WABUNGE WA CCM MJINI DODOMA

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula (kulia) akizungumza na wabunge wa CCM kwenye semina maalum ya Wabunge wote wa CCM inayofanyika kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wengine pichani ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye (kushoto). Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Ndugu Nape Nnauye (kulia) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza Mhe. Shanif Mansoor muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Mhe. Annastazia Wambura muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha wabunge wa CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wabunge wa CCM kabla ya kuanza kwa kikao cha wabunge hao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.