Sunday, April 10, 2016

Bulembo: Lowassa ni Fisadi, Namshauri Amwache Rais Magufuli na Badala yake Aende Kijijini Kuchunga Ng'ombe


Mwenyekiti wa  Jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo amemtaka waziri mkuu wa zamani Edward  Lowassa  amwache Rais Magufuli aendelee kufanya kazi zake.

Bulembo anakuwa kiongozi wa pili wa CCM kumvaa Lowassa aliyekosoa utendaji wa Rais  Magufuli  wa kutumbua majipu wakati  alipokutana na wanazuoni wa ndani na nje ya nje Alhamisi ya wiki hii, baada ya juzi  msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka  naye kumkosoa kuwa si kweli  kwamba watumishi wa umma wanafukuzwa bila kusikilizwa.

Akizungumza  mjini  hapa jana na wanachama wenzake wakati wa maadhimisho ya miaka 61  ya Jumuiya  hiyo yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro, Bulembo  alimtaka Lowassa  kutekeleza ahadi yake ya kwenda  Monduli kuchunga  ng'ombe  kama hatochaguliwa kuwa Rais.

"Kama yeye anasema kasi ya Magufuli ni ya muda au anakosea kutumbua majipu, basi tunamkumbusha kauli yake wakati akiongea na vyombo vya habari kuwa  akishindwa urais atarudi kijijini kwake kuchunga ng'ombe, tunaomba aende akafanye kazi aliyoahidi. " Alisema Bulembo.

Alisema anashangazwa na Liwassa aliyekuwa mgombea urais mwaka jana kupitia Chadema  chini ya mwamvuli wa UKAWA  kusema ndani ya CCM kumejaa ufisadi wakati yeye ni fisadi namba moja.

Katika hatua nyingine,  Bulembo  alisema ndani ya CCM kuna majipu yanayohitaji kutumbuliwa wakiwemo  Wasaliti.

Alisema  wanasubiri Rais Magufuli akabidhiwe uenyekiti wa CCM mwezi wa saba mwaka huu ili waanze kuyatumbua majipu hayo

No comments: