Friday, January 15, 2016

Madiwani Wa TEMEKE wafanya ziara ya Kukagua Miradi Ya Maendeleo





Story na Izack Magesa
 Balaza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya TEMEKE,wamefanya ziara yakukagua miradi mbalimbali   ya kimaendeleo iliyotekelezwa katika manispaa hiyo

Akizungumza hii leo wakati wa ziara hiyo mstahiki meya wa manispa ya Temeke,ABDALAH CHAUREMBO, amesema wameweza kutekeleza miradi mbalimbali ya manispaa hiyo kwa asilimia kubwa mpaka sasa hivyo wameweza kutumia zaid ya BILLION TATU za mapato ya ndani katika kutengeneza barabara,shule na zahanati za manispaa hiyo.

“tumeweza kuboresha huduma ya afya kwakujenga jengo la huduma kwa mama na mtoto,mfano ukiangalia  ukonyuma wakinamama wajawazito walikuwa wanalala wawili mpaka watatu kwenye kitanda kimoja kwa idadi ya wagonjwa themanin mpaka mia moja(80-100) ivyo tatizo ilo kwasasa litakuwa histolia”amesema CHAUREMBO    
Pia CHAUREMBO,amepongeza ukusanyaji mzuri wa mapato katika manispaa hiyo, ivyo amewataka wakuu wa  idara mbalimbali katika manispaa hiyo  kutokaa tu namirad ya maendeleo maofisin mwao bila tija bali wametakiwa kifanyia kaz kwa wakati ili wananchi wa manispaa hiyo wapate maendeleo  

Akizungumza, DOCTAR,mkuu wa manispaa temeke,AMANI MARIMA amesema wameanzisha mfumo mpya ya kielotroniki katika hospital hiyo,ambayo inatolewa na bank ya (CRDB) ambapo mteja ulipa katika bank hiyo kulingana na huduma ya afya anayo itaka, Hivyo kusaidia kupunguza foleni ya wagonjwa hospitalin hapo 

AIDHA, MKURUGENZI,wamanispaa ya Temeke PHOTIDAS KAGIMBO amesema wameweza kutekeleza mirad mingi katika manispa hiyo kwa asilimia kubwa kwa kujenga shule nyingi nakuweza kuvuka lengo la serikali  kwa kuongeza  idadi ya shule za sekondari zinazoanzia kidato cha kwanza  mpaka kidato cha sita  ikiwemo shule ya sekondali TEMEKE,ambapo wameweza kuongeza kidato cha tano hadi  cha sita,hivyo amewaomba madiwani hao kutoa ushirikiano kwao katika kulipeleka garudumu la maendeleo mbele 


No comments: