Wateja wa Tigo, AzamTV na LigaBBVA kwenda kuangalia mechi ya Barcelona bure

 Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya kujishindia safari ya kwenda kushuhudiamechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu .  Katikati yake  ni Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta.Kulia kwake Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam TV, Mgope Kiwanga .Promosheni  hiyo ya ushirikiano wa Tigo Pesa na Azam TV, inaanza rasmi leo hadi Machi 13 na washindi wawili watakwenda Hispania.
………………………………………………………………………………………………………..  
 
Tigo, Azam Media na LigaBBVA leo wametangaza
ushirikiano baina yao ambao utawapa fursa watumiaji wa huduma
Tigo Pesa
wanaonunua vifurushi vya  michezo vya AzamTV
kupata nafasi ya kusafiri bure bila malipo kwenda kutazama mechi ya ligi kuu
kati ya miamba wawili wa Hispania – Barcelon na Deportivo la Coruna
– itakayofanyika Aprili mwaka huu.
 
Akiongea katika uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam,
Meneja wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta amesema, “Kwa kufahamu mapenzi
makubwa waliyonayo watanzania kwa mpira wa miguu hasa ligi kuu ya Hispania,
Tigo imeungana na Azamtv na LigaBBVA ili kuwapa watanzania, hususan wateja wa
Tigo Pesa fursa hii adimu na bure ya kusafiri na kwenda kutazama mechi kati ya
Barcelona and Deportivo la Coruna itakayochezwa Aprili 17.”
 
Rutta alisema: “Mtumiaji wa Tigo Pesa anachohitaji kufanya kushinda
fursa hii ni kuhakikisha kimoja kati ya vifurishi vikuu vya AzamTV kipo hewani (Pure,
Plus, Play) na hapo atakuwa ameingia katika droo ya kumpata mshindi wa kwenda
kushuhudia mechi hii ya kusisimua. Tunapenda kuwahimiza wateja wa Tigo
watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa kuchangamkia fursa hii ya kusafiri bila malipo
kwenda Hispania.”
 
Tigo, kwa mujibu wa Meneja wa Promosheni wa Tigo Pesa huyo, ina zaidi ya
wateja milioni tano waliojisali katika huduma ya Tigo Pesa waliopo kila kona
nchini Tanzania
 
Akiongea katika uzinduzi huo. Mkurugenzi Mtendaji
wa Azam Media, Rhys Torrington alisema, “Kama kawaida yetu, malengo yetu daima
ni kuwapa kilicho bora zaidi wateja. Nchini Tanzania tunafahamu ni jinsi gani
watu wanavyopumua, kula na kuishi mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. Hii ni
sababu iliyotupa msukumo wa kuleta LigaBBVA ambayo ni mojawapo katika ligi bora
duniani kwa mashabiki wengi Tanzania ili kukata kiu yao ya mpira wa miguu.
Alisema “nafasi kama hizi hazijitokezi kila mara kushuhudia maajabu ya Messi,
Neymar na Suarez yakitokea”.
 
Tunapenda kuwahimiza mashabiki wote wa mpira wa miguu nchini Tanzania
kutumia fursa ya kipekee kutimiza kutumiza ndoto zao katika maisha.” Mbali na
washinfi wawili watakaosafiri kwenda nchini Hispania katika kipindi cha
promosheni hii, aidha zitatolewa zawadi mbalimbali kwa washindi zikiwemo jezi
asili za timu ya Barcelona, mipira ya miguu, mipira, tisheti, kalamu, miwani ya
jua na zawadi nyinginezo. Ili kushinda zawadi. watazamaji wa mechi za LigaBBVA kupitia
AzamTV watahitajika kupiga simu kabla ya mechi kuanza na wakati wa mapumziko na
kujibu maswali yatakaokuwa yanaulizwa.  
  
Torrington alisisitiza “ LigaBBVA ambao tunashirikiana nao, wamefurahishwa
na mapokezi mazuri ya watanzania kwa ligi ya ligi ya Uhispania kuanzia siku ya
kwanza, na katika kuunga mkono promosheni hii wametukabidhi vifaa vyenye nembo
ya LigaBBVA vitakavyotolewa kwa kwa washindi wa kila wiki na tunaamini huu ni
mwanzo wa mambo makubwa yajayo.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.