WANAHARAKATI WATILIA SHAKA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA SERIKALI YA MAGUFULI,WAMKUMBUSHA JAMBO


Mkurugenzi mtendaji wa TGNP LILIAN LIUNDI akifafanua jambo mbele ya wanahabari mapema leo katika mkutano huo
 Wanaharakati wa maswala ya jinsia nchini Tanzania wametilia shaka  ushiriki wa wanawake katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ikiwa ni siku mia moja za uongozi huo ambapo wamehoji kushushwa kwa kiwango cha wanawake waliochaguliwa katika sehemu muhimu za maamuzi katika serikali,

Mwenyekiti wa mtandao wa wanawake katiba na uchaguzi Bi RUTH MEENA akizungumza na wanahabari katika mkunao huo.
Katika mkutano wa wadau mbalimbali wa jinsia uliondaliwa na mtandao wa jinsia nchini TGNP uliokuwa na lengo la kujadili siku mia moja za uongozi wa awamu ya Tano, baadhi ya wanaharakati wamepongeza kasi aliyoanza nayo Raisi wa Tanzania DR JOHN POMBE MAGUFULI hasa katika hatua yake ya kupambana na ubadhilifu na kutaka kurudisha rasimilimali kwa wananchi wenyewe jambo ambalo wamelitaja kuwa ni moja kati ya mambo ambayo yalikuwa yanapiganiwa na wanaharakati mbalimbali nchini kwa miaka mingi iliyopita.

Akizungumza na wanahabari katika mkutano huo mkurugenzi mtendaji wa TGNP LILIAN LIUNDI amesema kuwa moja kati ya changamoto kubwa zilizojitokeza na zikawashangaza baadhi ya watanzania ni kuhusu swala la kuwashirikisha wanawake katika uongozi hasa baada ya uteuzi wa baraza la mawaziri na makatibu wakuu ambapo imeoneana wazi kuwa wanawake hawakupewa kipaumbele kama ilivyokuwa kampeni ya 50 kwa 50 katika serikali ya awamu ya nne.

Amesema kuwa uteuzi wa Makamu wa Rais mwanamke ilikuwa ni hatua moja nzuri ambayo ilipongezwa na kila mtanzania na watetezi wa haki za jinsia walijua ndio mwanzo wa wanawake kupewa nafasi kubwa katika serikali hiyo lakini Jitihada hizo zimeonekana kuanza kufifia kutokana na uteuzi anaoendelea kuufanya Mh Rais Magufuli,

Aidha baadhi ya washirilki wa mkutano huo akiwemo mwenyekiti wa mtandao wa wanawake katiba na uchaguzi Bi RUTH MEENA akizungumza na wanahabari amekiri wanawake kutokupewa kipaumbele kikubwa kama ilivyotarajiwa na wanaharakati wengi ambapo amemkumbusha Rais Magufuli kukumbuka kuwa Tanzania kuwa wanawake wengi ambao wanaweza kufanya kazi kubwa kama inavyoonekana kwa baadhi ya waliochaguliwa kwenye baraza lake hivyo katika Uteuzi wake ujao ahakikishe kuwa anawakumbuka wanawake kwa wingi.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.