MAHAKAMA KUU YA ARDHI YAWEKA ZUIO LA SIKU 60 NYUMBA ZA MABONDENI ZISIBOMOLEWE


DSC_1514Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulya akipata maelezo kutoka  kwa wakili anayesimamia kesi ya Msingi kwa wakazi wa Mabondeni kupinga kubomolewa nyumba zao, muda mfupi baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Ardhi kutoa hukumu ya maombi ya waombaji hao ambapo Jaji huyo ametoa kwa siku 60, nyumba hizo zisibomolewe na baada ya hapo mambo mengine ya kisheria yanaweza kufuata zaidi ikiweo kukata rufaa kwa pande zote mbili ikiwemo Serikali na walalamikaji hao. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog)

DSC_1518Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) akitoka katika Mahakama kuu ya Ardhi, baada ya kutolewa kwa hukumu juu ya kesi yao ya msingi ya kupinga kubomolewa nyumba za wananchi wa mabondeni ambapo Jaji wa Mahakama hiyo ametoa maamuzi ya siku 60 pekee kudumu kwa kusimamisha zoezi la ubomoaji na baada ya hapo maamuzi mengine yafuate.
DSC_1520
DSC_1520Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya akitoa ufafanuzi kwa wanahabari na wananchi wa mabondeni waliofurika kusikiliza kesi yao hiyo mapema leo.
DSC_1525
DSC_1525Wananchi hao wakimsikiliza mbunge wao huyo akitoa ufafanuzi wa kile kilichoamuliwa dhidi ya Mahakama kuu ya Ardhi.

Hata hivyo, Upande wa Mawakili wanaotetea kesi dhidi ya wananchi wa mabondeni wamebainisha kuwa, katika kuhakikisha haki inatendeka, kwa sasa wanapitia vifungu vya kisheria zaidi ilikuona wanachukua hatua gani katika kuhakikisha wanawapatia haki wananchi hao.

Kwa upande wake, Mbunge huyo ambaye aliweza kufika leo kwa dharura akitokea Bungeni mjini Dodoma, alifika Mahakamani hapo majira ya  mchana wa saa   huku kesi hiyo ikianza  saa 10 kaso robo na kudumu kwa saa moja na na robo, na kuamua Jaji Kente wa mahakama hiyo kutoa hukumu hiyo ambapo pia amezitaka pande zote kuwa zinazo haki ya kukata rufaa zaidi pindi watakapoona hawajatendewa haki.(P.T)

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.