Thursday, July 30, 2015

ADC nao Waionea huruma CHADEMA kwa kumchukua Lowasa,soma hii

Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji akizungumza na waandishi wa Habari mda huu
Jijini Dar es Salaam
SIKU chache kupita baada ya Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa kukihama chama chake cha awali cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,navyo vyama vingine vya upinzania vimekishukia Chadema na kusema kimeua upinzani nchini.

         Akizungumza na waandishi wa Habari leo  jiijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha ADC Said Miraji wakati alipokuwa anazungumzia suala la Lowassa kuhamia Chadema ambapo tayari ameshachukua fomu ya Kugombani Urais kupitia Chadema.      Chadema ambao umeunda Vyama vya upinzani vya kutetea katiba ya Wananchi UKAWA,ambapo Miradi amesema kwa sasa vyama vya upinzania vimejishusha hadhi kwa watanzania.
      
  “Kitendo hiki kimezidi kudhihirisha kuwa vyama vya upinzani tunapozungumza vitu basi vinavyokuwa ni vya uongo,kwasababu Katibu mkuu wa chadema Dakta Slaa aliaminisha umma kwamba lowassa ni miongoni mwa mafisadi papa”
       
 “Halafu leo wamemkaribisha kwenye chama chao na kumpa nafasi ya Urais,sasa leo watanzania watatuona sisi wapinzani ni waongo maana yale aliyoyasema Slaa pale mwembe yanga ni uwongo au?”amehoji Miraji.
        
  Miraji ameongeza kuwa kitendo cha chadema kumsimisha lowassa kunazidi leta mpasuka kwa wananchama waliokijenga chama hicho kwa zaidi ya miaka 20.
      
         “Inakuwaje mtu ahamie leo na leo hiyo apewe uongozi tena wa juu,maana ndani ya chama hicho kuna makada waliokijenga chadema toka 1992 lakini leo hao hao hawapewi nafasi ya kugombani urais badala yake leo unawatupa unampa mtu aliyekuja leo kisa anaumaarufu wa watu,je hivi unategemea wananchi wengine hawatakubali”ameongeza.

        Aidha Miraji amekitahadharisha  Chadema kuacha tabia ya kutegemea kuwachukua wabunge na madiwani kutoka CCM na kuwapa uongozi kwa kusema suala hilo litaweza kukivuruga chama hicho kwa madai ya kuwa CCM wamepandikiza watu wake kuja kumaliza upinzani nchini.

Habari Za Kimichezo Leo Nchini TanzaniaNUSU FAINALI KAGAME KIINGILIO BUKU TATU TU
Hatua ya nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja wa Taifa, huku kiingilio cha chini katika michezo hiyo kikiwa ni shilingi elfu tatu (3,000).

Viingilio vingine vya michezo hiyo ya kesho  ni VIP A ni shilingi elfu kuni na tano (15,000) na VIP B & C, Shilingi elfu kumi (10,000) na sehemu nyingine ya uwanja iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na rangi ya chungwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI, JIJINI ARUSHA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26 ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani leo Julai 30, 2015. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa vazi la kabila la Masai na Kiongozi wa Mila ya Laibuwanani, Kisota Lengitambi, wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwela Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani. leo julai 30, 2015. Picha na OMR

Ni Mafuriko Tena upya,Tizama LOWASA akiwasili makao makuu ya CHADEMA leo

Nimekuwekea picha wakati MH LOWASa akiwasili katika makao makuu ya chadema kukabidhiwa form ya kuomba ridhaa ya chama kugombea urais ndani ya chama hicho

Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akiwasili ofisi za Makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar,akiwa ameambatana na Mh Lowassa (hayupo pichani),kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
Rabsha za hapa na pale zilikuwepo kama uonavyo pichani wakati Mh.Lowassa akiwasili Makao Makuu ya CHADEMA  yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho.

Picha za awali Lowasa anachukua form hapa chadema


Maandalizi yanaendelea vizuri naona mitaa yote ya Bongo DSM naona barabara zote maelufu kwa maelufu ya watanzania wanazidi kujitokeza kumlaki na kumpungia mkono wa baraka na heri kamanda mpya Eddo Lowasa.
Katibu Mkuu wa CDM ndugu Slaa anatarajia kumkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya wanachadema.


Wednesday, July 29, 2015

Umeskia Alichosema LISSU Baada ya kusemekana anajipanga kuondoka Chadema


MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.


Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL LEO

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA SUMATRA, TRA, TABOA, RC-DSM NA WAZIRI WA FEDHA IKULU KWA MAZUNGUMZO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) TRA, SUMATRA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Fedha, wakati  walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa SUMATRA, TRA, na Wamiliki wa Mabasi Tanzania TABOA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Fedha, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015. Picha na OMR
 MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA ECG NA AL KAN KUTOKA MISRI, IKULU DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wafanyabiashara wa ECG na Al Kan kutoka nchini Misri, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa ECG AL Kan kutoka nchini Misri, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015. Picha na OMR


“MESI WA SIMBA ATUA COASTAL UNION

Meneja wa timu ya Coastal Union,Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal Union winga mpya wa Kulia,Ibrahim Twaha "Messi"mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
NA MWANDISHI WETU,TANGA
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kufanya usajili wa nguvu ili  kujiimarisha vilivyo katika safu mbalimbali ambapo jana ilifanikiwa kuingia mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili aliyekuwa winga wa kulia wa Simba,Ibrahim Twaha “Messi”

Utiliaji saini wa mkataba huo ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mjini hapa na kushuhudiwa na viongozi waandamizi akiwemo Katibu Mkuu Kassim El Siagi na Meneja wa timu hiyo,Akida Machai.

winga wa kulia Mpya wa Coastal Union Ibrahim Twaha " Messi" akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Coastal Union kulia ni Katibu Mkuu,Kassim El Siagi kushoto ni Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai
Akiuzngumza mara baada ya kumalizika utiaji saini huo,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao hasa anapokuwa uwanjani .

Alisema kuwa winga huyo ana vitu adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa maendeleo timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

  “Niseme tu safari hii tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara na hili tunalifanya kuhakikisha tunarudisha kombe mkoani hapa ambalo tulilichukua mwaka 1988 “Alisema El Siagi.

Kwa upande wake,Ibrahim Twaha “Messi”mara baada ya kusaini mkataba huo alihaidi kuipa mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika safari za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.

  “Sasa ni kama nimerudi nyumbani kwa sababu awali nilikuwa naitumikia timu hii hivyo najisikia faraja kubwa kurudi tena Coastal Union mi nihaidi kushirikiana nao kwa lengo la kuipa mafanikio “Alisema Messi.

Awali akizungumza,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiri kufanya usajili nzuri ambao utaiwezesha kutwaa ubingwa na kurudisha makali yao ya miaka ya nyuma.

Tigo yazindua Duka Jipya Ifakara

ifakara picha no 1
Katibu Tawala wilaya ya Kilombero ndugu Yahya Naniya akikata utepe ikiwa ni ishara rasmi ya  uzinduzi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini, kutoka kushoto ni Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo, Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero na mwisho kulia  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki Goodluck Charles.
ifakara picha no 7
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki, Goodluck Charles akizungumza machache kwenye hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
ifakara picha no 8
Katibu Tawala wilaya ya Kilombero ndugu Yahya Naniya, akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini.
ifakara picha no 2
Wafanyakazi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini wakipozi kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyevaa tai nyekundu ndugu Yahya Naniya ambae ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kilombero, muda mfupi baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo.
ifakara picha no 4
Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo akitoa maelekezo jinsi watakavyo hudumia wateja kwa mgeni rasmi Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero ndugu Yahya  Naniya baada ya uzinduzi wa duka hilo lililopo Ifakara mjini.
ifakara picha no 5
Muonekano wa duka jipya kwa wateja wa Tigo lililopo Ifakara mjini.
ifakara picha no 6
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa duka la Tigo Ifakara mjini ndugu Yahya  Naniya ambae ni Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero (wapili kutoka kulia) akiwa katika meza kuu na  Goodluck Charles Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki(wa pili kushoto)  Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero(kushoto) na Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo (kulia).
 

Tuesday, July 28, 2015

Museveni, former African Presidents to discuss steps to take for Africa’s integration

An integrated continent has been the goal of African countries since the attainment of independence more than 50 years ago. Arguments for speeding up the integration process have been advanced by many, and it is generally agreed that integration would be politically and economically beneficial for Africa. The key challenge is to find a way to make this vision a reality.

H.E. Yoweri Kaguta Museveni, President of Uganda, and former Presidents Benjamin William Mkapa of Tanzania, Olusegun Obasanjo of Nigeria, Bakili Muluzi of Malawi, Jerry Rawlings of Ghana, Hifikepunye Pohamba of Namibia and Festus Mogae of Botswana are set to attend the African Leadership Forum 2015, to be held on July30thin Dar es Salaam.

Hizi Kauli ngumu Za Lowasa Nimezinasa wakati wa hotuba yake,haikutegemewa Tanzania

Baada ya yaliyotokea Dodoma wakati wa mchakato wa kuteua mgombea Urais wa CCM, nimechukua muda kutafakari kwa kina, mustakabali wangu ndani ya Chama na Taifa kiujumla.
Watu wengi wananiounga mkono wamekuwa wakisubiri nifanye maamuzi magumu, na baada ya mashauriano marefu nimeamua kuondoka CCM kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),


Tizama Mbowe Akimwagia Shukrani Rais KIKWETE,imewafurahisha watu nayo

A

CCM sio mama yangu,Mji wa Dodoma wasimama Kwa Muda Wakati Lowasa Akifanya Maamuzi Magumu

 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Picha zaidi ingia MICHUZI BLOG

AZAM NA YANGA KESHO MTOTO HATUMWI DUKANIHatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio yakiwa kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.

Mechi hiyo ya pili inatarajiwa kuanza saa 10:15 jioni inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kufuatia timu hizo mbili zinatotokea jijini Dar es salaam kuwa na upinzani mkali kuanzia katika Ligi Kuu a Vodacom Tanzania na michuano mingine.

Digital Advertising the future to reaching Tanzanian Millennials

 Tanzanian brands have been urged to embrace and adopt digital advertising to reach their target consumers if a sustained growth of commerce is to be achieved.

On average, the Tanzanian user looks at their smartphone more than 200 times in a day which consists of time spent checking social media feeds to messaging on WhatsApp and e-mails. Data from Internet World Stats shows that Tanzania recorded 7,590,794 million internet users as of December 2014 translating to 15.3% Tanzanians being consistently online.
With more Tanzanians using smartphones coupled with the ever reducing data prices and increased speeds, the internet is one medium that no brand should ignore.

Monday, July 27, 2015

Picha--Vurugu kubwa mkutano wa ACT shinyanga,zomea zomea yatawala,story nzima iko hapa


Vurugu hizo zimeanza baada ya katibu mwenezi wa ACT Wazalendo taifa Sabini Richard kupanda jukwaani na kuwatangazia wananchi kuwa kiongozi wa taifa wa Chama Hicho Zitto Kabwe hatahudhuria mkutano kutokana na kuwa na kazi zingine za kichama.


Kufuatia taarifa hizo wananchi walianza kupiga kelele na kuondoka kwenye mkutano huo huku wakilalamika kuwa kwanini chama hicho kiliwatangazia kuwa Zitto atakuwepo kwenye mkutano huo.

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA YAIPIGA JEKI MANISPAA YA ILALA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi akipokea
Madebe maalum la kuhifadhia takataka,Katika ni Mkurungenzi wa
Usalama wa Chakula Kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Raymond
Wigeng iliyofanyika katika eneo la wazi la Posta ya zamani leo Jiji Dar es Salaam.

 Mkurungenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi akitoa shukrani kwa
uongozi mzima wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kupokea msaada wa madebe ya kuhifadhia takataka ili zisizagae hovyo msaada huo umetolewa katika eneo la wazi Posta ya zamani
leo Jiji Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika kikao hicho Kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) iliyofanyika katika eneo la wazi Posta ya zamani leo Jiji Dar es Salaam. 

Picha na Emmanuel Massaka WA MICHUZI BLOG 

Kampuni ya Tigo yazindua minara Mkoani Geita

Wakazi wa Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe Mkoani Geita,wakimsikilza Mkuu wa Mkoa huo Fatma Mwassa,wakati wa uzinduzi wa mnara mpya wa mtandao wa Tigo.

Meneja Masoko wa Tigo kanda ya Ziwa Ali Mashauri (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa,alipofika kuzindua mnara mpya katika Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa,akiongozana na wananchi kuondoka baada ya kuzindua mnara wa Tigo katika Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa(aliyevaa suti)akikata utepe kuzindua mnara mpya wa mtandao wa Tigo katika Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe Mkoani Geita.

ROBO FAINALI KAGAME KUANZA KESHOHatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuanza kesho Jumanne kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa kwanza utakua ni kati ya Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya Rwanda itakayotoshuka dimbani saa 7:45 mchana kucheza na vijana wa Kwesi Appiah timu ya Al Khartoum kutoka nchini Sudan.

Yametimia hapa,UKAWA wamsafisha Lowasa rasmi,Lipumba Asema anakaribishwa sana

Yale yaliyokuwa yanasemwa kuwa Mbunge wa Monduli EDWARD LOWASA atajiunga na umoja wa katiba ya wananchi ukawa sasa imekuwa rasmi baada ya umoja huo kujitokeza muda huu na kumkaribisha rasmi na kusema kuwa sasa anakaribishwa yeye pamoja na watanzania wengine kuwa wanakaribishwa kujiunga na harakati hizo.


Katika mkutano wa wanahabari uliomalizika muda huu hapa makao makuu ya chama cha wananchi CUF mkutano ambao umehudhuriwa na wenyeviti wote wa vyama hivyo wamesema kuwa sasa rasmi wanamkaribisha lowasa kujiunga na harakati zao kwani bado wanaamini ni mtu safi ambaye alichafuliwa na watanzania bado wanaimani nao japo kuwa alitemwa katika mchakato wa chama cha mapinduzi.
Nje ya makao makuu CUF muda huu
Mh mbatia anasema kuwa umoja huo lengo lake ni kuondoa mfumo uliopo ambao unaongozwa na CCM hivyo wwatafanya kila njia ambayo itasaidia kufanikisha zoezi hilo.
Maswali mengi ya wanahabari yalikuwa yakiwataka viongozi hao kuonyesha kuwa LOWASA sio fisadi kama ambavyo waliwahi kumshambulia viongozi hao wamesema kuwa kiongozi huyo sio fisadi kwani hadi sasa hana kesi yoyote mahakani ya ufisadi.

Kuhusu mgombea wa urais wa umoja huo mbatia anasema kuwa  mwanzoni mwa mwezi wa nane huku mwenyekiti wa chama cha NLD anasema kuwa hakuna ubaya kama wakimchagua mh LOWASA kugombea nafasi hiyo.
Mkutano umemalizika kwa viongozi hao kusema kuwa UKAWA iko imara na ndio tumaini jipya la watanzania na hakuna mtu wa kuivuruga.