Wednesday, January 20, 2016

Yale yaleee--Serikali ya Magufuli yaanza maigizo,TRA yavamiwa Na Compyuta Kuibiwa,Maswi ahamishwa fasta-ZITTO afunguka asema ni Sarakasi za serikali


Katika magazeti ya leo likiwemo gazeti la Mwananchi wameandika Story Inayohusu kuvunjwa na kuibiwa Kwa Compyuta ndani ya ofisi ya kamishna mkuu wa TRA jambo ambalo limezua taharuki na watanzania wengi kubaki wakisubiri kusikia nini kimetokea.

Mchana wa leo Ikulu ya Tanzania Ghafla imetangaza kuwasimamisha kazi wafanyakazi kadhaa wa ofisi hiyo kama inavyoonekana katika Taarifa niliyokuwekea mwisho wa story hii,huku pia Ikulu ikimuondoa ELIAKIMU MASWI katika nafasi ya Naibu kamishna wa mamlaka hya mapato TRA na sasa amerejeshwa katika nafasi yake ya awali aliyokuwa nayo ya katibu Tawala wa mkoa wa manyara kwa kile ambacho kimetajwa kuwa ni kumaliza kwa kazi maalum aliyokuwa kuifanya ndani ya TRA.

Sakata hilo limzua sintofahamu huku maswali mengi yakiwa ni Nani amehusika na wizi wa Comppyuta hizo,na kwanini Maswi ameondolewa haraka katika nafasi yake huku ikulu ikijitetea kuwa ni baada ya kumaliza kazi maalum aliyoagizwa.
Mtandao huu pia umemnukuu katibu mkuu kiongozi OMBENI SEFUE akisema kuwa ndugu ELIAKIMU MASWI amerejeshwa katika nafasi yake ya awali kwa sababu amemaliza kazi yake na huku tunakoenda kunahitaji utaalamu kuliko ule aliokuwa nao yeye.

Moja kati ya viongozi wa upinzani wanaosifika kwa hoja zenye umakini Ambaye ni Mbunge ZITTO KABWE kwa kupitia mitandao ya kijamii ameonyeshwa kushangazwa na sakata hilo huku akisema kuwa hayo ni maigizo ya serikali ya awamu ya Tano huku akitumia neno SARAKASI za serikali.Endelea kufwatilia sakata hili
mag

No comments: