Tuesday, June 30, 2015

CHANZO KIFO CHA MWANDISHI KAMUKARA--KAULI YA DK MENGI YAIBUA UTATA MKUBWA

Mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi akiaga mwili wa Marehemu Edson Kamukara
Mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi akiaga mwili wa Marehemu Edson Kamukara

KAULI aliyeitoa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dokta Reginald Mengi wakati wa Kumuaga Mhariri wa Gazeti la Mawio pamoja na Mtadandao wa Mwanahalisi Oline Marehemu  Edson Kamukara,Mapya yazidi kuibuka  ambayo yamefichika.(Mtandao huu umedokezwa),Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
     
Kauli hiyo ya Dokta Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT) aliitoa Jumamosi ya wiki iliyopita kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati wa kuaga mwili wa Edson Kamukara,
  
Kwa mujibu wa Dokta Mengi alisema waandishi wa Habari nchini wanaficha ukweli juu ya kueleza sababu ya kifo cha marehemu Kamukara.
    

MABERE MARANDO AWAONYA NEC 'KUTOCHEZEA' BVR DAR ES SALAAM, PWANI
Kufuatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuutangazia umma kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura liliokuwa lianze tarehe 04/07/2015 kwa Jiji la Dar es Salaam na tarehe 25/06/2015 kwa mkoa wa Pwani kwamba limeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa tena; Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda Pwani (Mikoa ya Temeke, Kinondoni, Ilala na Pwani) kinaitaka Tume ifanye yafuatayo: 

GHASIA:HALMASHAURI ZIACHE KUTEGEMEA SERIKALI KUU

Baadhi ya Halmashauri manispaa zimeonywa kuwa na tabia ya kuitegemea serikali kuu na badala yake iwe na vyanzo vya mapato vya ndani kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo katika halmashauri zake.

TIZAMA VIJANA WA MKWASA WANAVYOJIFUA KUWAFWATA UGANDA KWAO STARS KUWAFUATA UGANDA ALHAMIS
Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamis kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika siku ya jumamosi nchini humo.

Mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma nchini Uganda.

“Wachezaji wote waliopo kambini wanaendelea na mazoezi, vijana wanajituma mazoezin, morali ni ya hali ya juu naamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa siku ya jumamosi” alisem Mkwasa.

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamisi jioni kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air) ikiwa na kikosi cha wachezaji 20, benchi la ufundi pamoja na viongozi.

Aidha Mkwasa amesema ataongea na waandishi wa habari siku ya alhamis asubuhi saa 5 kamili - Karume juu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano na kuweka wazi kikosi kitakachosafiri kuelekea nchini Uganda.

Stars imeweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo na inafanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani kila siku jioni kuanzia majira ya saa 10 jioni.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA TBEA YA CHINA, IKULU DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Ofisini kwake, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya TBEA, Zhong Yanmin, wakati alipofika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya TBEA, Zhong Yanmin, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2015 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya TBEA, uliofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 30 2015 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kampuni  ya TBEA, Zhon Yanmin (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2015. Kushoto ni Mkarimani wa Makamu Mwenyekiti huyo. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Ujumbe wa Kampuni ya TBEA, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Ikulu  jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2015. 

MEMBE ALIVYORUDISHA FORM YAKE YA URAIS LEO

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akikabidhi fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rajabu Luhavi alipozirejesha katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Kulia ni Mkewe Mama Dorcas Membe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akizungumza na wanaCCM baada ya kurejesha fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma jana, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Kulia ni Mkewe Mama Dorcas Membe na (kushoto) ni Kada wa CCM, Kapteni mstaafu Alhaj Mohamed Ligola.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rajabu Ruhavi baada ya kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana kurudisha fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Picha zote na John Badi

Monday, June 29, 2015

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNE 30,2015 YAKO HAPA

U-15 YAICHAPA 3-0, KOMBAINI YA MBEYA

 TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kombaini ya vijana chini ya umri wa 17 ya mkoa wa Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi dakika 45 za kwanza zilimalizika U15 wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Timoth Maziku dakika ya 17 kwa guu la kulia akimalizia krosi ya Nahodha Issa Abdi.

Baada ya bao hilo, Mbeya Kombaini walitulia na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa timu ya taifa, hali ambayo ilifanya timu hizo zishambuliane kwa zamu huku pia vijana wakionyesha uwezo wa kuridhisha.

Dakika ya 72, Albinius Haule almanusra aisawazishie bao Mbeya kama si shuti lake zuri la kitaalamu alilopiga kutoka umbali wa mita 25 kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.


Nahodha Issa Abdi aliifungia timu ya taifa bao la pili dakika ya 82 kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya Timoth Maziku kuangushwa nje kidogo ya boksi na Richard Paul.

Emmanuel Ntindi wa Mbeya alijifunga dakika ya 87 katika harakati za kuokoa krosi ya Asad Ally dhidi ya Maziku.

Mchezo ulikuwa mzuri, vijana walionyesha ufundi wa hali ya juu na Mbeya pamoja na kufungwa, walicheza vizuri na kilichowakwamisha kupata japo bao moja ni uhodari wa kipa Kelvin Deogratius wa U15 ya taifa.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana kesho jioni kwenye Uwanja Sokoine na mapema Jumanne U15 watarejea Dar es Salaam na vijana kuvunja kambi hadi watakapokusanyika tena mwishoni mwa mwezi ujao kwa safari ya Zanzibar kwa michezo mingine ya kujipima.


Vijana hao walio chini ya kocha Bakari Shime wanaandaliwa kwa ajili ya kucheza mechi za kufuzu Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2017 na kila wiki ya mwisho wa mwezi watakuwa wakikutana kwa mazoezi na michezo ya kujipima nguvu.

Kikosi cha Mbeya Kombaini kilikuwa; Edward Mwakyusa, Josephat Frank, Seif Gabriel, Emmanuel Ntindi, Richard Paul/Hassam Abdallah dk87, Goodluck Ezeria, Amiri Nyeo, Castro Issa, Albinius Haule, Biya Stephen na Daniel Samson/Castro Moses dk73.

Tanzania U15; Kelvin Deogratius, Kibwana Ally, Faraji John, Maulid Salum, Ally Hussein, Athumani Maulid/Rashid Kilomtola dk75, Robert Philipo/Morris Michael ‘Chuji’ dk86, Asad Ally, Timoth Joseph, Issa Abdi na Juma Zubeiry/Juma Juma dk61.

MSIKITI WA GADDAFI DODOMA WAMSHUKURU MEMBE

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), kwa waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani humo jana, wakati waumini hao walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati waumini hao, walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na  waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati waumini hao walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akibadilishana mawazo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani, wakati waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma, walipomwita jana kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Mkoani humo, Zidikheri Swedy Kheri.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani (kushoto), wakishiriki katika chakula cha usiku kilichoandaliwa na waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi.

SAKATA LA WANAUME WA ROMBO,SASA NI MAANDAMANO KUPINGA KUDHALILISHWA


TIZAMA NYALANDU NA LOWASA WALIVYOHITIMISHA ZIARA ZAO ZA KUUSAKA URAIS LEO

l1
Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Milonge, akionyesha fomu zenye orodha ya majina ya wanachama wa ccm,104,03  waliomdhamini kugombea urais, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa(kulia).
l2
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Kanali Mstaafu, Isaac Mwasongo, akisindikiza na Mwanasiasa Mkongwe, Steven Mashishanga(kushoto) baada ya kuzngumza katika mkutano wa Waziri Mkuu wa zamani,Edward Lowassa, wa  Mkoa wa mwisho wa kupokea majina ya wadhamini kugombea urais
l3l4l6
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa akitoa shukrani katika kuhitimisha Mkoa wa mwisho wa kupokea orodha ya majina ya wadhamini wa kugombea urais
ny1
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakiwa wamezungukwa na umati mkubwa wa watu wakati alipokwenda kuomba udhamini kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida, jana. Katika tukio hilo maelfu ya wananchi walijitokeza kutaka kumdhamini katika harakati zake za kuwania kuteuliwa na CCM kuwania urais. Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo, lakini aliwataka radhi na kuomba kudhaminiwa na wanachama 45 tu kama matakwa ya CCM yanavyoelekeza.

MAUAJI YA MMILIKI WA SHULE YA MTAKATIFU ZION,WATATU MBARONI


WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MMILIKI WA SHULE YA MTAKATIFU ZION

                Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion iliyopo  maeneo ya Ununio, Mbezi Beach wilaya ya kipolisi Kawe mkoa wa kipolisi wa Kinondoni aliyejulikana kwa jina la ANNA D/O MIZINGI, Miaka 48, Mfanyabiashara, Mkazi wa Boko.

Sunday, June 28, 2015

WAISLAM WAONYESHA KUCHOSHWA NA HALI YA TAIFA LA PALESTINA,SOMA WALICHOKISEMA LEO

Kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam Dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA akizungumza wakati wa semina hiyo
Waumini wa dini pamoja na viongozi mbalmbali na viongozi wa kitaifa katikia nchi zote duniani wametakiwa kuliangalia Taifa la palestina kwa jicho la tatu kutokana na kutengwa na mataifa mengi huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka kutokana na vita iliyodumu kwa muda mrefu sasa.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA  wakati wa semina ya maimam na mashekh kuhusu QUDS (PALESTINA) na matatizo wanayoyapata wananchi wa taifa la palestina na mataifa mengine ya masharaki ya mbali ambayo yamekumbwa na machafuko makubwa kipindi cha karibuni.
Baadhi ya picha za matukio mbalimbali kutoka katimka machafuko huko Palestina
Akizungumza kwa uchungu kiongozi huyo amesema kuwa mataifa mbalimbali pamoja na mashirika makubwa ya kutoa misaada kama umoja wa mataifa yamekuwa hayana msaada wowote kwa taifa la palestina jambo ambalo limeendelea kuwaumiza watu wa taifa hilo na kuendelea kukandamizwa na mataifa ya Israel na mataifa mengine yanayowazunguka.
Amesema kuwa Taifa la palestina ni Taifa ambalo lina mchanganyiko wa dini na madhehebu mbalimbali hivyo wanaoumia katika dhuluma hizo ni watu wa dini zote huku akitanabaisha kuwa kuna haja ya wakristo na waislam nchini na duniani kuungana kwa pamoja kupinga kwa kasi kubwa dhuluma hizo wanazofanyiwa Taifa la palestina.
Viongozi mbalimbali wa Dini ya kiislam waliohudhuria semina hiyo
Amesema kuwa Palestina ni nembo ya dunia kwani ndio nchi yenye historia kubwa duniani,na ni alama ya dini zote kwani ina mchanganyiko wa dini mbalimbali,huku akisema kuwa ndani ya taifa la palestina dhuluma yoyote wanayofanyiwa wapelestina ni dhuluma kwa dini zote wakristo pamoja na waislam.
Amesema kuwa kwa sasa wajibu mkubwa wa viongozi wa kidini na wapinga dhuluma kote nchini ni kuhakikisha kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinatokea katika mataifa hayo likiwemo taifa la palestina,na kuwaeleza watu juu ya umuhimu wa taifa la palestina kwa dunia na historia yake kwa ujumla.
Nje ya semina hiyo
Semina hiyo ambayo imewakutanisha maimam pamoja mashekh mbalimbali imefanyika Jijini Dar es salaam kwa kuandaliwa na (Tanzania ithnasheriya TIC pamoja na hawzar imam swadiq yani chuo cha imam swadiq kilichopo kigogo post jijini Dar es salaam.
Akizumgumzia malengo ya kufanyika kwa semina hiyo  kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania shekh HEMED JALALA amesema kuwa ni kuwakumbusha watanzania kuwa amani hii iliyopo nchini kwa sasa wajue kuwa na taifa la palestina wanahitaji kuwa nayo lakini wanaikosa hivyo watanzania waiangalie palestina kwa jicho la pekee na kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia.

Fastjet announces new route linking Tanzania and Malawi
Low-cost airline expands its pan-African network with a new, direct international route between commercial centres of Dar es Salaam and Lilongwe

Fastjet Tanzania has announced that its newest and fifth international route will commence on 27th July 2015 between Dar es Salaam, Tanzania and Lilongwe, Malawi.

Services between Dar es Salaam’s Julius Nyerere International Airport and Malawi’s Lilongwe International Airport will initially operate twice a week on Mondays and Fridays, using fastjet’s modern Airbus A319 jet aircraft with seating for 156 passengers. More capacity is expected to be added by fastjet to this route as demand increases for its safe, quick, affordable and on-time service.

MEMBE AWATAKA WATANZANIA WASIKUBALI KUTISHWA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofika mjini Kigoma jana, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake, haviwezi kutishwa na mtu yeyote katika kutekeleza maamuzi yoyote kutokana na kuwa na historia ya kuwa na msimamo usioyumba na uongozi thabiti.
Membe ambaye ni miongoni mwa wana CCM waliotangaza nia ya kuwania urais kupitia chama hicho, amesema yeye binafsi hatokuwa na kinyongo kwa maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na chama hicho hata ikiwa yatakuwa maamuzi machungu kwake.

Saturday, June 27, 2015

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI 28 JUNE 2015

HUZUNI YATANDA DAR,MBOWE,DK SLAA WAUNGANA NA WANAHABARI KUAGA MWILI WA EDSON KAMUKARA


Pichani ni mkurugenzi wa magazeri ya halisi piblisher na mwandishi nguli wa habari za uchunguzi tanzania SAID KUBENEA akiuaga mwili wa mfanyakazi mwenzake EDSON KAMUKARA LEO Jijini Dar es salaam
Aliyekuwa mwandishi wa habari wa magazeti ya hali halisi publisher wazalishaji wa gazeti la mawio na mwanahalisi online Marehemu EDSON KAMUKARA leo mwili wake umeagwa Jijini Dar es saalaam na kusafirishwa kwenda kupumzishwa nyumbani kwao Bukoba baada ya kufariki ghafla Juzi Nyumbani kwake Mabibo Jijini Dar es salaam.
EDSON KAMUKARA alifariki Dunia Terehe 25 huu nyumbani kwake kwa kile kiinachotajwa kuwa ni ajali ya moto huku wengine wakisema ni ugonjwa wa malaria.
Habari za kifo chake zilianza kuenea kwa kasi majira ya saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo ambapo Taarifa hizo zilikuwa zikieleza kuwa ndugu EDSONI KAMUKARA alifariki baada ya kulipukiwa na jiko la GESI lililokuwa ndani kwake huku Taarifa nyingine kinzani ambazo zinazidi kuenezwa zikidai kuwa ugonjwa wa malaria ndio uliosababisha kifo chake.
Katika shuguli hiyo ya kuaga mwili huo katika viwanja vya LEADERS leo asubuhi ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maswala ya habari wakiwemo mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Tanzania REGNALD MENGI,mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE,pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali na mashirika mbalimbali pamoja na wanahabari ambao ndugu EDSON  alikuwa akishirikiana nao kwa ukaribu.
Nimekuwekea picha mbalimbali za matukio katika shighuli hiyo huku tukizidi kufwatilia kwa ukaribu sababu za kifo hiki cha ghafla 

Wanahabari mbalimbali wakilia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili EDSON KAMUKARA

RAIS JAKAYA KIKWETE, MAKAMU WAKE DKT. BILAL WAWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA GEITA, VIWANJA VYA KARIMJEE, DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Juni 27, 2015 kwa ajili ya kushiriki shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max. Picha na OMR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete,  akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wa Dkt. Bilal, wakati walipokuwa katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Bilal, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na baadhi ya Viongozi wakijumuika na waombolezaji katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR