Saturday, January 16, 2016

SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AHIMIZA UMOJA MIONGONI MWA WAISLAM

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza na wanahabari wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika Jijini Dar es salaam.
 Na Exaud Mtei (Msaka Habari)

Madhehebu ya kiislam Nchini kote na duniani wametakiwa kujenga umoja wa kudumu,kukaa kwa pamoja na kujadIli maswala yanayowahusu jambo ambalo litasaidia kuleta amani baina ya dini hiyo na dunia kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim  wakati wa sherehe maalum zilizowakutanisha waislam wa Madhehebu ya shea na sun kwa ajili ya kusherekea na kukumbaka kwa pamoja siku ya kuzaliwa kwa mtume muhammad s.a.w Jijini Dar es salaam.
Akizumngumza katika sherehe hizo Kiongozi huyo amesema kuwa kitendo cha madhehebu hayo mawili kukutana na kukaa kwa pamoja ni ishara nzuri ya kuonyesha kuwa Dini sio uadui bali ni umoja na uoendo hivyo akaitaka dunia kwa ujumla kutambua hilo.

Amesema kuwa hakuna haja ya kuendelea kujenga chuki na uhasama baina ya madhehebu hayo bali jambo sahihi  ni kukaa kwa pamoja na kujadili mambo yanayowahusu na yale yatakayoshindikana kutokana na itikadi za kidini yaachwe ili yasiwe ni chanzo cha chuki mbalimbali.

Mmoja kati ya walimu wa Kidini ambaye alishiriki katika sherehe hizo  MSABAHA SHABAN MAPINA akizngumza na wanahabari umuhimu wa kukutana kwa waislam wa imani tofauti 
Mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na baadhi ya washiriki katika sherehe hizo ambapo mmoja wa walimu wa kidini MSABAHA SHABAN MAPINA amesema kuwa sherehe ya kukutana kwa madhehebu hayo mawili yenye imani Tofauti tofauti ni jambo la kuigwa na Tanzania nzima pamoja na dunia kwani ni njia nzuri ya kujenga umoja wa kidini ambao ilikuwa umeanza kutetereka 

No comments: