WABUNGE WA MTWARA WAMEAMUA HAYA KUHUSU AHADI ZA MAGUFULI ZA BARABARAWabunge wa Mtwara wameahidi kwenda kumuona Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa lengo la kumkumbusha ahadi zake za ujenzi wa barabara  alizozitoa katikakipindi cha kampeni ambazo mpaka sasa hazina daliliyoyote ya kujenga.

Hiyo inatokana na kutengwa Sh3.5 bilioni pekee kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na ahadi yake ya Sh 60 Billioni ambayo ilielekezwa katika ujenzi wa kilomita 210 lakini mpaka sasa hakuna pesa inayoonekana kuongezeka.
Hatua hiyoilikuja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha bodi ya barabara baadhi ya wabunge wa mkoa wa Mtwara wanasema Rais alitoa ahadi za ujenzi wa barabra lakini hakuna dalili zozote zinazoonesha utekelezaji wake na badala yake pesa iliyopo ni shilingi Billion3.5 pekee.


Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Katani katani anasema raisi Magufuli wakati wa kampeni aliahidi ujenzi wa barabara ya Mtwara-Nanyamba-Tandahimba-Newala hadi Masasi lakini hamna dalili.

“Rais aliahidi wapiga kura wa Mtwara kuwa ile barabara imetengewa pesa zaidi ya 60 bilioni lakini leo jambo la ajabu kwenye kikao cha bodi ya barabara tunapewa sanaa za 3.5 bilioni ambazo haziwezi kufanya kitu chochote maana huwezi huwezi  kuzungumzia suala la km210 afu unatoa ahadi km 50 afu kwenye bajeti hamna hata km 5.

Naye mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe alisema wakulima wa eneo lake wamekuwa wakijihusisha na kilimo lakini wakulima wamekuwa wakipata shida ya barabara kwa ajili ya kusafirisha mazao sambamba na serikali kupeleka kiasi kidogo cha bajeti.

“Tunacheleweshwa  kwenye mambo mengi sababu ya barabara,kuwa na barabara ni jambo moja na kuwa na barabara inayopitika ni jambo jinginekwasababu sehemu kubwa ya ananchi wangu ni wakulima hawana barabara wanashindwa kusafirisha mazao yao toka eneo moja kwenda jingine,”alisema Mwambe na kuongeza

“ Tunafikiri sasasserikali ifikie mahali itekeleze ahadi zake za msingi unapoambiwa utaletewa 7blioni kwaajili ya kutengeneza barabara halafu unaletewa 5bilioni kunakuwa na upungufu,pesa wanayokuwa wameitenga ni ndogo huwezi kufanya jambo,pia ni vizuri kuamua leo tunaanzia hapa tunamalizia sehemu Fulani kuliko leo unajenga hapa kesho unajenga pale tunakuwa hatuwezi kumaliza barabara zetu,”alisema Mwambe

Hata hivyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego alisema bado wanaendelea kuwasilina na wizara husika ili kuweza kupata pesa na kukamilisha ujenzi wa barabara.

Kikao cha Bodi ya  barabara KInachokutanisha wabunge pamoja na viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa kwa lengo la kutazama maendeleo yanayopaswa kufanyika katika sekta ya ujenzi wa Barabara kwa mkoa Mtwara.’


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.