Wednesday, January 20, 2016

JAJI LUBUVA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA NEC

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani) leo 20 Januari, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam wakati alipofungua Mkutano wa Wajumbe wa Baraza hilo uliojadili mambo mengi yakiwemo Afya, rushwa ufanisi kazini na Utawala bora. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana. Ramadhani Kailima.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji
Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani) leo 20 Januari, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam wakati alipofungua Mkutano wa
Wajumbe wa Baraza hilo uliojadili mambo mengi yakiwemo Afya, rushwa
ufanisi kazini na Utawala bora. Kulia ni Katibu wa Mkoa TUGHE Bwana Gaudensi Kadyango na katikati ni Katibu wa Baraza hilo Bi. Rose Malo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana. Ramadhani Kailima akiongea na Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani) leo 20 Januari, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa
Wajumbe wa Baraza hilo uliojadili mambo mengi yakiwemo Afya, rushwa
ufanisi kazini na Utawala bora.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana. Ramadhani Kailima (aliyesimama mbele) akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC leo 20 Januari, 2016 katika Ukumbi
wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam wakati wa Ufunguzi wa
Mkutano wa Wajumbe wa Baraza hilo uliojadili mambo mengi yakiwemo Afya, rushwa
ufanisi kazini na Utawala bora.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC wakifauatilia taarifa toka kwa Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika leo 20 Januari, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC leo 20 Januari, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa
Wajumbe wa Baraza hilo uliojadili mambo mengi yakiwemo Afya, rushwa
ufanisi kazini na Utawala bora.
(Picha zote na Benedict Liwenga)
 
Na Benedict Liwenga.
Awataka kuzingatia maadili na Kanuni za Utawala bora na maadili katika utendaji kazi,
·
Awataka kuepukana na rushwa na kushinda vishawishi vya rushwa.
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji
Mstaafu Damian Lubuva amewataka Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC kuboresha
mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi ikiwemo kuzingatia maadili na kanuni za Utawala
Bora na kuepukana na rushwa.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati
alipofungua Mkutano wa Kumi na Mbili wa Baraza la Wafanyakazi na kuongea na
Wajumbe wa Tume hiyo pamoja na Wajumbe wengine wa TUGHE ngazi ya Taifa na
Matawi.
 
Jaji Lubuva amesema kuwa, Mabaraza ya Wafanyakazi yameundwa Kisheria
kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi ya Taasisi ili kusimamia
rasilimali pamoja na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi husika, hivyo kufanyika
kwa mkutano huo ni moja ya chachu ya kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza
ufanisi na tija katika Taasisi hiyo.
Akizungumzia kuhusu masuala ya rushwa, Jaji Lubuva ameeleza
kuwa, moja ya jukumu la NEC ni kuimarisha na kukuza demokrasia na Utawala Bora,
hivyo watumishi wa Tume hiyo hawanabudi kuzingatia maadili na kanuni za utawala
bora na maadili katika utendaji wa kazi zao pamoja na kuepukana na vitendo vya
rushwa na vishawishi vyake.
‘’Nimeambiwa kuwa, katika kikao hiki mtajadili kuhusu mada
mbalimbali kama vile Taratibu za Utendaji kazi Serikalini, masuala ya
uanzishaji SACCOS, Utekelezaji wa Bajeti na miradi ya Maendeleo, Ukimwi, Bima
ya Afya na masuala ya Madawa ya kulevya, niwaombe kujadili mada hizo kwa kina
na busara huku mkitambua kuwa matokeo ya majadiliano yenu ni kwa ajili ya
maslahi ya Taasisi yetu na Taifa kwa ujumla’’, alisema Lubuva.
Kwa upande mwingine, Jaji Lubuva amewataka wajumbe wa Baraza
hilo kujadili masuala ya afya kwa Wafanyakazi hususani suala la ugonjwa
waUkimwi katika sehemu ya kazi ambapo aliwaasa kila mfanyakazi kujikinga dhidi
ya janga hilo kwa kulinda afya yake na ya familia yake ili Taifa liweze
kunufaika na nguvu kazi iliyopo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Bw. Ramadhani Kailima ameitaka jamii kuondokana na dhana potofu
dhidi ya Tume hiyo kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu na chaguzi ndogo
zilizofanyika Tume hiyo imekuwa haina kazi ya kufanya mpaka uchaguzi mwingine  kwa kufafanua kuwa, Tume hiyo ina majukumu
mengi hata baada ya uchaguzi ikiwemo Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga
Kura, Uandaaji na Uratibu wa Kura za Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, Uratibu
wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi.
‘’Sio kweli kwamba Tume ya Uchaguzi mara bada ya Uchaguzi
Mkuu na chaguzi nyingine ndogo zilizofanyika kwamba ndo basi hatuna cha
kufanya, Tume ina majukumu mengi hata baada ya uchaguzi kama vile Uratibu na Usimamizi
wa Utungwaji wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Uundaji wa Mpango Mkakati
wa Tume, Uandaaji wa Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa wateja, Usimamizi wa
Ujenzi wa Jengo la Tume na Usimamizi wa chaguzi ndogo pale zinapojitokeza na
Mrekebisho ya Muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi’’, alisema Kailima.
Mkutano huo umefunguliwa leo ukiwahusisha Watumishi wa
Taasisi toka NEC, Wajumbe wa TUGHE ngazi ya Taifa na Matawi ambao jumla yao ni
54.

No comments: