Saturday, October 31, 2015

Matokeo Ya Darasa La saba 2015 yako hapa



TACCEO WALAANI UVAMIZI WA POLISI KWENYE KITUO CHAO CHA UANGALIZI WA UCHAGUZI

Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO ndigu HEBRON MWAKAGENDA akizngumza na wanahabari mapema leo kuhusu uvamizi wa ktuo chao uliofanywa na jeshi la polisi wakati wa mchaguzi mkuu wa Tanzania
 Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia uchaguzi nchini Tanzania TACCEO umelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kuvamia kituo cha ukusanyaji wa matukio mbalimbali yaliyokuwa yanajili wakati mchakato wa uchaguzi ulipokuwa unaendelea na kuchukua baadhi ya vifaa vya kituo hicho na kuwakamata baadhi ya maafisa wake.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo KAIMU MWENYEKITI WA UMOJA HUO BW HEBLON MWAKAGENDA amesema kuwa tukio hilo lilitokea octoba 29 majira ya saa nane katika eneo la mbezi bichi eneo ambalo kituo hicho kilikuwepo.

Bwana Mwakagenda amebainisha kuwa wakiwa kazini walishuhudia gari ya jeshi ya polisi ambayo ilikuwa na polisi sita waliokuwa wamevaa mavazi ya kujihami pamoja na silaha za moto wakiingia kituoni hapo ambapo askari hao walianza kuchukua vifaa vyao mbalimbali walivyokuwa wanafanyia kazi zikiwemo kompyuta za mezani 25,kompyuta mpakato 3 simu 25 za ofisini na kuwakamata waanglizi wao 36.

Aidha Bwana Mwakagenda ameeleza kuwa matukio ambayo yanafanywa na jeshi la polisi yanatakiwa kulaaniwa na kila mpenda Demokrasia maana yanalenga katika kudhoofisha demokrasia nchini ambayo ndo msingi wa utawala bora
Wanahabari wakichukua Taarifa hiyo
Hata hivyo BW MWAKAGENDA  ameitaka selikali kutotumia vyombo vya dola katika michakato yeyote ya kidemokrasia kwani kwa kufanya hivo kunaweza kuleta uvunjifu wa amani iliyojengwa kwa mda mrefu.

Ameongeza kuwa swala hilo limetokea huku vyombo vya dola vikitambua wazi kuwa uangalizi huo wa uchaguzi ulifwata misingi yote iliyowekwa kikatiba na sheria pamoja na kuwa na vibali na vitambulisho maalum kutoka tume ya uchaguzi vilivyowaruhusu kufanya kazi hiyo kihalali.

Kaimu mkutugenzi wa LHRC ambao ni wataribu wa mtandao huo IMELDA LULU URIO akizungumza katika mkutano huo
Akizngumza na wanahabari katika mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC ambao ndio waratibu wa mtandao huo Bi IMELDA LULU URIO amesema kuwa tukio la kuvamiwa kwa waangalizi wao na jeshi la polisi sio la kwanza kwani wakati waangalizi hao wakifwatilia zoezi la uandikishwaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa BVR huko Njombe waangalizi wao walivamiwa na polisi na kupigwa wakiwa katika kazi zao na hadi leo hakuna ufafanuzi wowote uliotolewa na mamlaka husika kuhusu chanzo cha tukio hilo.

Friday, October 30, 2015

MAGUFULI AWASHUKURU WAPIGA KURA

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wapenzi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla fupi ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa uliofanyika oktoba 25 mwaka 2015. 
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana(katikati) pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa sherehe ndogo ya kushukuru wapiga kura walioipa CCM ushindi.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwa  wananchi waliojitokeza kumpongeza nje ya Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.

CUF wapigilia Msumari mwingine sakata la zanzibar na ZEC

Pichani ni Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi  wa Chama cha wananchi CUF,Twaha Taslima akizungumza
na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam
kupinga uamuzi wa ZEC

Janet Mbene Ashukuru wapiga kura na wana CCM kwa kumchagua

MBUNGE mteule katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene (CCM) amewashukuru wananchi
wa jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na  Dkt. Jonh
Magufuli anayewania urais.

Polisi yavamia kituo cha ukusanyaji taarifa cha TACCEO na kukamata maafisa 36 pamoja na vifaa

Wakili Imelda - Lulu Urio Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC

Mtandao wa Asasi za Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini jana ulipata pigo katika mwendelezo wake wa kukusanya taarifa juu ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 kama unavyoendelea nchi nzima baada ya Jeshi la Polisi kuvamia kituo cha kukusanya taarifa kilichopo katika ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ofisi ya Mbezi Beach. Tukio hilo lisilo la kawaida lilitokea Majira ya saa nane mchana baada ya polisi kufika kituoni hapo na kuwaweka wahusika wa kituo hicho wapatao 36 chini ya ulinzi na kuwashinikiza kusimamisha kazi na Kufungua mitambo bila kutoa sababu ya kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC ambao ndio waratibu wa TACCEO Wakili Imelda – Lulu Urio amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kuvamia na kusimamisha shughuli ambazo zinafanyika kwa mujibu wa sheria na pia zinafanyika kwa kibali kutoka Tume ya Uchaguzi ya Tanzania.”Kitendo hiki ni cha kidhalilishaji ukizingatia sisi( TACCEO)  tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na pia tuna vibali vya kufuatilia uchaguzi kwa mujibu wa sheria” Kituo chetu kinaaminika kwa kufanya kazi kwa maslahi ya umma wa Tanzania na hii sio mara ya kwanza kwa sisi kufuatilia uchaguzi za nchi hii hivyo tumeshangazwa na kusikitishwa na kitendo hiki cha polisi kuvamia bila taarifa” – Aliongeza.

Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC Wakili Harold Sungusia akizungumza kwa masikitiko katika eneo la tukio alisema “mpaka sasa hatujui kosa kwani tumekuwa tukifuatilia chaguzi mbali mbali toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini na tumekuwa tukifuata sheria na taratibu zote zinazopaswa kama waangalizi na hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupa vitambulisho vya uangalizi kwa kutambua mchango na nafasi yetu”.


Hata hivyo sakata hilo bado linaendelea kwani wafanyakazi pamoja na vifaa vyao vya kazi ikiwemo kompyuta 27 pamoja na simu zao za mkononi ambavyo vimeshikiliwa na Jeshi la polisi likiongozwa na afisa mpelelezi wa Kituo cha Polisi cha Kawe aliyefahamika kwa jina la Mgonja. Wafanyakaizi wamefikishwa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.

MALINZI AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI RAIS MAGUFULI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Dk. John Pombe Magufuli kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika salamu zake, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi za mikakati yake ya kuongeza uwekezaji wa serikali katika maendeleo ya mpira wa miguu na michezo kwa ujumla.

Kauli ya RAILA ODINGA kwa Lowasa Na Rais mteule Magufuli

Waziri Mkuu wa zamani Kenya Raila Odinga amempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais Tanzania.

Akiongea katika mahojiano na BBC, Mhe Odinga amemshauri mgombea wa upinzani Mhe. Edward Lowassa Kuwa Kama Hajakubaliana na Matokeo basi Aende Mahakama kushtaki Kama yeye Alivyofanya wakati akigombea Urais Kenya na kushindwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Ameeleza pia matumaini yake kwamba Dkt. Magufuli atahakikisha kuendelea kwa uhusiano mzuri uliopo katia ya Tanzania na Kenya, na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendeleza ndoto ya kuelekea kwenye Shirikisho la nchi hizo.

PONGEZI KWA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKA KWA WANACHAMA WA CCM,TAWI LA CCM CHINA

TAWI LA CCM CHINA TUNAKUPONGEZA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KWA KURA NYINGI KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WA AWAMU YA TANO.TUNAKUTAKIA AFYA NJEMA NA MAFANIKIO KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WA JUU WA NCHI YETU.

Kuna umuhimu kwa viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar kukutana - Jaji Mutungi

Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi (wa pili kushoto) na baadhi ya wajumbe wa Ofisi hiyo. Kushoto ni msajili wa vyama Zanzibar Bw. Rajab Baraka. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, amesema kuna umuhimu kwa viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar kukutana, ili kutatua mzozo wa kisiasa uliojitokeza.
Amesema Zanzibar ni nchi amani, hivyo hakuna haja ya kuruhusu migogoro ya aina hiyo ambayo inaweza kupelekea kuvurugika kwa amani na kuipotezea sifa Zanzibar katika jamii ya Kimataifa.
Jaji Mutungi akiambatana na baadhi ya wajumbe wa ofisi hiyo ya msajili pamoja na msajili wa vyama kwa upande wa Zanzibar Bw. Rajab Baraka, ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Amesema kuna kila sababu ya kulinusuru taifa kuingia katika migogoro isiyokuwa ya lazima, na kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe ili kumaliza tatizo hilo.
Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, amesema amekuwa akichukua juhudi binafsi kukutana na wagombea wenzake kuzungumzia tatizo hilo, lakini baadhi yao wanaonekana kutokuwa tayari kulizungumza.
Amesema hapendi kuona Zanzibar inaingia katika machafuko yanayoweza kuepukwa, na kwamba viongozi wengine pia wanapaswa kufikiria amani na maslahi ya Zanzibar kuliko maslahi binafsi.
Katika hatua nyengine Maalim Seif amemshutumu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Bw. Jecha Salim Jecha kwa kuiingiza nchi katika migogoro ya kisiasa na kikatiba.
Akinukuu vipengele vya Katiba ya Zanzibar, Maalim Seif amesema kipindi cha Urais wa Zanzibar ni miaka mitano kuanzia tarehe ya kuapishwa, hivyo kuanzia tarehe 02/11/2015 kipindi cha Urais wa Zanzibar awamu ya saba kitakuwa kimemalizika. 

Hivyo amesema bila ya kuchukuliwa juhudi za dharura, kuanzia tarehe 02 mwezi ujao kwa mujibu wa katiba, Zanzibar itakuwa haina Rais, Serikali wala Baraza la Wawakilishi.

Thursday, October 29, 2015

Heeh--Magufuli atangazwa Rais wa Tanzania,Lowasa Ajitangaza rasmi Rais wa Tanzania

Watanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tumeainisha kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.

• Upunguzwaji wa kura zangu

• Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
• Tunaendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.

Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani
Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.

Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.

Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015

KAMPUNI YA SWALA ENERGY YAFANYA TAFRIJA NA WADAU BAADA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA AGM

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swala Energy Ltd, David Ridge akizungumza na Wadau wa Swala wakati wa tafrija mchapalo(cocktail) iliyofanyika jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki, Tafrija hiyo ilifanyika baada ya mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo AGM.

Katibu wa kampuni ya Swala Energy Ltd, Yohana Mganga (katikati) akiongea na meneja uendeshaji wa Swala Frank Whitehead(kushoto) na Meneja miradi mipya Neil Taylor wakati wa tafrija mchapalo(cocktail).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swala Energy Ltd, David Ridge akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali.

Mkurugenzi wa Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia (katikati) akifuatilia jambo, kulia ni mke wa David Ridge na kushoto Mkurugenzi wa Maendeleo na  Biashara wa Frontline, Hellen Kiwia.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swala Energy Ltd, David Ridge akizungumza na wadau.Meneja

 miradi mipya Kampuni ya Swala, Neil Taylor akibadilisha mawazo na Mwanahisa wa Swala Harold Temu.

Wednesday, October 28, 2015

TUME YATOA UFAFANUZI KUHUSU UCHELEWESHWAJI WA MATOKEO YA URAIS

1Na Beatrice Lyimo-Maelezo Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Damian Lubuva ametoa ufafanuzi juu ya ucheleweshaji wa matokeo ya  awali ya ngazi Rais kutoka majimbo mbalimbali nchini.

Akitangaza matokeo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 27, 2015  jijini Dar es salaam Jaji Lubuva amesema kuwa Tume inasubiri matokeo hayo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka katika majimbo yote nchini.

MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO

????????????????????????????????????
Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe. 
Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi. Kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya. 
Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa. Bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura. Hata hivyo, tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi, na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

TANGAZENI MATOKEO YA WABUNGE HARAKA KUEPUSHA FUJO--TACCEO WATOA RAI

Mwenyekiti wa mtandao wa asasi zaidi ya 17 zinazoangalia chaguzi TACCEO Bi MARTINA KABISAMA akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam
 Mtandao wa asasi za Kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO ambao unaratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ambao ni waangalizi wa ndani wa uchaguzi  unaoendelea nchini wamewataka wasimamizi wa uchaguzi ambao bado hawajatangaza matokeo ya wabunge katika majimbo mbalimbali kufanya hivyo mara moja kwa kuwa ucheleweshaji wa matokeo hayo unaweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani katika maeneo hayo.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam kupitia kwa mwenyekiti wa mtandao huo wa TACCEO Bi MARTINA KABISAMA wakati wakitoa tathmini ya uchaguzi huo hadi sasa ambapo amesema kuwa ucheleweshwaji wa kutangazwa kwa matokeo ya ubunge katika maeneo mbalimbali umekuwa ni changamoto kubwa ambayo imekuwa ikisababisha kutumika kwa nguvu ya polisi pamoja na vurugu kubwa kutokana na wananchi kukosa uvumilivu wa matokeo hayo.

Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi sura namba 343 ya sheria za Tanzania katika kifungu cha 8(a) inatamka kuwa msimamizi wa uchaguzi analazimika kutangaza matokeo ya uchaguzi mara moja pasipo kuchelewa baada ya kukamilisha kujumlisha kura hizo,huku akisema taarifa walizonazo kutoka kwa waaangalizi wao zinaonyesha kuwa kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo ni katika majimbo zaidi ya 21.
Kaimu Mkuruhenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC Bi IMELDA LULU URIO akizungumza wakati wa kutoa report ya maendeleo ya uchaguzi wa mwaka huu nchini kwa mujibu wa waangalizi wao mbalimbali nchi nzima
Ametolea mfano baadhi ya majimbo ambayo tatizo hilo lilijitokeza na kusababisha taharuki kubwa kuwa ni Temeke,Ilala,Simanjiro,na Zanzibar ambapo kumekuwa na sababu mbalimbali zinazochangia ikiwemo wagombea kudai kurudiwa kuhesabu kura,wagombea kukataa kusaini,kupotea kwa baadhi ya nyaraka husika,kupotea kwa baadhi ya masanduku ya kura,kuchelewa kupokea vifaa kutokana na changamoto za kijografia,ambapo hali ya kuchelewa huko kumesababisha wananchi kukosa uvumilivu na kuhisi kuwa kuna mbinu chafu zinazofanywa na kuamua kufanya fujo ikiwemo kuchoma baadhi ya ofisi za serikali.


Aidha katika hatua nyingine mtandao huo umebaini kuwepo kwa matumizi makubwa ya nguvu za dola kutoka kwa polisi kwa wananchi wasio na hatia wanaofurahia matokeo yao ya ushindi,huku wakisema matumizi hayo ya nguvu yanawafanya hata raia wema kuzoea vurugu na fujo na kuona kama mchakato wa democrasia ni mchakato wa fujo na vurugu,ambapo amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha linatenda haki kipindi hiki.

LOWASAA TENA--Sikia alichokisema,apinga matokeo yanayotolewa na NEC

 Ndugu waandishi wa habari;
Tumewaita hapa kuwaomba muwaeleze Watanzania wenzetu, jumuiya ya kimataifa na marafiki zetu wengine wa ndani na nje, kwamba hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kote nchini.
 
Hii ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Katika maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya wananchi.
 
Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli.
 
Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa.
 
Kwa mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na Mtambile, kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma, Same Mashariki, Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, siyo kura za uchaguzi mkuu wa rais. Tunaweza kuiita, “mzimu wa uchaguzi.”
 
Ndugu waandishi wa habari;
Tangu kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) – mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya rais,
 Hata hivyo, Tume imeendelea kutangaza matokeo hayo, bila kujali kile ambacho tumekieleza na kukilalamikia, kana kwamba tunachokisema ni ujinga, uzushi na uwendawazimu. Hili halikubaliki.
 
Aidha, katika maeneo mengine, likiwamo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyoko mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi, yanatofautiana na yale ambayo yamekusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo.
 
Hali kama hiyo ipo pia katika majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA na wale wa vyama washirika vya CUF na NCCR – Mageuzi, ama wamekuwa na nguvu kubwa au wameibuka washindi.
 
Upo ushahidi wa wazi ambao, ninyi waandishi mnaweza kwa kutumia uandishi wenu kuuthibitisha kwamba, katika majimbo yote ambako wagombea wa UKAWA wameshinda, TUME imechelea kutangaza matokeo ya urais kwa sababu zinazothibitisha kuwapo kwa mikakati ya hila.
 
Ikumbukwe kwamba matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada tu ya Jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabia kura na kuwakamata wataalam wetu waliokuwa wakipokea matokeo ya kura za rais nchi nzima ambayo hadi uvamizi huo ulipofanyika tulikuwa tukiongoza katika maeneo mbalimbali.
 
Ndugu waandishi wa habari;
Tunaamini kwa dhati kwamba, uvamizi huo ulifanyika mahususi kwa malengo ya kufanikisha uchakachuaji huo ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa sasa na NEC.
 Wakati tukijua kwamba NEC ndiyo mamlaka pekee ya kisheria ya kutangaza matokeo ya urais, tunapenda kuwataarifu Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati uvamizi huo ulipofanyika kura zetu za urais tulizokuwa tumezikusanya zilikuwa zikionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60.
 
Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na watendaji wa NEC, mimi Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, tunautangazia umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC.
 
Ndugu waandishi wa habari;
Kutokana na makosa hayo makubwa, tunaitaka NEC kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo ya urais na kuanza upya kufanya uhakiki wa kile wanacholetewa na wasimamizi wa majimbo ambacho ushahidi unaonyesha kuwapo kwa vitendo vya hila ambavyo vinafanywa na NEC.
 
Ndugu wana habari
Kile kinachofanywa na NEC hapa ndiyo kile kile kinachoendelea kufanywa kule Zanzibar leo na ZEC ambako kunafanyika juhudi kubwa na za makusudi kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa wazi wa ushindi wa Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF anayeungwa mkono na UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad.
 
EDWARD LOWASSA
MGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA