Wednesday, September 30, 2015

Hiki ndicho atakachokifanya Mke wa Lowasa kesho Asubuhi sanaaa

Baraza la Wanawake Chadema- BAWACHA wanayo furaha kubwa kuwaalika wanawake wapenda mabadiliko kwenye kongamano kubwa la hatma ya shida na changamoto za Mwanamke katika jamii kwa zaidi ya miaka 54 ya Uhuru wa Taifa hili, na kuangalia chachu ya Mabadiliko yatakayoleta Maendeleo ya Wanawake na Taifa.

Ni alhamisi hii ya tarehe 01/10/2015 saa tatu asubuhi pale Ubungo plaza blue peal Hotel.

Mgeni rasmi ni mama Regina Lowasa! Wote mnakaribishwa kwani Chimbuko la maendeleo katika Taifa ni Wanawake!
Ukisikia Tangazo hili fikisha kwa wahusika wote!

Wanawake wote wa CHADEMA, CUF, NCCR, NLD, vikundi mbalimbali na Wanawake wote msio wanasiasa mnakaribishwa pia mtapata fursa ya kuelezea changamoto mbalimbali.

VIDEO--Sheikh HEMED JALALA asimulia mkasa mzima aliyoyaona kwenye ibada ya HIJJA


Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA ameibebesha mzigo wa lawama serikali ya Saudi Arabia kufwatia vifo vya watu zaidi ya elfu nne vilivyotokea siku chache zilizopita wakati wa Ibada ya hija iliyofanyika nchini humo huku akisema kuwa vifo hivyo ni uzembe wa wazi wa waandaaji wa ibada hiyo.

Lawama hizo amezitoa leo Jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili nchini Tanzania pamoja na waumini wengine wa dhehebu hilo wakitokea katika ibada hiyo ambapo amesema kuwa ni wazi mauaji yaliyotokea katika ibada hiyo ni ya kusikitisha sana na yalitokana na uzembe wa waandaaji wa ibada hiyo kutokana na kasoro nyingi zilizoonekana.

Amesema kuwa moja ya sababu kubwa iliyosababisha mauaji ya waumini wengi ni kufungwa kwa njia kubwa za kutoka na kuingilia wakati wa urushwaji wa mawe kumpiga shetani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa wa watu na kusababisha vifo vingi.

Aidha Sheikh JALALA ameongeza kuwa katika maeneo yote ya ibada hiyo kulikuwa kumezungukwa na kamera eneo lote lakini watu walikuwa wakifariki kwa mfululizo kwa kila baada ya dakika tatu lakini wahusika hawakuona na hakuna msaada wowote ambao ulikuwa unatolewa na wahusika licha ya kuwepo kwa kamera kila kona.

Baada ya tukio hilo Sheik jalala amesema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa ni lazima serikali ya Tanzania iungane na nchi ambazo zina idadi kubwa ya mahujaji ambao wanaenda katika ibada hiyo waweze kushirikishwa katika mipango ya ibada hiyo ili kuweka mipango ambayo itawafanya waumini kuwa salama wakati wa ibada hiyo kwa kuwa hakuna mtu anayekwenda katika ibada hiyo kwa ajili ya kufa.

TOROKA UENDEEE--Sasa ni Kesho Dar es salaam,wote mnakaribishwa huko



Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri ni kuwa jana tumekurepotia habari za uzinduzi wa kampeni mpya ya mgombea wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA iliyopewa jina la TORIKA UJE ambayo ilipangwa kuzinduliwa leo Jijini Dar es salaam,Habari za ndani zinaeleza kuwa Watanzania wengi wamekuwa na maombi ya jinsi ya kufika kwenye shughuli hiyo jambpo ambalo limewalazimu waandaaji wa Tukio hilo kulifanya katika maeneo ya wazi ili watanzania wengi waweze kulishughudia.Habari za ndani ambazo tunazo sasa ni kuwa alhamis ndio tukio hilo litafanyika na hii ni moja ya Taarifa ambazo tunazo unaweza kupitia na kushare na wengine



Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kinakualika katika mkutano wa mgombea Urais kupitia vyama vinavyounda ukawa mh. Edward Ngayai Lowassa utakaofanyika alhamisi ya tarehe 1 october katika viwanja vya tanganyika pekas kawe kuanzia saa nane mchana wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na maeneo jirani mnakaribishwa UKAWA tumaini letu..

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MWANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA IKULU DAR, AAGANA NA BALOZI WA MALAWI TANZANIA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuwasili nchini. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (wa tatu kulia kwake) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, (katikati yao) wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Sept 30, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuwasili nchini. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 kwa ajili ya kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 alipofika kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi. Picha na OMR

Tigo yatoa mchango wa madawati 700 kwa shule za umma mkoani Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, (kulia) akimkabidhi madawati Kaimu Ofisa Elimu Mkoa huo, Gerald Kifyasi baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya Sh49milioni kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo leo.

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Nyanda za juu Kusini Jackson Kiswaga akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi madawati.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini, Diego Gutierrez, (kushoto) akimkabidhi madawati yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Tigo imetoa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya 49 milioni kwa shule za msingi za wilaya za Rungwe, Mbozi na Mbeya Mjini.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, (kulia) akimkabidhi madawati Ofisa Elimu Shule za Msingi Jiji la Mbeya, Deusdedit Bimbalirwa, baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya Sh49milioni kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo leo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro  (kulia) akiwa ameketi kwenye dawati na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini, Diego Gutierrez, mara baada ya kampuni ya Tigo kumkabidhi  mhe. Kandoro madawati 700 yenye thamani ya Sh49 milioni kwashule za msingi za wilaya za Rungwe, Mbozi na Mbeya Mjini .

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein Aendelea na Mikutano Yake ya Kampeni katika Viwanja cha Garagara Mtoni Zanzibar,

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua tena kuongoza Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndg Yussuf Mohammed akizungumza na Wananchi na WanaCCM katika viwanja vya garagara mtoni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na kuwatana Wananchi kumpigia kura Dk Shein, ili kuzidi kuleta maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pemba katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 

Miezi Mitano sasa Tazara Hawajalipwa mishahara,Muda huu Wameamua kukutana,soma hii


 Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) leo wameibuka na kudai kuwa sasa ni miezi motano hawajui wala kuonja ladha ya mshahara huku kukiwa hakuna maelekezo wala kauli yoyote kutoka serikalini jambo ambalo limezua taharuki kubwa ndani ya mamlaka hiyo na kusababisha wafanyakazi wa shirika hilo kukutana kujadili hali hiyo inayowakumba.


Mtandao huu umekutana na mkutano uliokuwa unafanyika ndani ya mamlaka hoyo ulioitishwa na chama cha wafanyakazi wa reli nchini Tanzania TRAWU kikiwashirikisha wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo ambapo mada kuu katika mkutano huo ni kujadili hali ngumu waliyonayo ambapo wamesema kuwa hadi sasa  ni mwezi wa tano hawajapata mishahara yao huku wakiwa wamelalamika serikalini bila majibu ya kuridhisha.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Reli nchini TRAWU Bwana MUSA KALALA akizngumza wakati wa mkutano unaoendelea sasa Hapa Tazara Baina ya chama hicho na wafanayakazi lengo lao ni kudai mishahara yao
Mwenyekiti wa chama hicho MUSA KALALA amezungumza na mtandao huu kuhusu madhumuni ya mkutano huo ambapo amesema kuwa lengo lao sasa ni kupaza sauti yao kuhusu mishahara  ili serikali iweze kuwasikiliza na kuwasaidia.
Bwana MUSA amesema kuwa huu ukiwa ni wakati wa uchaguzi ni lazima serikali itambue kuwa wafanyakazi wa shirika hilo ni wapiga kura,na wanawahudumia wapiga kura hivyo kuwanyima haki yao kwa muda mrefu kunaweza kusababisha matatizo makubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ameongeza kuwa kumekuwa na matatizo makubwa yanayowakumba wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na wengine kufukuzwa kazi au kusimamishwa kutokana na kuonekana wanadai haki yao kwa kasi mbele ya jamii jambo ambalo amesema sasa uongozi wa chama hicho unaliangalia ili waliofukuzwa waweze kurejea kazini mara moja.

Tuesday, September 29, 2015

Lowasa Yupo Dar es salaam tayari kufanya Tukio hili la kihistoria,Tizama hii

Habari ambazo zimetufikia ni kuwa mgombea Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia UKAWA ndugu EDWARD LOWASA kesho anataraji kufanya tukio lingine Dar es salaam katika hotel ya  Bahari Beach Tukio ambalo ni uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la TOROKA UJE,kampeni ambayo inatajwa kuamsha Ari ya wapenzi wa vyama hivyo huku ikitajwa kuwa inaweza kuwazoa baadhi ya vigogo na kuhamia chama hicho.Mtandao huu utakuwa karibu na matukio hayo na utakupa kinaga ubaga .

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AUNGURUMA MTERA KWA KIBAJAJI, AWAAMBIA WANAMVUMI MSIDANGANYIKE

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika tarafa ya Mvumi jimbo la Mtera wilaya ya Chamwino leo wakati akiendelea na kampeni zake katika majimbo ya Isimani mkoani Iringa, Kibakwe na Mtera  mkoani Dodoma, ambapo amewaomba wananchi hao kutohadaika na wagombea wanaowadanganya kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijafanya kitu kwa miaka 54
Dk. Magufuli amesema kuwaambia watanzania CCM haijafanya kitu kwa  miaka 54 ni jambo ambalo linachekesha  kwani  Utulivu na amani  tuliyonayo  ni matunda ya uongozi bora wa viongozi wa serikali ya CCM waliopita wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere, “Wanapita kwenye barabara za lami zilizojengwa na serikali ya CCM tena nikizisimamia mimi John Pombe Magufuli, Wanatumia miundombinu ya mawasiliano na Umeme uliosambazwa kwa zaidi ya  asilimia 40 nchini na serikali ya CCM lakini wanasema haijafanya kitu ni jambo la kushangaza.
Mbaya zaidi wamekuwa viongozi wa serikali  tena wakiwa na nyazifa kubwa serikalini,  sasa kama walishindwa kuwajibika  na kuwatumikia watanzania wakiwa serikalini kwa nini hawakuondoka  mapema, Lakini  muda wote wakabaki CCM wakisifia mafanikio hayo ambayo leo wanayaponda. Si sawa kabisa hao wanatafuta madaraka kwa kutaka kuwadanganya watanzania nawaasa msikubali kudanganywa waongo hawa.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-MVUMI-DODOMA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Isimani mkoani Iringa Mh. Willliam Lukuvi katika mkutano uliofanyika kata ya Pawaga.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika mji wa Mvumi mkoani Dodoma leo.

JAJI LUBUVA amkwepa mbowe kiaina,ni swala la mabadiliko ya Tume

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imeshindwa kuzijibu tuhuma alizotoa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Tuhuma hizo ni zile za ubadilishaji holela kwa wakurugenzi  ndani ya tume hiyo pamoja na Idara ya usalama wa Taifa kuhusika katika ufanyaji kazi pia kwenye tume hiyo.

            Hayo yabainika leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya watu wenye ulemavu na NEC mkutano huo wenye  lengo la kuwapatia uelewa kuelekea uchaguzi mkuu ambapo mara baada ya mkutano huo waandishi wa habari walimfuata Mwenyekitiwa NEC Jaji mstaafu  Damian Lubuva ili kutaka kujua kuhusu madai hayo ya Mbowe.

Lowasa Aendelea Kutikisa Tanga leo,Tizama Hii ya mchana

Msafara wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha democrasia na maendeleo chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vya UKAWA mchana wa leo imemlazimu kusimama muheza Tanga baada ya mamia ya wakazi wa maeneo hayo kuzuia msafara wake ili tu kumuona na kumsikia.Hapa kuna picha za awali ,picha zaidi za mikutano yake leo zitakujia baadae

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA HAFLA YA UCHANGISHAJI FEDHA KWA AJILI YA UHIFADHI WA VYANZO VYA MAJI KATIKA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME YA MTERA, KIHANSI, KIDATU, NYUMBA YA MUNGU NA PANGANI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani. Hafla hiyo ilifanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mwenyekiti wa Mabibo Beer, Wines & Spirits na Mkurugenzi wa VIP Engineering Marketing Ltd, Benedicta Rugemalira, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya IPTL, Parthiban Chandrasakaran,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utwala wa REA, George Nchwale,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Monday, September 28, 2015

Tizama alichokifanya Magufuli Nyumbani kwa MSIGWA Iringa

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Samora  Manispaa ya Iringa wakati alipokuwa akiwaomba kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Dk. Magufuli amesema “Nipeni kura za ndiyo bila kubagua vyama vyenu kwa kuwa nitakuwa rais wa Watanzania wote  wakati nikitekeleza majukumu ya  kuwatumikia watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo,  Hata wale wa CHADEMA huwa mnasema (Peoples Power) mpeni Magufuli hiyo Power ili awe rais wa Watanzania wote” .
 Dk. John Pombe Magufuli akizungumza zaidi na wananchi wa Manispaa hiyo amesema Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kujenga mahusiano ya Kidiplomasia na mataifa mbalimbali ndiyo maana Tanzania ina mahusiano mazuri na nchi nyingi duniani zikiwemo nchi jirani, Amesema kwamba mara atakapochaguliwa na kuwa kiongozi wa Tanzania atahakikisha anadumisha mahusiano hayo na kuifanya Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii  na Kisiasa
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa leo
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  wa tatu kutoka kulia, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa  pamoja na wasanii wa Bongo Movie wakinyanyua mikono yao juu kama ishara ya Umoja ni Ushindi katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika mjini Iringa leo hii

Tanga Haina Mwenyewe--LOWASA nusura Asababishe maafa makubwa,mamia wazimia,picha zote zipo hapa

Wananchi waliolazwa chini baada ya kuzimia ni ndani ya mkutano ulioahirishwa Tanga uwanja ulikua mdogo sana. .




TANGA

Chopa iliyombeba Lowassa imeshindwa kutua kwenye eneo la Mkutano kutokana na Umati wa watu waliojitokeza mda huu hapa Tanga
Hivyo imelazimika kwenda kutua airport kisha kurudi uwanjani kwa gari!!
Inaelezwa Tanga ya leo sio ile ya mwaka 47 watu wanataka

Wananchi waliolazwa chini baada ya kuzimia ni ndani ya mkutano ulioahirishwa Tanga uwanja ulikua mdogo sana. .



 Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa amelazimika kuahirisha mkutano mjini Tanga baada ya maelfu ya wakazi waliojitokeza kushindwa kuenea ndani ya uwanja wa Tangamano jijini Tanga


Kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Tanga shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5,6,7, 8  zililazimika kusimama kwa muda baada ya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliojitokeza katika uwanja wa Tanagmano, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea kwa mkutano huo.

Licha ya juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo kushindikana jambo lililomlazimu Mh.Edward Lowassa kulazimika kusitisha mkutano huo.

Je? Nini kauli ya Chadema baada ya mkutano huu kuvunjika, John Mrema ni meneja kampeni wa Chadema.

Uamti huo wa wakazi wa jiji la Tanga ulionekana dhahili  ulionekana dhahili kuwashinda maafisa wa taasisi ya mslaba mwekundu redcros mjini Tanga.

Akiwa jiji Tanga katika siku yake ya kwanza ya kampeni alifanya mikutano katika maeneo ya Bumbuli Mombo kabla ya kuhitimisha katika uwanja wa Tanagmano mjini Tanga ambapo aliahidi kuboresha sekya ya afya ndani ya siku miamoja baada ya kuapishwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI, DAR, KUZIKWA KESHO MOROGORO.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mume wa marehemu Celina Kombani, aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  Ahmad Pangolani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Mawaziri wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro. 

Mkutano wa Kampeni Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Shein, Viwanja vya Bungi Zanzibar

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Mhe Shamsi Vuai Nahodha akisalimiana naViongozi wa CCM wa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuwasili katika viwanja vya mkutano wa hadhara wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika viwanja vya mpira bungi. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika viwanja vya mpira bungu kuhudhuria Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
Wanachama wa CCM wakiingia katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakiwa na picha za Wagombea 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla alipowasili katika viwanja vya Bungu kuendelea na Kampeni zake za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Sunday, September 27, 2015

Picha za wakina LOWASA na UKAWA walichokifanya nyumbani kwa MREMA Vunjo

Mgombea ubunge jimbo la Vunjo Mhe. James Mbatia akiongea na wananchi wa Kahe jimbo la Vunjo katika viwanja vya Oria shule ya msingi leo Jumapili 27/09/2015 

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa na Mhe. Fredrick Sumaye wakiwasili katika viwanja vya Oria shule ya msingi na kupokelewa na mgombea wa ubunge kwa jimbo la Vunjo kupitia NCCR Mageuzi,leo Jumapili 27/9/2015

Uzalendo wamshinda Mgombea wa CCM JOHN MAGUFULI ataja live jukwaani wanaokihujumu chama chake


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana aligeuka mbogo baada ya kuamua kuwataja hadharani watu wanaohujumu kampeni zake kwa kujifanya mchana wako pamoja na usiku wakigeukia upande wa upinzani.


Akiwahutubia wananchi wa mkoani Shinyanga jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Dk. Magufuli, alisema kuna mamluki wanaokihujumu chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Saturday, September 26, 2015

Tizama jinsi LOWASA alivyowasili Hai kwa MBOWE kwa kishindo


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati alipowasili eneo la Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.