Monday, August 31, 2015

Magazeti ya leo jumanne september 01,2015,yote yapo hapa

GLOBAL PEACE FOUNDATION, TAWI LA TANZANIA KUHAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Viongozi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana  
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha amani nchini Tanzania katka kipindi hiki  kuelekea uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda na kushoto ni Ofisa Utawala wa GPFTZ, Hilda Ngaja.
 
 Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (kushoto) na  Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda, wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
 Ofisa Utawala wa Shirika hilo, Hilda Ngaja (kushoto) na Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu (kulia), wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………

DR. MAGUFULI AITIKISA SONGEA, AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA

????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa  anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi  na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Amesema pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
Amesema ataongeza zaidi  kasi yake katika utendaji  tofauti na alipokuwa  Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa  akichaguliwa na watanzania kuwa rais  yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
Dr John Pombe Magufuli pia alitembelea  na kuweka shada la maua  kwenye kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki  miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumba ni kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SONGEA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya CCM Ndugu William Lukuvi.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani Ruvuma.

Picha 14--Tizama Lowasa alivyopeleka mafuriko yake Njombe leo,aweka historia mpya

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya Shirika la Nyumba (National Housing) Mjini Njombe tayari kwa kuhutubia Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, anazoendelea kuzifanya kwa nchi nzima. Picha zote na Othman Michuzi, Njombe.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Makambako, waliofurika kwa wingi wenye Polisi Makambako, Mkoani Mkoani Njombe leo Agosti 31, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake. Katika hotuba yake, Mh. Lowassa amewatoa hofu wana CCM wanaotaka kujiunga na Ukawa kutoogopa kuchukua uamuzi huo kwani huu ni mwaka wa mabadiliko. Pia amewaomba Watanzania wanaomuunga mkono katika mikutano yake ya hadhara kutoishia hapo na badala yake kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Mwaka huu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Makambako, wakishangilia hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa

STARS YAMALIZA KAMBI UTURUKI
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro chini ya Kocha wake Mkuu Charles Boniface Mkwasa imefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe – Kocaeli nchini Uturuki.

TASWA FC, TASWA QUEENS WAMALIZA ZIARA YAO YA MKOA WA ARUSHA NA TANGA BILA KUFUNGWA, TASWA QUEENS WAIBUKA MABINGWA WA BONANZA LA TASWA ARUSHA

Kikosi cha Taswa Fc

Mchezaji wa Taswa Fc, Martine Peter, akimtoka mchezaji wa timu ya IMS Maji ya Chai, wakati wa mchezo wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Hussein Omari na Imman Makongoro wa Taswa Fc na Taswa Queens, wakifurahia baada ya kukamata Kuku katika mchezo wa kukimbiza kuku kwenye Bonanza la 10 la Taswa Arusha mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Mchezaji wa Taswa Queens, Oliver Arbogasti, akimiliki mpira wakati wa mchezo wao na timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC. Katika mchezo huo Taswa Queens, ilishinda mabao 37 - 3.

Sunday, August 30, 2015

AISEE--Umeona hii ya ukawa shinyanga mjini,unaweza kutizama sasa


Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamefurika katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mkuu ujao wilaya ya Shinyanga hususani jimbo la Shinyanga Mjini.Mkutano huo umeongozwa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema ndugu Patrobas Katambi maarufu kwa jina la "Mzimu wa Shelembi".

Viongozi wengine machachari waliohudhuria mkutano huo ni mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Kahama mjini mheshimiwa James Lembeli,mgombea ubunge jimbo la Kishapu Fred Mpendazoe na mgombea ubunge jimbo la Msalala kupitia Chadema ndugu Paul Malaika.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog Kadama Malunde, alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha 38,Angalia hapa chini


Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo la Shinyanga

SAMIA SULUHU wa CCM atia timu Iramba,Ahadi ya elimu bure yatolewa


Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini.


Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Babati Mjini.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Babati Mjini.


Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM.
Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Lowasa aanza kazi-Tizama alichokifanya mkoani Iringa

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, William Joseph Mungai, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015.Picha na Othman Michuzi, Iringa.

Waziri wa zamani wa Elimu, Mh. Joseph Mungai akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015.Picha na Othman Michuzi, Iringa.

 Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015.Picha na Othman Michuzi, Iringa.


Umati wa Wakazi wa Mji wa Iringa Mjini ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Sabasaba, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Agosti 30, 2015.Picha na Othman Michuzi, Iringa.

Tizama jinsi wasanii hawa walivyojitokeza jana kwenye kampeni za UKAWA

Bob juniour
Jana katika viwanja vya jangwani katika ile uzinduzi wa Kampeni nilikutana na baadhi ya wasanii ambao walikuwa wanamsapot mgombea huyo,wamo wa music na wasanii wa kuigiza yani bongo movie,unaweza kutizama baadhi ya picha zao wakuwa kwenye shughuli ile.

Saturday, August 29, 2015

Soma kwa umakini Hotuba hii ya LOWASA aliyoitoa leo,HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA
YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU

Sasa hapa yapo maneno yoote waliyotoa wazungumzaji waliozungumza leo pale jangwani,unaweza kuyasoma hapa
9:31 Mchana: Edward Lowassa akiwa na mgombea mwenza Haji Duni wanaingia kwenye viwanja vya Jangwani wakiwa kwenye gari la wazi.

9:43 Mchana: Lowassa amefika meza kuu na kuketi, meza kuu pia wamo Maalim Seif, Duni, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Salum Mwalim na wengineo.

9:48 Mchana: Sasa ni muda wa viongozi wa dini kuomba dua, Said Riko kwa niaba ya dini ya Kiislam anaomba dua na atafata mchungaji Gwajima kwa upande wa dini ya kikristo kuongoza sala kwa niaba ya wakristo.

9:56 Mchana: Baada ya dua, kilichopo kwa sasa ni wimbo wa taifa

Salum Mwalimu(9:59): Tunakutana hapa kwa sababu ya mambo mawili, jambo la kwanza kuzindua rasmi kampeni zetu. Jambo la pili ni kuzindua ilani yetu ya uchaguzi mkuu, japokuwa inazinduliwa na CHADEMA inaungwa mkono na vyama vyote vilivyo kwenye UKAWA.

U-15, MORO KOMBAINI ZATOKA SARE


TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa 15 leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Moro Kids Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mchezo wa kirafiki.

VIJANA WATANO U-15 WAELEKEA AFRIKA KUSINI


Wachezaji watano kutoka katika kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) wanaondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando Pirates kwa ajili ya kufanya majaribio.

Tizama mabango niliyokutana nayo leo pale jangwani

Hapa kuna mkusanyiko wa matukio mbalimbali katika mkutano wa Ufunguzi wa kampeni za umoja wa katiba ya wananchi UKAWA katika viwanja vya jangwani leo jioni,sasa mdau wangu nimekutana na baadhi ya mabango nikapenda nije kushare na wewe utizame watanzania walichokuwa wanakisema katika mkutano huo,story na uchambuzi wa maswala yaliyojitokeza katika mkutano huo ntakuwa nakupa kuanzia leo na kuendelea mdau wangu

Mafuriko ya Lowasa yazua makubwa jangwani,wengi wazimia kwa kukosa hewa

Kuna mengi sana umeona na kusikia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa UKAWA leo jangwani,hili nadhani hukuliona,baadhi ya watu walizimia kutokana na wingi wa watu na kulazimisha watru wa huduma ya kwanza kuanza kufanya kazi ya kuwsaidia watu kiafya.Report nzima ya mkutano huo itakujia muda mchache kaa hapa hapa mdau

Friday, August 28, 2015

Tizama majumuisho ya ziara ya lowasa Dar es salaam leo

Msanii Juma Nature A.k.a Kibla akiongoza wasanii wenzake kuwasalimia viongozi wa UKAWA leo Ijumaa 28/08/2015 ikiwa ni majumuisho ya ziara ya Mgombea Urais Mhe. Lowassa kwa jiji la Dar es salaam 

Nimekuwekea mambo muhimu aliyoyazungumza ZITTO KABWE leo Jijini Dar es salaam

Mh ZITTO KABWE kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo akionyesha bango la mgombea ubunge jimbo la kongwe ambaye anadaiwa kuanza kusambaza mabango ya kampeni kabla ya muda husika na tume ya uchaguzi kuliacha swala hilo licha ya malalamiko kadhaa kutoka kwa wapinzani 

 Chama cha ACT wazelendo leo kimenza mafunzo ya siku mbili mfululizo kwa wagombea wake wa nafasi za ubunge nchini mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na kujiamini zaidi kuelekea kufanya kampeni na kutafuta nafasi za uwakilishi wa katika majimbo mbalimbali kikiwa ni chama pekee nchini Tanzania kulichoendesha mafunzo kama hayo kwa sasa.

Kiongozi mkuu wa chama hicho ZITTO ZUBER KABWE akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo hayo amesema kuwa chama hicho ni chama pekee nchini Tanzania kilichodiriki kuwapa mafunzo ya kuelekea katika uchaguzi ili kuwaweka katika mstaari mmoja wa kuhakikisha kuwa wanakwenda na lugha moja kwa watanzania kueleza mipango na ilani ya chama hicho.
ZITTO KABWE akiendelea kutoa mafunzo kwa wagombea ubunge zaidi ya 90 walioshiriki katika mafunzo hayo
ZITTO KABWE anasema kuwa chama cha ACT wazalendo ndio chama pekee nchini Tanzania ambacho kina agenda maalum kwa watanzania tofauti na vyama vingine ambavyo amesema kuwa vinatumia mbwembwe na ulaghai kwa watanzania bila kuweka wazi nini wanataka kuwafanyia watanzania.

Kauli za Rais MKAPA sasa zaibua mengine,TACCEO waibuka na kusema haya

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ambao ndio waratibu wa mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi Tanzania TACCEO akizngumza na wanahabari kwa niaba ya mwenyekiti wa mtandao huo mapema leo jijini Dar es sakaam kuhusu uhakiki wa majina ya daftari la kudumu la wapiga kura na mwenendo wa uchaguzi mkuu nchini Tanzania
 Ikiwa ni siku chache Tangu Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh BENJAMIN MKAPA  kutoa kauli ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kuwa ni lugha chafu, sakata hilo limeanza kuchukua sura mpya baada ya wadau mbalimbali kuanza kujitokeza kulaani na kupinga matumizi ya lugha kama hizo katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.

Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO wamekuwa wa kwanza kuibuka na kulaani vikali vitendo hivyo ambavyo wamedai kama tume ya uchaguzi na vyombo husika vitafumbia macho vinaweza kusababisha machafuko na chuki kwa watanzania.

Akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam HELLEN KIJO BISIMBA kwa niaba ya nmwenyekiti wa TACCEO amesema kuwa matumizi ya lugha za kejeli,dharau,na vijembe katika kampeni yataleta chuki na hatimaye kupelekea uvunjifu wa amani jambo ambalo lazima wanasiasa wawe makini wanapokuwa majukwaani kuepuka kuwagawa watanzania na kuwapandikiza chuki.
Baadhi ya wanabari wakichukua Taarifa hiyo