WATANZANIA WAULA CAF


Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi watakaochezesha na kusimamia michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC), kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) pamoja na kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) mwaka 2017.


Michael Richard Wambura ameteuliwa kuwa Kamisaa wa Mchezo Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) kati ya Al Shandy ya Sudan dhidi ya FC Lupopo mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili nchini Sudan.
Mwamuzi Israel Mujuni akisaidiwa Frank Komba na Soud Lila, mwamuzi wa akiba akiwa ni Mfaume Ali Nassoro katika mchezo kati ya Renaissance Football Club (Chad) v E.S.T. (Tunisia) wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) nchini Chad.
Mchezo namba 97 wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kati ya Lesotho v Shelisheli Machi 29, 2016 utachezeshwa na Israel Mujuni akisaidiwa na Ferdinand Chacha, Samuel Mpenzu huku mwamuzi wa akiba akiwa Waziri Sheha.
Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atachezesha mchezo kati ya Burundi v Congo DR kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20), Aprili 4, 2016 mjini Bunjumbura akisaidiwa na Frank John Komba, Alli Kinduli, huku Martin Eliphas Saanya akiwa mwamuzi wa akiba.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.