Tuesday, March 31, 2015

MAGAZETI YA LEO APRIL 01.2015,YAKO HAPA


MANENO MAZITO ALIYOYATOA GWAJIMA JANA BAADA YA KITINGA POLISI

 Baada ya jana askofu gwajima kutoka hospitali alipokuwa amelazwa na kufika kituo cha polisi kinondoni kwa ajili ya kutoa maelezoamesema haogopi kulitetea Tamko lilotolewa na jukwaa la kikristo nchini ambalo linawahamasisha waamini wa dini hiyo-
       Kuipigia kura ya Hapana Katiba iliyopendekezwa na Bunge  Maalum la katiba,ambapo amesema atalipinga hata kama serikali ikimwekea vikwazo.
           Kauli kiongozi wa huyo wa Kiroho ameitoa jana kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo alipojisalimisha ili kuhojiwa  mara mwisho baada ya kutoka kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam alupolazwa kutokana kuugua gafla wakati akiwa kwenye mahojiano na Jeshi la polisiwiki iliyopita.
     
      Akiongea na waandishi wa Habari kwa kujihami mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi Wilaya kinondoni na kupewa Dhamana na kituoni hapo huku wakijazana waamani wake waliojitokeza na kumpokea Askofu wao.ambapo amesema hawezi kutishika wala kuyumbika kutokana na vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea anaodai wakristo nchini ambao wamewekewa Katiba anayoiita ni mbovu.
         “Mimi nimetoka kwa amani nashukuru sana mungu animeponya salama,ila nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao anakandamizwa na mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
          Askofu Gwajima ameongeza kuwa kwa kuwataka viongozi wenzake kuheshimu tamko la Jukwaa la Kikristo na hata  yeye mwenyewe amesema ataliheshimu sana.
        “Nawaamomba viongozi wa dini wenzangu tuliheshimu Tamko hili la kikristo,na endapo tukiwa tofauti tutakuwa tunakwenda tofauti na tunajivunjia heshima kwa jamii ambapo tulionekana kuwa na msimamo mmoja wakati tukilitoa na mimi mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho”ameongeza Gwajima.
           Alipoulizwa na waandishi wa Habari kuhusu Afya yake amesema hawezi kuzungumzia Afya yake akasema mwenye ruhusa ya kumsemea afya yake, akawataka waandishi kutoendelea kumuuliza huku akiwataka waamini wake kushangilia kwa ushindi waliupata anadai umetokana na nguvu ya mungu.

TAARIFA KAMILI KUHUSU ASKARI WALIOUAWA HUKO MKURANGA PWANI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliowavamia, kuwauwa askari wawili na kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG.

Tukio hilo limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko barabara ya Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Katika tukio hilo majambazi wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Majambazi hao wakiwashambulia ghafla askari hao kisha kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 ndani ya magazine na kutokomea kusikojulikana.

Majina ya askari wa Wilala ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo:
1.    D.2865 SGT FRANCIS,
2.   E.177 CPL MICHAEL,  
Askari mwingine mwenye namba D.5573 D/SGT ALLY amejeruhiwa kwa risasi kwenye paja la mguu wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya Temeke kwa matibabu. Askari huyu kabla ya kujeruhiwa alipambana vikali na majambazi hayo kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo aina ya SMG ambayo pia walishindwa kumpora hivyo wakatokomea kuelekea pori la vikindu.

Katika oparesheni hiyo, nguvu na mbinu zote za kipolisi zitatumuika ambapo vikosi vya Dar es Salaam na Pwani vilianza kufanya oparesheni hiyo mara baada ya tukio ili kuhakikisha kwamba majambazi hao wanapatikana haraka iwezekanavyo.

Pamoja na oparesheni hiyo kali inayoendelea, Jeshi la Polisi linachunguza ili kubaini kama tukio hili linaashilia vitendo  vya ugaidi au ni ujambazi wa kutumia silaha.

Natoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kupitia (dhana ya polisi jamii) kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa hali na mali kwa kutoa taarifa sahihi.

Matukio haya ambayo yamekuwa yakitokea mkoa wa Pwani mara kwa mara ni lazima yakomeshwe ili kuhakikisha kwamba havijirudii.

KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO KIJANA,DC MAKONDA AJA NA HII NJEMA KWA VIJANA SASA,USIPITWE

Mkuu wa wilaya ya kinondoni DC PAUL MAKONDA akizngumza nna wanahabari mapema leo juu ya mchakato wa kusaka vipanji kinondoni ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni
 Mnamo tarehe 31 March mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amehitisha waandishi wa habari na kutangaza kuwa ameanzisha Kinondoni Talent Search ambayo itahusika kusaka vipaji vya watoto wenye vipaji kama; Kucheza, Kuimba, Kuchekesha na vingineo.
Akizungumza na waandishi wa leo alisema; Kinondoni Talent Search ni mpango wenye lengo kuu la kuwatambua vijana waishio kwenye wilaya ya Kinondoni wenye vipaji vya kuimba, Kuchekesha ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi jambo linalowafanya kushindwa kuonesha vipaji vyao mwisho ndoto zao kufifia.Hivyo, lengo kuu la mpango huu ni kuwawezesha kupata njia za kutimiza ndoto zao kupitia uwezo wao
Mwimbaji maarufu ambaye ni mmoja kti ya wanakamati wa mashindano hayo PETER MSECHU mzaa wa SOPHIA REMIX akizngumza na wanahabari leo
 Kwa ufupi ni kwamba, Kinondoni Talennt Search inalenga kwanza, kuwatengeneza nafasi za mafanikio vijana wenye vipaji, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu waliopo kwenye sekta zao.Lakini kubwa zaidi, kutoa hamasa kwa vijana wote wa Wilaya ya Kinondoni na Tanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuendeleza vipaji vyao, kuepuka mambo yanayoweza kuviua na kuharibu malengo yao ya baadae, mfano matumizi ya dawa ya kulevya, ngono zembe na vitendo vya uporaji.Bila kusahau kuwakumbusha vijana wote kuwa ukimiliki kipaji unakuwa ajira, ni kujua tu namna ya kukitumia ili kikufae na kukufikisha utakapo, na ndio maana kauli mbiu ya mpango huu nikipaji chako, ajira yako’ alisema.
Msanii wa vichekesho mc PILIPILI naye alikuwepo
Ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa kwa kiwango cha juu na kufikia lengo, Paul Makonda ametengeneza kamati maalumu yenye wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na baadhi ya wasanii ambao wana uzoefu zaidi katika nyanja ambazo tunazigusa kwenye mpango huu.

1.Jumanne Mrimmy – Afisa utamaduni (Manispaa ya Kinondoni)
2.Sebastian Mhowera – Afisa Uhusiano – (Manispaa ya Kinondoni)
3.Peter Msechu – Msanii wa Bongo Fleva
4.Jokate Mwegelo – Mwimbaji/Mbunifu
5.Mc-pilipili -Mchekeshaji


MPYA--MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA SINZA HAPA,TIZAMA KINACHOENDELEA

Unaweza ukadhani kama hapa kuna mvua kuibwa sana ya mafuriko katika eneo hili lakisi sio kweli,hapa ni Dar es salaam sinza eneo la africasana ambapo moja ya chemba za maji ipepasuka mchama huu karibu kabisa na makazi na maduka ya watu,hali ya kiafya katika meeneo haya ni mbaya na maeneo makubwa sana yapetapakaa maji machafu na watu imebidi wakimbie maeneo yao ya kazi ili kukwepa adha hii kubwa,msaada wa haraka unahitajika kutoka kwa viongozi wa maeneo haya,ni karibu kabisa na kituo cha daladala cha sinza africasana lakini maji yametapakaa hadi maeneo ya bamaga kukizunguka chuo cha ustawi wa jamii hapa bamaga,wananchi wanaomba msaada waharaka ili kuokoa afya zao pamoja na hali ingine.
Kama Mnavyoona maji nji mengi kiasi kwamba hadi magari sasa yanaanza kupata matatizo katika barabara hiyo kutokana na wingi wa maji hayo.PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI

Hapa ndipo maji hayo yanapotoka ni chemba ambayo imepasuka muda mfupi uliopita lakini maji yake ni mengi kiasi kwamba yanaleta shida kubwa katika maeneo haya

Monday, March 30, 2015

MAGAZETI YOTE YA LEO JUMANNE MARCH 31,2015 YAKO HAPA

GWAJIMA MOVIE-LIPUMBA AMTEMBELEA HOSPITALINI


 Profesa Ibrahim Lipumba,mchana wa Leo tarehe 30/03/2015, amemtembelea Askofu Josephat Gwajima aliyelazwa TMJ Hospital Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima aondolewa katika chumba cha uangalizi Maalum (ICU) TMJ baada ya kupata nafuu na hali yake kuendelea vizuri.


Picha za Prof Ibrahim alipomtembea Askofu Gwajima Hospitalini



TAARIFA MPYA KUHUSU WALE WALIOTAKA KUMTOROSHA GWAJIMA JANA


TAARIFA YA NYONGEZA/UFAFANUZI YA TUKIO LA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA AKIWA HOSPITALI


Leo tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe 29/03/2015. Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za Short Gun.
Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:

TENGA, MALINZI WAZUNGUMZIA UCHAGUZI WA CAF, FIFA



Leo Rais wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) akiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wamezungumzia uchaguzi wa CAF na FIFA.

Rais Tenga ameishukuru familia ya TFF kwa kumuunga mkono katika kugombea tena nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF katika uchaguzi utakaofanyika Aprili 7 mwaka huu Cairo. Tenga ni mgombea pekee wa nafasi hiyo kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

WAZIRI LAZARO NYALANDU AHAMASISHA ELIMU KWA WATANZANIA

Wanajumuiya ya wanafunzi waliosoma katika shule ya Ilboru wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipokuwa akiwahutubia katika chakula cha hisani cha kuchangia ukarabati majengo ya shule hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa kitengo cha Masoko Mfuko wa Pensheni cha GEPF, Aloyce  Ntukamazina, akizungumzia unufaikaji wa mafao ya mfuko huo [pindi unapojiunga nao wanajumuiya ya wanafunzi waliosoma katika shule ya Ilboru waliokutana katika chakula cha jioni kuchangia ukarabati wa majengo ya shule hiyo yaliyochakaa kupita kipimo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki. 

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, akiwahutubia wanafunzi wenzake waliosoma katika shule ya Ilboru ya Arusha katika chakula cha usiku kilichoandaliwa rasmi kuchangia ukarabati wa majengo cha shule hiyo . Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. .


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA KONGAMANO LA 3 LA VIJANA WA TANZANIA NA CHINA, JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake jana Machi 29, 2015 wakati akifunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China kuhusu masuala ya Uongozi, wakati alipokuwa akiwasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto kufunga kongamano hilo jana Machi 29, 2015. Picha na OMR


Meza kuu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika, Chen Lin, baada ya Makamu kufunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakati akiondoka ukumbini hapo baada ya kufunga rasmi Kongamano la tatu ya Viajana wa Tanzania na  China, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Picha na OMR

KUHUSU KAFULILA NA ACT LEO,SOMA HAPA


Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, amekanusha kuhamia chama cha kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).


Kafulula amesema kuwa hana sababu ya kuhama chama hicho na kukiri kuona katika mitandao ya kujamii habari kuwa anahama chama chake na kuhamia ACT jambo ambalo halina ukweli wowote.
Amesema kuwa huenda tetesi hizo zimekuja baada ya kuwa na marafiki wengi wa chama hicho na kusema kuwa urafiki na wanachama hao hauna maana kuwa anahamia chama hicho.
Hata hivyo Kafulila amehoji ana urafiki na wanachama wa Chadema, CCM, na vyama vingine mbona hawajavitaja, na kudai kuwa Zitto, amehama kutokana na kuwa na migogoro na chama chake lakini yeye hana sababu ya kuweza kukihama chama chake.
Ameongeza kuwa atabaki kuwa Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, na kuendelea na kampeni za kujenga chama hicho ikiwemo yeye kurudi bungeni pamoja na chama hicho kuongeza wabunge wengi zaidi.

Sunday, March 29, 2015

FASTJET WAZINDUA SAFARI MPYA-SASA NI KUTOKA KILIMANJARO HADI MWANZA,NA KILIMANJARO KWENDA ENTEBE UGANDA

Meneja   Mkuu wa Shirika  la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akimkabidhi tiketi mwandishi wa habari toka gazeti la  Jamboleo, Richard Mwangulube aliyeshinda zawadi ya tiketi ya bure ya kusafiri kwenda Mwanza nakurudi Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa safari mpya wa shirika hilo toka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Kilimanjaro kwenda Entebe Uganda hafla hizo zilifanyika Mkoani Arusha leo


Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akimkabidhi tiketi mwandishi wa habari toka Radio 5 Linus Kilembu aliyeshinda zawadi ya tiketi ya bure ya kusafiri kwenda Mwanza nakurudi Kilimanjaro wakati wauzinduzi wa safari mpya wa shirika hilo toka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Entebe Uganda hafla hizo zilifanyika Mkoani Arusha .

Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akimkabidhi tiketi mwandishi wahabari toka gazeti la East African Business Week ,Elisha Mayallah aliyeshinda zawadi ya tiketi ya bure ya kusafiri kwenda Mwanza nakurudi Kilimanjaro wakati wauzinduzi uliofanyika  Mkoani Arusha wa safari mpya wa shirika hilo toka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Entebe Uganda.

Meneja Mkuuwa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akiongean awandishi wahabari Mkoani Arusha leo wakati wauzinduzi wa safari mpya ya ndege ya Fastjet kutoka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Kilimanjaro kwenda Entebe Uganda, pembeni yake kuliani Lucy Mbogoro Afisa Mahusiano na Masokona kushoto ni Neema David Afisa Biashara wote toka shirika hilo.

Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akimkabidhi tiketi mwandishi wahabari toka Tbc Sechelela Kongola aliyeshinda zawadi ya tiketi ya bure ya kusafiri kwenda Mwanza nakurudi Kilimanjaro wakati wauzinduzi wa safari mpya washirika hilo toka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Kilimanjaro kwenda Entebe Uganda hafla hizo zilifanyika Mkoani Arusha 

HIVI TCRA IPO AU IMEKUFA---AMKENI MCHUKUE HATUA

11039142_10200327749914253_7953568182828634952_n
“Screen shot” ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog uchwara kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika habari za uongo, matusi
………………………………………………………………………………………………
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa mambo ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine mengi, Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo wanayoyatumia vibaya.
Kupitia BLOG, mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa ama kufanyaia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote anaweza kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha BLOG hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazosi za kweli.
Tunaamini wapo watu wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha ya kuwa si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii, kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi? Jamani kweli hii ni haki?, tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama kinakiuka maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
1
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma.
Tunaamini Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.
Tukumbuke huko nyuma kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua ambapo walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa wanaweka picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za viongozi wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si mambo.
Hivyo ni wakati sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili ikiwemo kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe hatua.
Mtandao huu unaamini kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye miongoni mwa blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?” wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana wanaapokutana na habari kwenye hizo blog uchwara.
Wadau waliochangia mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha…. hili ndiyo tatizo kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger and a self-appointed journalist… UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka kichefu chefu… full of attention-seeking sensationalism… utakuta heading: HATARI, Vilio na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu kutaka watu wazisome blog zao.” Alieleza Mahundi.
Hata hivyo wachangiaji wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya ICT ili kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
IMG-20150310-WA0045
Modewji blog tunaamini pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo kwani kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi bomu likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.
Hata hivyo, mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana na TCRA na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!.
Tuandikie maoni yako kupitia kwenye mtandao huu hapo chini ama kupitia simu 0719076376 au 0714940992