Friday, January 22, 2016

TIGO WAZINDUA UDHAMINI WA MBIO ZA NUSU MARATHON MJINI MOSHI

Meneja
Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari
28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka
pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
 
 Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, akifafanua jambo   kwa waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Tigo kwa mbio za Nusu Marathon mbio hizo zitafanyika Februari
28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka
pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga(watatu kushoto, ).akizindua mbio za Kilimanjaro Marathon kwa upande wa Moshi. Wengine ni wadhamini wakuu wa mbio hizo kutoka kushoto, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania-Kilimanjaro na Tanga, Richard Temba, Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Listone Metacha na Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO, Caroline Kakwezi.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
 
Wageni waalikwa ambao  ni wadhamini wa Kili Marathon wakifurahia jambo baada ya Mkuu wa wilaya Mh Novatus Makunga kuzindua mbio za Kili Marathon kwa upande wa Moshi ambapo zitafanyika hizo zitafanyika Februari
28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka
pande mbalimbali za dunia.
Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
Mbio za Nusu Marathon
2016 zimezinduliwa jana mjini Moshi, huku ikiwa imebaki mwezi moja kabla za
mbio hizo kufanyika.


Meneja Mawasiliano wa
Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari alisema mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani
Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali
za dunia.
“Tumeonelea ni vizuri
kuzindua mbio hizi rasmi hapa Moshi  ambako
zitafanyika ili kuashiria kuwa mambo yamekamilika,” alisema.
“Tigo imeingia mwaka
wake wa 2 kama mdhamini wa mbio za kilomita 21.2 hizi. Kwa mujibu wa Meneja
huyo, wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Kilimanjaro beer 45, Gapco kwa km
10 viti vya magurudumu na baiskeli ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt kwa km
5.
Wengine ni KK Security,
TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair na
Keys Hotel.
Alisema Tigo imewekeza
zaidi ya Sh Millioni 200 katika mashindano hayo na kuwa hapo badaye watatangazo
mchanganuo mzima wa zawadi zitakazotolewa.
Alitoa shukrani za
pekee kwa mkoa wa Kilimanjaro na chuo kikuu cha Ushirika MOshi (MoCu), zamani
kikiitwa MUCCoBS kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Akizindua mbio hizo
mjini hapa, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makung, aliwapongeza Kilimanjaro
Premium Larger,Tigo wadhamini wengine na wandaaji kwa kujielekeza vyema  kila mwaka, akiongeza kuwa
mashindanoyametokea kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kimichezo ndani na
nje ya nchi.
“Mashindano haya pia
yamekwenda mbali zaidi katika kukuza utalii, kwani wanariadha wa kimataifa na
wageni wao hufanya utalii baada ya mashindano na hiyo kufaidisha uchumi wan
chi,” alisema Makunga.
Makunga aliawataka
wanariadha wa Tanzania kuhakikisha wanajiandaa vyema ili watwae zawadi nyingi
zaidi kwa kadiri zilivyopangwa kwa kila mbio. Aliongeza kwamba wizara yake
inaunga mkono kabisa ubunifu kama huo na kuzitaka kampuni nyingine kufuata
nyayo hizo kwa kudhamini mashindano hayo kila mwaka.
 
Aliwapongeza wandaaji,
Wild Frontiers, waratibu wa kitaifa Executive Solutions, Chama cha Riadha
Tanzania (RT) na wizara yenye dhamana ya michezo kwa kuhakikisha siku zote
kwamba tukio hili linafikiwa .
“Mbio hizi zimeleta
mwamko mpya katika riadha hapa nchini kwa kuwapa fursa vijana wetu
wanaochipukia kuweza kujipima na wanariadha mashuhuri kimataifa. Changamoto hii
imekuwa na faida kubwa,ambapo vijana wetu wameweza kutambua uwezo wao na kuweza
kujiamini  zaidi wanapokwenda kushiriki
mashindano mbalimabli kwenye nchi za kigeni,” alisema.
 
Meneja wa Tigo Kanda ya
Kaskazini Henry Kinabo, alisema kwamba kampuni yake imefurahishwa kupata fursa
ya kudhamini mbio za nusu marathoni kwa kilimota 21 kwa mwaka wa pili
mfululizo.
“Natoa rai kwa
washiriki wajiandae vizuri ili safari hiituweze kunyakua mataji mengi,” alisema
Kinabo.

Meneja Masoko wa Gapco
Tanzania, Caroline Kakwezi, ambaye kampuni yake inadhamini mbio za kilomita 10
kwa wanaotumia viti vya magurudumu na wale wanaonyonga baiskeli kwa mikono
ambazo wanazidhamini, alisema zimekua na mvuto mkubwa na ushindani mkubwa pia
na kwamba katika mwaka wao wa tano katika udhamini wameshuhudia mbio hizo
zikikua.
“Tunawashukuru wateja
wetu wote kwa kuendelea kutuunga mkono, safari hii tutatoa usafiri, malazi na
chakura kwa washiriki wote kutoka Dar es Salaam katika mbio hizi za walemavu na
yote haya hayawezekani bila ushirikiano tunaoupata kutoka kwa wateja
wetu”alisema.
 

No comments: