Monday, March 21, 2016

DKT. ALI MOHAMMED SHEIN ASHINDA URAIS WA ZANZIBARKWA ASILIMIA 91.4, NI USHINDI MKUBWA KATIKA HISTORIA YA ZANZIBAR MIAKA YA KARIBUNI



Dkt. Ali Mohammed Shein (pichani), ametangazwa leo Machi 21, 2016, kuwa ameshinda uchaguzi wa marudio wa Zanzibar kwa asilimia 91.4, ushindi ambao umeelezwa kuwa ni mkubwa kwa kiongozi wa Zanzibar usinda katika miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo Dkt. Shein amepata ushindi huo katika mazingira ambayo, chama kikuu cha upinzani visiwani humo yaani CUF, kiliususia uchaguzi huo kwa maelezo kuwa uchaguzi wa marudio si wa haki kwa vile uchaguzi ulikwishafanyika Oktoba 25, 2015 ambapo chama hicho kilielekea kushinda. Hata hivyo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC), Jecha Slim Jecha, aliufuta uchaguzi huo kwa maelezo kuwa ulijawa na ghiliba na haukuwa huru na wa haki.

http://www.jamiiforums.com/attachments/matokeo-jpg.331454/
Kwa mujibu wa matangazo ya leo ya matokeo ya uchaguzi huo wa Zanzibar, Mwenyekiti Jecha alisema, anayemfuatia Dkt. Shein, amepata asilimia 3.4 ambapo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, chama kinachofuatia kile kilichoshinda, ndicho kitatoa makamu wa kwanza wa rais.

No comments: