Sunday, May 31, 2015

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNE 01,2015,YAKO HAPA

SOMA SAENTENSI 23 ZENYE MATUMAINI ALIZOTOA NCHEMBA WAKATI AKITANGAZA NIA YAKE


1.Mwigulu: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwaajili ya nchi yetu

DIWANI WA CCM AWASHUKURU MABALOZI KATIKA KATA YAKE KWA KAZI KUBWA WANAYOFANYA

Diwani wa kata ya Ndugubi iliyopo katika Jimbo la Kinondoni Mh CHARLES MGONJA akizungumza na mabalozi wa mitaa mbalimbali waliojitokeza katika kikao hicho ch pamoja cha kujadili maswala mbalimbali ya maendeleo yanayofanyika katika kata yao.kikao ambacho kilifanyika katika shule ya secondary Turiani

 Diwani wa kata ya Ndugubi iliyopo katika Jimbo la Kinondoni mh CHARLES MGONJA leo amekutana na mabalozi wote waliopo katika kata yake kwa lengo la kuwakutanisha kwa pamoja kujadili  kuhusu kazi ambazo zinafanywa na diwani huyo pamoja na kuwashukuru madiwani hao kwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa mambo ya maendeleo katika kata hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu nje ya mkutano huo amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa mbalozi hao kuwa wamekuwa hawapati nafasi kama hiyo ya kukutana na kujadili kwa pamoja na viongozi walio juu yao pamoja na kazi kubwa wanayoifanya,jambo ambalo limemsukuma kuwakutanisha mabalozi hao kujadili kwa pamoja na kuelewa kila kitu ambacho serikali yao inakifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Mabalozi mbalimbali waliojitokeza katika kikao hicho
Amesema kuwa ufanisi wa kiongozi wa ngazi za juu za serikali hauwezi kuwa na maana kama hauna mahuziano mazuri na viongozi wa ngazi za chini za wakiwemo mabalozi hao kwani ndio wanaohakikisha kuwa katika mitaa yote kunakuwa na ulinzi wa kutosha na kuimarisha amani katika maeneo yote ya kata hizo.

TIGO YADHAMINI MASHINDANO YA MBUZI DAR ES SALAAM

  1. Watoto wakicheza katika puto maalum la Tigo (Jumping Castle) wakati wa tamasha la mbio za Mbuzi (Goat Race) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Vijana wakiingiza Mbuzi katika eneo la kukimbilia wakati wa tamasha la mbio za Mbuzi (Goiat Race) lilofanyika jijini Dar es Salaam

  1. Vijana wakikimbiza Mbuzi ili kupata mshindi wa mbio hizo wakati wa tamasha la mbio za Mbuzi (Goat Race) lillilofanyima Dar es Salaam.

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo John Wanyancha akikabidhi hundi kwa mmiliki wa Mbuzi aliyeshinda, Mark Golding kutoka kampuni ya PM Group

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, John Wanyancha akipata huduma katika banda la Tigo, wakati wa tamasha la mbio za mbuzi (Goat Race), zilizofanyika Jijini Dar es Salam ili kukusanya pesa za kusaidia jamii

TIZAMA ALICHOKIFANYA TENA DK SLAA ZIARA YAKE


Katibu Mkuu Dk. Slaa yuko katika ziara ya kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura linavyokwenda na kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu; ambapo pia anakagua maandalizi ya chama kwenda kushinda uchaguzi kwa kushirikiana na vyama washirika wa UKAWAHapa ni Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma ambapo Dkt. Slaa amehutubia mkutano mkubwa wa kihistoria kuwahi kufanyika mjini hapo.
 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA MARIAN BAGAMOYO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo,  kwa pamoja wakikata utepe kuzindua Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, kwa pamoja wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu, katika Ibada maalum ya uzinduzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian, baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo Mei 31, 2015 mjini Bagamoyo. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, baada ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo na baadhi ya viongozi na waumuini  baada ya kuzindua rasmi Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkandarasi wa majengo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian wakati akitembelea kujionea ramani ya Chuo hicho baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo mjini Bagamoyo. Picha na OMR

WASIRA ALIPUKA,AMPIGA KIJEMBE KIAINA LOWASA,ATANGAZA NIA YA KWENDA MAGOGONI


Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, amnabe pia ni Mbunge Bunda mkoani Mara, Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia baadae mwaka huu.


Katika hotuba yake ya takribani dakika 60 mh WASIRA ametumia muda mwingi kukemea vitendo vya rushwa hiuku akiwahmiza wananchi kumchagua kiongozi ambaye hatawaibia mali zao na badala yake wamchague mtu ambaye atawatumikia watanzania.

Saturday, May 30, 2015

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 31,2015 YAKO HAPA

PICHA 50-ALICHOKIFANYA LOWASA HUKO ARUSHA LEO ZIKO HAPA

 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.

TIZAMA DK SLAA ALIVYOANZA ZIARA YAKE,AKABIDHIWA UCHIFU

Kiongozi wa Machifu wa Kabila la Wanyiha, Greenwell Msangawale akimvisha vazi maalum la kichifu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa na kupewa jina 'Mwene wa Mbozi' ambapo pia alikabidhiwa silaha ya jadi aina ya mundu wakimtuma kazi ya kuendeleza vita dhidi ya ufisadi na ubadhirifu nchini ambao umekuwa moja ya sababu za umaskini wa Watanzania. Tukio hilo limefanyika kwenye Uwanja wa Ichenjezya, Vwawa, wilayani Mbozi, Mkoa wa Mbeya ambapo kiongozi huyo amefanya mkutano wa hadhara baada ya kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR. 

TIZAMA ATAKAPOSIMAMA LOWASA LEO KUZUNGUMZA NA WATANZANIA

Kama hujui kinachoendelea ni hivi waziri mkuu wa zamani wa Tanzania mh EDWARD LOWASA leo anatarajia kutangaza nia yake ya kuwania urais wa Tanzania katika viwanja vya sheik Amri Abeid Mkoani arusha,tukio hilo ambalo linatarajia kuweka historia mpya linasemekana kuwa litarushwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania live.Hapa nimekuwekea picha kadhaa za muonekano wa uwanja huo ambao utafanyika shughuli hiyo picha hizi zimepigwa majira ya asubuhi,ntakuwa nakupa kila kinacheendelea katika viwanja hivyo

Friday, May 29, 2015

WAISLAM--HATUHUSIKI HATA KIDOGO NA UGAIDI UNAOENDELEA AFRICA,SOMA HII

Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA akizungumza na wajumbe mbalimbali kutoka dini zote waliohudhuria katika kikao hicho Jijini Dar es salaa kikao kilichikua na lengo la kujadili kwa pamoja hatma ya bara la africa na ugaidi unaoendelea humo
Imeelezwa kuwa vitendo vya ugaidi na mauaji yanayofanywa na watu mbalimbali barani  Africa na duniani kwa ujumla hayahusiani hata kidogo na dini ya kiislam kama ilivyokua ikielezwa na wadau mbalimbali kuwa mauaji hayo yanahusiana na imani ya dini ya kiislam.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dare es salaam na kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA wakati akizungumza katika kikao cha pamoja cha viongozi wa dini zote kikao kilichoandaliwa na chuo cha kidini cha IMAM JAFAR SWADIQ,kigogo Jijini Dar es salaam.
Muwakilishi wa wakiristo katika mkutano huo pastor PRINCE ERASTO IKONGO kutoka pentecoste akizngumza katika kikao hicho ambapo amewataka waumini wa dini za kikristo kuondoa hofu juu ya waislam padala yake wadumishe umoja na amani iiyopo nchini
Amesema kuwa ugaidi katika bara la Africa umekuwa ukitafsiriwa kuwa ni jambo ambalo limekuwa katika msukumo wa dini ya kiislam jambo ambalo amesema kuwa watanzania wanapaswa kuelewa sio sahihi kuwatuhumu waislam kwa ugaidi kwani hakuna kitabu chochote kinachoruhusu muislam kufanya mauaji kwa mwadamu mwenzake.
Amefafanua kuwa mivutano na Ugaidi uliyopo barani Africa umekuwa ukisababishwa na mambo matatu ambayo ameyataja kuwa ni ugaidi wa kifikra,kiuwezo na ugaidi wa kudai haki.
Wajumbe mbalimbali wakichangia
Aidha Ameongeza kuwa dini zote duniani hakuna hata ushaidi wa dini moja ambayo inaruhusu ama kushabikia vitendo vya mauaji ya kigaidi yoyote yanayotokea afrika..
Katika hatua nyingine sheikh JALALA akizungumzia swala ambalo limekuwa likitamkwa na serikali kuwa viongozi wa dini ya kiislam wamekuwa wakiwafundisha vijana wao wa mbinu na njia za ugaidi ameitaka serikali kuacha kauli hizo kwani ni kauli za kichochezo na zisizo na ushahidi wowote na badala yake wafwatilie swala hilo kiundani pasipo kuitaja dini yoyote kuhusika.
Akizungumza katika kikao hicho muwakilishi wa wakiristo katika mkutano huo pastor PRINCE ERASTO IKONGO kutoka pentecoste Tabata amesema kuwa viongozi wa dini za kikiristo wamekuwa na hofu kubwa juu ya ndugu zao ambao ni waislam hofu ambayo wamejengewa kuwa viongozi wa dini za kiislam pamoja na waumini wao ni watu wa mauaji na ugaidi jambo ambalo amewatoa wasi wasi wakristo na kuwataka kujenga umoja na mshikamano juu ya waislam na dini zote Tanzania ili kuidumisha amani ya nchi.

Amesema kuwa hofu iliyojaa miongoni mwa viongozi wa dini za kikristo ni hofu ambayo imejengwa na wanadamu kuwa waislam ndio wanaohusika na mauaji mbalimbali ambayo yanatokea duniani ya kigaidi jambo ambalo linapaswa kufutika miongoni mwa wakristo ili waweze kudumisha umoja wanchi.

Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es salaam Ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya ukombozi wa bara la Africa kilikua na kauli mbiu ya TUUNGANE KWA PAMOJA KUUPINGA UGAIDI AFRICA ambapo kimehudhuriwa na viongozi kutoka dini zote huku lengo kuu la kikao hicho likiwa ni kujadili kwa pamoja maswala ya ugaidi barani Africa na kuona ni njia gani zinazoweza kutumika kuondokana na tatizo hilo.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 30,2015 YAKO HAPA


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA LEO

bi1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiteremka kwenye Ndege walipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mtoto Ernest Nkayala alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Elin Mwandobo alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
(Picha na OMR)

TIZAMA RATIBA YA DK SLAA KUANZIA KESHO ANAVYOIZUNGUKA TANZANIA


Kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma wa Watanzania kuwa Katibu Mkuu, Dk. Willibroad Slaa atafanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi, ambapo atakuwa na shughuli kadhaa, ikiwemo kukagua mwenendo wa uandikishaji wa wapiga kura unaofanyika kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR).

Thursday, May 28, 2015

TIGO NA HUAWEI ZATOA MSAADA WA KOMPYUTA 10 NA HUDUMA YA INTANETI KWA SHULE YA MSINGI CHUDA MKOANI TANGA

ta1
Meneja Mahusiano kwa Umma wa kampuni ya Huawei Jin Liguo akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga, Msaada huo ulitolewa na Kampuni ya Tigo kushirikiana na Kampuni ya Huawei. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles ,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Chuda Omari Masukuzi na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula.
ta2
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles akikabidhi msaada wa  Kompyuta zenye intaneti ya bureya Tigo kwa  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chuda Mkoani Tanga Bw. Omari Masukuzi hiyo ni moja kati ya kompyuta 10 zilitolewa na kampuni ya Tigo pamoja na Huawei kwa shule hiyo. Wanaoshuhudia wa pili toka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula, Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa Huawei  Jin Liguo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Abdallah Suleiman.
ta3
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga, Msaada huo ulitolewa na Kampuni ya Tigo kushirikiana na Kampuni ya Huawei. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Magalula Said, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Chuda Omari Masukuzi.
ta4
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chuda Mkoanin tanga wakipokea Kompyuta kwa niaba ya wenzao ambazo zilitolewa na kampuni za Tigo na Huawei.
ta5
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
Meneja Uwajibikaji kwa Jamii wa Kampuni ya Tigo Bi. Woinde Shisael akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Abdallah Suleiman wakati wa sherehe za kukabidhi msaada wa kompyuta 10 kwa  shule ya msingi Chuda Mkoani Tanga leo
ta6
Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga
ta7
Mwalimu wa shule ya Chuda Bi.Teddy Simba akipokea simu kwa niaba ya wenzake toka kwa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula. Simu hizo zitawaweza walimu wa shule hiyo kuweza kuwasiliana wao kwa wao na kuperuzi intaneti  bila gharama yeyote kwa kupitia mtandao wa Tigo.