Friday, January 22, 2016

DK SHEIN ASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UWT KATIKA KIJIJI CHA KIANGA WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

SH1
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kushoto Baba Mazazi wa Marehemu Asha Bakari Makame Mzee Bakari Makame na Viongozi wengine wakiwa katika mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kianga wakati wa mazishi hayo leo asubuhi.
SH2
VIJANAS wa Chama cha Mapinduzi wakiwa amebeba jeneza likiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari Makame wakati wa maziko yake katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja leo asubuhi.
SH3
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Viongozi wa Serikali wakishiriki katika Mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kijiji cha Kianga nje kidogo ya Mji wa Unguja Wilaya Magharibi B.
SH4
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwaka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.

SH5
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
SH6
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
SH7
MAKAMU wa Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi.
SH8
BABA Mzazi wa Marehemu Mzee Bakari Makame akiwaka mchanga katika kaburi la mwanawe baada kuzikwa katika makaburi ya Kianga Kijijini Wilaya ya Magharibi B Unguja.
SH10
WANANCHI wakihughuria mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja leo asubuhi.
(Picha na Ikulu)

No comments: