Tuesday, April 5, 2016

HATIMAYE ILE REPOTI YA UCHAGUZI KUTOKA KWA WAANGALIZI WA NDANI TACCEO YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji FRANSIS MUTUNGI akikata utepe wa uzinduzi rasmi wa Report ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 iliyoandaniwa na mtandao wa asasi za kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO.Pembeni yake ni mwenyekiti wa mtandao huo MARTINA KABISAMA na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC HELLEN KIJO BISIMBA wakushughudia Tendo hilo
 Na Exaud Mtei
Mtandao wa asasi za kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO kwa kushirikiana na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC leo wamezindua rasmi report yao ya uangalizi wa uchauzi wa mwaka 2015 uliofanyika nchini Tanzania huku report hiyo ikieleza baadhi ya mambo mbalimbali ambayo yalikuwa kama Changmoto katika uchaguzi huo.
Baada ya kuzinduliwa Rasmi wakionyesha Report Juu
Report hiyo ambayo imeelezea changamoto na mafanikio ya uchaguzi mkuu uliomalizika mwaka jana imeelezea mambo yote kuanzia katika mchakato wa uadikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura hadi kufikia hatua ya kupiga kura na mchakato wa utangazwaji wa matokeo ya uchaguzi ambao ulimazika kwa Rais JOHN POME MAGUFULI kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Tazania.
Afisa na mwanasheria  kutoka katika mtandao huo wakili HAMIS MKINDI akielezea mambo kadhaa yaliyomo ndani ya Report hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi huo
Akifafanua kuhusu report hiyo jijini Dar es salaam afisa kutoka katika mtandao huo wakili HAMIS MKINDI amesema kuwa kumekuwa na changamoto kadhaa ambazo zimeanishwa katika report hiyo ambazo serikali,tume ya uchaguzi,na wadau wote wanapaswa kuzisoma ili kuzifanyia kazi kwa ajili ya maadalizi ya uchaguzi mkuu ujao.
Msajili wa vyama vya siasa akikabidhiwa copy yake na mwenyekiti wa TACCEO Bi Martia Kabisama
Akizitaja baadhi ya changamoto hizo amesema ni pamoja na kukosekana kwa elimu ya uraia kwa mpiga kura kwa kiasi cha kutosha kwa katika maeneo mengi ya nchi ,ukosefu wa rasilimali kwa tume ya uchaguzi jambo ambalo liliathiri kwa kiwango kikubwa ufanisi wa tume hiyo,baadhi ya vyama kushindwa kushiriki kampeni za uchaguzi kwa ukosefu wa fedha,pamoja na vyama hivyo kukosa nafasi katika vyombo vya habari kama iliyokuwa inapatikana kwa vyama viwili vilivyokuwa vinasigana vikali.
Wawakilishi kutoka katika vyama kadhaa vya siasa walioshiriki katika tukio hilo
Ameongeza kuwa katika report hiyo ambayo imeandaliwa na TACCEO kwa kushirikiana na LHRC ambao walikuwa na waangalizi wasiopungua 2100 nchi nzima imeelezea pia maswala kadhaa ambayo yalijitokeza kwa mara ya kwanza katika uchaguzi huo likiwemo la ushindani mkubwa uliokuwepo baina ya vyama viwili vya CCM na muungano wa vyama vinne vya upinzani vya UKAWA,ambao umeelezewa kuwa ni ushindani ambao haukuwahi kuonekana tangu kuanza kwa democrasia nchini Tanzania.
Matukio mengine ambayo yametajwa katika Report hiyo ambayo ni nadra kutokea nchini ni pamoja na aina ya kampeni ambazo zilikuwa zikifanyika na vyama viwili vikuu vilivyokuwa vinachuana vikali pamoja na hamasa kubwa iliyokuwa kwa wananchi juu ya uchaguzi huo.

Akizungumza katika haflka hiyo mgeni rasmi msajili wa vyama vya siaa nchini Tanzania Jaji Fransis Mutungi Amesema kuwa pamoja na changamoto zilizotajwa na waangalizi hao lakini pia yapo mambo mazuri yaliyofanywa na serikali hivyo wataitumia Rreport hiyo kushugulikia changamoto hizo ili kuboresha kuelekea uchaugzu ujao.

Katika hafla hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya siasa nchini,wadau wa maendeleo kutoa nchi Tofauti duniani pamoja na wangalizi wa uchaguzi huo mkuu kutoka TACCEO.

No comments: