KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

LUG1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Kangi Lugola, wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Juliana Shonza.
LUG2
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, akiongoza kikao wakati  Kamati hiyo ilipokutana na Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira.
LUG3
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Adadi Rajabu na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
LUG4
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rajabu (wa tatu kulia), wakikagua mojawapo ya samani za ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, ambazo zimetengenezwa na Jeshi la Magereza, wakati  Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
LUG5
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ilipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Wa kwanza kutoka kushoto (waliokaa) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na wa tatu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Rajabu.
LUG6
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho wa  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Alphonce Malibiche, akielekeza jinsi ya kutambua taarifa sahihi za mwombaji wa kitambulisho cha Taifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati Kamati hiyo ilipotembelea Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.
LUG8
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto) mara baada ya Kamati hiyo kumaliza ziara yake katika  Makao Makuu ya Wizara hiyo na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.
LUG9
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto), mara baada ya Kamati hiyo kumaliza ziara yake Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.(Picha na Wizara ya Mambo ya Nchi)

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.