Sunday, January 24, 2016

WAISLAM--UGAIDI USIFANANISHWE NA DINI YETU

Mwenyekiti wa Imam Buhari islamic Foundation ambao ndio waandaaji wa semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam SHEIK KHALIFA KHAMIS  akizngumza na wanahabari nje ya semina hiyo kuhusu malengo mahususi ya semina hiyo.Picha zote na Exaud Mtei wa HABARI24 BLOG

Na Exaud Mtei (Msaka Habari)
Vyombo vya ulinzi nchini pamoja na seriali kwa ujumla wametakiwa kuelewa kuwa vitendo vya ugaidi vinavyotokea nchini Poamoja na duniani kwa ujumla havina uhusiano wowote na dini ya kiislam kama jinsi ilivyokaririwa na wengi hivyo dini zote nchini ziaminiane na kupiga vita vitendo vyote vya kigaidi duniani.
Kiongozi mkuu wa madhehebu ya shia nchini Sheikh HEMED JALALA akizungumza na wanahabari leo
Hayo yemeelezwa leo katika semina iliyowakutanisha waumini wa dini ya kiislam kwa pamoja iliyoandaliwa na taasisi ya Imam Buhar Islamic Foundation iliyokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja changamoto zinazoikumba dini ya kiislam kwa sasa hususani swala la ugadi ambalo limeendelea kuwa tishio kwa kizazi cha sasa.
Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa Imam Buhari Foundation ambao ndio waandaaji wa semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam SHEIK KHALIFA KHAMIS amesema kuwa dini ya kiislam haina mahala popote inapofundisha watu wake mafunzo ya kigaidi,mauaji,na vitendo vya kinyama vinavyotendeka duniani hivyo ni lazima watanzania na dunia kwa ujumla kuacha kuamini kuwa vitendo vya kigaidi vinafanywa na waislam.

“Leo akipatikana mtu mmoja ambaye kavaa kanzu kafanya vitendo vya kigaidi basi inachukuliwa kuwa waislam woote ni magaidi dunian,sio kweli na hatufundishi ugaidi katika dini zetu,tunaomba vyombo vya dola kufuta mawazo haya mabaya juu ya uislam”amesema.
Waislam waliohudhuria semina hiyo wakisikiliza kwa makini
Ameongeza kuwa semina hiyo imekuja mahususi kuwakumbusha waislam jukumu lao la kujenga umoja miongozi mwao na kwa watanzania kwa ujumla jambo ambalo litasaidia katika kuendeleza umoja na mshikamano wa watanzania uliopo.
Aidha katika hatua nyingine naye Kiongozi mkuu wa madhehebu ya shia nchini Sheikh HEMED JALALA akizungumza na wanahabari ameipongeza taasisi ya Imam Buhar kwa kuandaa semina hiyo ambayo amesema imekuja wakati muafaka ambao vitendo vya ugaidi vimeshika kasi sana katika nchi nyingi jambo ambalo linaendelea kuzua hofu kwa dunia nzima.

Baadhi ya picha zinazoonyesha madhara ya vitendo vya kigaidi duniani
Amesema kuwa nchi ya Tanzania ni moja kati ya nchi chache duniani ambazo zinaishi kwa umoja na mshikamano pamoja na upendo wa hali ya juu hivyo semina hiyo itatumika kuwatahadharisha watanzania kuepuka sana kukaribisha vitendo vya kigaidi katika nchi yao kwani itasababisha hatari kubwa.PICHA ZOTE ZA SEMINA HIYO ZIPO CHINI BOFYA







No comments: