Mkuu wa mkoa wa Dar es
samaa SAID MECK SADIC amewataka waanchi na wadau mbalimbali kuungfa mkono hatua
iliyochukuliwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na DR JOHN POMBE
MAGUFULI katika kusimamia maendeleo ya elimu na kuhakikisha inatekeleza
ipasavyo wanafunzi wapate elimu.
Ameyasema hayo leo Jijini
Dar es aalaam wakati wa mkutano na wakazi pamoja na wazazi wanafunzi
walioandikishwa kwa ajili ya Darassa la kwanza katika shule ya msingi maji
matitu ambayo zaidi ya wananfuzi 8276 wameandikishwa kwa mkoa wa Dar es salaam
kujiunga na darasa la kwanza mwaka huu.
Akizngungumza na
wananchu hao mkuu huyo wa mkoa wa Dar es salaamamesema kuwa sera ya Rais ya
elimu bure imepokelewa kwa uzito kubwa na wananchi wameandikisha watoto wao kwa
wingi na kuvuka makadirio kwa zaidi ya asilimia iliyokusudiwa hivyo jamii
inatakiwa kuunga mkono jitihada hizo kwa
kuchangia madawati kwa ajili ya kuleta uboreshaji zaidi katika elimu hiyo.
Aidha amesema kuwa
serikali kupitia mkoa amnaoungoza imepanga kuelekeza zaidi ya Billion 4 katika
elimu baada ya kupunguza fedha katika matumizi yasoyo ya lazima ikiwa ni njia
ya serikali ya kubana matumizi.
Naye mstahiki meya wa
manispaa ya Temeke ABDALA CHAUREMBO akizungumza katika mkutano huo ameahidi
kuwa halmashauri yake imedhamiria kuanza utekelezaji wa agizo kwa ujenzi wa
shule mpya na kuongeza madarasa pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za
kielemu katika eneo lake,
Katika hatua nyingine
mkuu wa mkoa wa Temeke SOPHIA MJEMA amepongeza sera ya Rais ya elimu bure kwa
kuwa amepanga kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata elimu bora na yenye Tija
kwa jamii
No comments:
Post a Comment