubwa katika ukuaji wa secta ya usafirishaji na uchukuzi nchini Tanzania

Picha tatu za juu zikionyesha washiriki mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo

Monday, January 26, 2015

TAARIFA MUHIMU TOKA DRFA LEO


http://2.bp.blogspot.com/-efmpN9l5Ow4/UV6TScJEzDI/AAAAAAAAUTA/NNuRUEqVBQw/s1600/BALL.png

PANAMA FC,BOOM FC,KUANIKA 18 BORA  LIGI YA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mechi ya kiporo katika michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam kati ya klabu za Panama FC dhidi ya Boom FC, itapigwa kesho kwenye uwanja wa Airwing,ukiwa ni mchezo ambao utatoa fursa kwa DRFA kutangaza timu 18 zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya 18 bora ya michuano hiyo.

Michuano hiyo ya ligi mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,inaingia katika hatua ya mwisho katika hatua ya mwisho ambayo itatoa wawakilishi wa mkoa Dar es salaam katika ligi ya mabingwa wa mikoa ya TFF.

Kivumbi cha hatua ya 18 bora,kitaanza kutimka tarehe 4 /02/2015.

LIGI YA WANAWAKE YA MKOA WA DAR ES SALAAM.

ESCROW--NCCR MAGEUZI WATAKA RUGEMALIRA NA KINA TIBAIJUKA WAKAMATWE MARA MOJA


Katibu mkuu wa NCCR-MAGEUUZI,ndugu, MOSENA NYAMBABE akizngumza na wanahabari mapema leo
          Chama cha NCCR-MAGEUZI kimeshangazwa na hatua za kuwapeleka mahakamani watu kadhaa ambao wanahusika katika kupokea mapesa ya ESCROW huku mtoa rushwa akiranda mitaani bila kukamatwa kwa kosa la kutoa rushwa.

Akizungumza na wanahabari leo mapmaa jijini Dar es salaam katibu mkuu wa chama hicho MOSENA NYAMBABE amesema kuwa chama chake kinapenda kujua ni kwanini wanaotuhumiwa kupokea rushwa za amana ya TEGETA ESCROW wanafikishwa mahakamani lakini anayetuhumiwa kutoa rushwa kupitia amana ya TEGETA ESCROW ambaye ni JAMES RUGEMALIRA hachukuliwi hatua yoyote hususani ya kupelekwa mahakamani.

Aidha amesema kuwa pia watua ambao wamewajibishwa na wengine kujiondoa wenyewe kama profesa ANNA TIBAIJUKA,ENDREW CHENGE,WILLIAM NGELEJA,VICTOR MWAMBALASA na DANIEL YONA , PAUL KIMITI na wengine waliotajwa kupokea pesa hizo wanastahili kukamatwa na kufikishwa mara moja mahakamani kwani nao ndio chanzo cha tatizo hilo.

Aidha chama hicho kimesema kuwa kinasikitishwa na hatua ya chama cha mapinduzi CCM kuwafumbia macho mafisadi hadi hapo wananchi wanapowafichua na ndipo nao huibuka na kuchukua hatua kitu ambacho kinaonyesha kuwa chama hicho kina ajenda ya siri na wahujumu uchumi wa Tanzania.