Monday, November 30, 2015

Lipumba Afika Ikulu Kumpongeza Rais Magufuli Kwa Ushindi wa kishindo

ba7
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba9Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba10Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015

BILIONI 4 ZA SHEREHE ZA UHURU KUPANUA BARABARA YA MWENGE-MOROCO YENYE UREFU WA KILOMITA 4.3

indexSehemu  ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni  nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo.

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATUHUMIWA KUMI NA MBILI WA WIZI WA MAKONTENA.

po1Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo katika picha leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchunguzi wa sakata la watuhumiwa wa wizi wa makontena 329. (Picha na Anitha Jonas) – MAELEZO
po2
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Zitto Kabwe aibua tena Ufisadi wa $600m,soma story nzima hapa


Ufisadi wa $600m hati fungani za Serikali: Tusikubali ya Rada, hatua zichukuliwe

Taasisi ya Serious Fraud Office ya Uingereza ( SFO ) inafanya mazungumzo na Benki ya Standard Group ya Afrika ya Kusini Lakini iliyoorodheshwa katika soko la hisa ya Uingereza ( London Stock Exchange ) ili kumalizana kuhusu tuhuma za rushwa katika ununuzi wa hati fungani za Serikali ya Tanzania yenye thamani ya dola za kimarekani milioni Mia Sita ( $ 600m ). Mazungumzo hayo yanafanywa mbele ya Jaji katika mji wa London.

RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA OFISINI KWAKE IKULU DAR.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMRRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na  Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis. Picha na OMR

U15 YAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15)  imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.

Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.

Sunday, November 29, 2015

Breakin newzz--SHEKH PONDA AACHIWA HURU


BREAKING NEWS: Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia

WAFANYAKAZI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAFANYA BONANZA LA KUMUAGA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU, WATWAA KOMBE

sa2
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya VPO Sports Club, Nehemia Mandia, baada ya kuibuka na ushindi katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR

sa01Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akizungumza wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, liliandaliwa na timu ya timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (V.P.O Sports Club) lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete, uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 205. Katika Bonanza hilo lililoshirikisha jumla ya timu Nne za VPO Sports Club, Wizara ya Mambo ya Nje, Kamati ya Amani waliochanganyika na Mabalozi na Amana Bank waliochanganyika na Zanzibar Fc, Timu ya VPO Sports Club iliibuka na ushindi kwa kuwafunga Mambo ya nje kwa jumla ya mikwaju ya penati 5-4 na kutwaa kombe la Bonanza hilo. Picha na OMR
sa3Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR

TUMEDHAMIRIA KUWATUMIKIA WATANZANIA – MAJALIWA

ks1Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ks2Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akiwa na  baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ks3Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ks5Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim majaliwa akiwasha moja ya pikipiki tatu ili kuashiria mkaka ti wa kueneza injili wakati alipohitimisha  maadhimisho ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye  ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.  
ks6Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akifurahia jambo  na baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Saturday, November 28, 2015

NI HUZUNI--SAFARI YA MWISHO YA KAMANDA ALPHONCE MAWAZO


Mwili wa marehemu Alphonce Mawazo ikiwasili nyumbani kwa baba mdogo (Charles Lugiko) Nyegezi jijini Mwanza ukitokea Hospital ya Bungando kwaajili ya ibada fupi.


Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita Alphonce Mawazo ukitolewa Hospital ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba Mdogo ( Charles Lugiko) huko Nyegezi na kurudi katika viwanja vya Furahisha ili kupata heshima za mwisho kitaifa.

Familia ya Marehemu Alphonce Mawazo wakiendeshwa na mchungaji kwa ibaa fupi iliyofanyika nyumbani kwa baba Mdogo wa Marehemu.

AMOS MAKALLA APIGA MARUFUKU LIKIZO ZA MA DC, WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA MKOANI KILIMANJARO


Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
KATIKA hali inayoonyesha ni joto kali la kuwatumikia Watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, amepiga marufuku likizo za Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.

RC Makalla aliyasema hayo juzi katika kikao cha kazi na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara wa halmashauri na Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa huo kwa ajili ya kupeana mikakati ya majukumu ya kuwatumikia Wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla, ikiwa ni hatua nzuri ya kwenda na kasi ya Dr Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mkoa huo ili kujipanga katika majukumu mbalimbali ya kuwatumikia wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Baadhi ya watendaji wa Mkoa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa huo, Aamos Makalla alipozungumza nao jana. Katika kikao hicho, RC Makalla alipiga marufuku likizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara ili kujipanga na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.

KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE TAOLEA UFAFANUZI MAAGIZO YA RAIS KWA WATENDAJI SERIKALINI

index

CHANZO CHA MAJI CHA RUVU CHINI KUWATUA AKINA MAMA NDOO ZA MAJI.

ru1Meneja Mradi Ruvu chini Mhandisi Emmanuel Makasa akiwaonesha waandishi wa habari sehemu ya bomba la kusafirisha maji kutoka chanzo cha Ruvu chini kwenda jijini Dar es salaam.
ru2Sehemu ya bomba la kusafirisha maji kutoka chanzo cha Ruvu chini kwenda jijini Dar es salaam lilivyozamishwa chini tayari kwa kusafirisha maji ambayo yatawanufaisha wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani kwa matumizi mbalimbali.
ru3Baadhi ya mitambo ya kusafisha maji ambayo yamesafishwa tayari kwa matumizi ya wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani.
ru4Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi kutoka Wizara ya Maji wakiwa eneo la chanzo cha maji cha Ruvu Chini.
ru5Fundi akiendelea na kazi ya kuunganisha na kuchomelea bomba la maji ambalo litasafirisha maji kutoka Ruvu Chini kwenda jijini Dar es salaam.
ru6Muonekano wa maji yakiwa mtoni kabla ya kuanza kusafishwa kupitia hatua mbalimbali  kwa matumizi.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Friday, November 27, 2015

Kleyah aachia video ya Msobe Msobe

MWANAMUZIKI KLEYAH AZINDUA VIDEO YAKE MPYA YA MZOBE MZOBE ALIYOMSHIRIKISHA BARNABA BOY

Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya  Maarufu  kama bongo fleva KLEYAH ambaye anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo  hatimaye amezindua nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la MZOBE MZOBE wimbo aliomshirikisha msanii maarufu  maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC nyimbo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.

KLEYAH ambaye ni Mhitimu wa shahada ya mawasiliano kutoka chuo kikuu cha cha Phoenix nchini marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la kimataifa la UNDP kabla ya  kuacha na kuamua kurejea nchini kwa ajili ya kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa kufanya kazi na watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kufanya nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu nchini humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini Kenya kwa sasa OGOPA DJS.

Katika nyimbo yake mpya ambayo ilizinduliwa Tarehe 6 Mwezi November na kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla na hatimaye leo umefanyika uzinduzi wa Video yake ya wimbo wa MZOBE MZOOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali vya Televission kwa ajili ya kumtambulisha msanii huyo ambaye anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii ya music wa kizazi kipya.

Akizungumza nara Baada ya uzinduzi wa Video yake msanii KLEYAH amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji wakubwa nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha album yake ambayo amepanga kuizindua mwezi July mwaka 2016 album ambayo ametamba kuwa itasheheni aina mbalimbali za misic ili kuwafurahisha mashabiki wanaofwatilia kazi zake.

Ameongeza aliamua kufanya music kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo wake  huku akieleza kuwa kusoma na baadae kufanya music ni jambo la kuigwa na wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii kutoboa tu si ndani ya nchi lakini Barani Africa na duniani kwa ujumla 

SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU

w1Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa hazina yakauka, taarifa hizo ni za upotoshaji kwani mfumo wa Serikali wa bajeti unaiwezesha Serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa Serikali ndizo hutumika. Kushoto ni Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw. Immanuel Tutuba na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
w2Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya Fedha za Serikali ambazo zitaelekezwa kwenye shughuli zitakazowagusa wananchi ikiwemo uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awali fedha hizo zilipangwa kutumika katika sherehe za Uhuru na shughuli zisizo za lazima. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari. (MAELEZO) Bw. Vicent Tiganya.
w3Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna Serikali inavyokusanya mapato yake na kuyaingiza katika mfuko mkuu wa Serikali ili yaweze kutumika katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Kulia kwake ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na kushoto ni msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.
w5Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Fedha na vyombo vya habari ambapo Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara hiyo Bw. John Cheyo alitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali kulingana na mipango iliyowekwa katika kuwahudumia wananchi.

KAMANDA MPINGA AZINDUA OPERESHENI PAZA SAUTI,JIJINI DAR ES SALAAM LEO

mp1Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP  Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
mp2Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari  zake mkoani wakati wa  kuzindua  wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona  viashiria vya uvunjifu wa sheria za  barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.

BALOZI SEFUE KUHUSU KUSIMAMISHWA KAZI KAMISHNA MKUU TRA

on1Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari hawapo pichani kuhusu upotevu wa makontena zaidi ya 349 huku akiwa ameshika nyaraka yenye orodha ya makontena hayo.
on2.Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue akionesha nyaraka hiyo mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano huo.
on3Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue wakwanza kushoto akifafanua jambo mbele ya wanahabari.
msi1

JK ATINGA OFISINI KWAKE LUMUMBA

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya  CCM Ofisi Ndogo Lumumba