Sunday, February 7, 2016

MPYAA-Wajumbe wa Tume ya uchaguzi zanzibar ZEC wamkaanga JECHA muda huu,wasimulia kinachoiangamiza zanzibar,soma hii

 Na Exaud Mtei(Msaka Habari)

Wakati wadau mbalimbali wa maswala ya kisiasa wakipinga kile kinachoendelea visiwani Zanzibar,nao wajumbe wawili wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC Ndugu NASSOR KHAMIS MOHAMED na  AYOUB HAMAD  wameibuika jijini Dar es salaam leo na kupinga marudio ya uchaguzi unaotaraji kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kwa madai kuwa uchaguzi huo sio halali kulingana na matukio yaliyotokea tangu kufanyika kwa uchaguzi halali wa October 25 mwaka jana.

Wakizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam makamishna hao wamesema kuwa sababu kubwa ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo ni kutokana na kuvurugwa kwa katiba ya zanzibar tangu tukio la kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana ambapo wamesema kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo hakuwa na mamlaka ya kisheria kufuta uchaguzi huo bila kuwashirikisha makamishna wa tume hiyo.
Mjumbe wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar NASSOR KHAMIS MOHAMED akizngumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam
Wamesema kuwa sababu nyingine inayowafanya kupinga uchaguzi wa marudio ni kutokana na kukamilika kwa uchaguzi wa mwaka jana ambapo uchaguzi huo ulikuwa umekamilika na baadhi ya washindi wa viti vya uwakilishi na udiwani walishakabidhiwa vyeti vyao na mawakala kusaini kuwa uchaguzi huo hauna kasoro hivyo wanashangaa kuambiwa kuwa uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi zilizo pelekea kuubatilisha uchaguzi huo.

Wameongeza kurudiwa kwa uchaguzi huo ambao unatarajiwa kutumia zaidi ya billion  saba hadi kukamilika kwake ni matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwani uchaguzi Zanzibar ulishafanyika na tayari na kinachoendelea ni mbinu za kuubatilisha uchaguzi huo.

Wameongeza kuwa tukio la kufutwa kwa uchaguzi huo lilitanguliwa na matukio kadhaa ambayo yalionyesha wazi kuwa kuna kikundi cha watu ambacho kinamshauri mwenyekiti wa tume hiyo JECHA SALUM JECHA na sio maamuzi ya tume nzima.

“Tarehe 26 october mwaka jana CCM walileta barua ya malalamiko na kumtaka mwenyeikiti na tume kufuta uchaguzi huo wakati tayari tulishaanza kutoa vyeti kwa washindi,ambapo mwenyekiti aliitisha kikao cha tume na tulipitisha kwa pamoja kuwa maombi ya CCM hayakuwa na mashiko hivyo mchakato unaendelea”amesema NASSOR KHAMIS ambaye ni mmoja wa makishna wa tume hiyo.
Mjumbe mwingine AYOUB HAMAD akifafanua jambo mbale ya wanahabari kuhusu kile kinachoendelea Zanzibar
Ameendelea kusema kuwa baada ya maamuzi ya tume ndipo siku iliyofwata mwenyekiti JECHA hakufika katika ujumuishaji wa matokeo kwa siku nzima na ndipo waliposikia kuwa ametangaza kufuta uchaguzi bila kuwashirikisha wajumbe wengine wa tume hiyo na baada ya hapo ndipo ofisi yetu ilianza kuzungukwa na wanajeshi na kuamuriwa tusifanye lolote huku jaji mkuu wa mahakama ya Zanzibar naye akiwa amekamatwa na kupekwa polisi.

Wamesema kuwa kwa matukio kama hayo wanaamini kuwa tume hiyo imeacha kufanya kazi zake kisheria na sasa inafanya kazi kisiasa jambo ambalo linampotezea sifa mwenyekiti wa ZEC kuendelea kuiongoza tume hiyo.

Aidha wamesema kuwa hali iliyopo ndani ya tume kwa sasa sio hali ya kawaidia ambayo inaweza kusimamia uchaguzi wa haki kwani wajumbe wamekuwa wakipingana kwa kila hoja inayoletwa jambo ambalo linafanya uchaguzi wa marudio kutiliwa mashaka na wajumbe wengi wa tume hiyo.
Wajumbe hao wa ZEC wametoa wito kwa wajumbe wengine ndani ya tume hiyo kuacha kufwata mkumbo na kuamua kusimamia sheria inavyosema ili kuwapatia wazanzibar haki yao ya kikatiba

No comments: