Wednesday, April 6, 2016

TIGO YAWAPA WATEJA WAKE OFA ZAIDI KWENYE WHATSAPP YA BURE

Mkuu wa  Kitengo Kitengo cha Vifaa vya Intaneti wa Tigo David Zakaria akiongea na  waandishi wa habari  (Hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam., kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha (Picha na Maktaba)
Wateja watafurahia ofa hizo wakinunua kifurushi cha shilling 1,000
Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa maisha ya kidijitali imeboresha ofa yake ya WhatsApp ya bure  kwa kutangaza  kuwanufaisha zaidi wateja wake  pindi wanaponunua kifurushi cha kila siku cha extreme kwa shilingi 1,000.
Faida ya nyongeza  inajumuisha muda wa maongezi wa dakika 50, sms bila kikomo, Mb 8 zitakazotumika ndani ya saa 24 pamoja na kutumia WhatsApp bure. Tigo ilianza kuwapa wateja huduma ya WhatsApp bila malipo kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu kila wanaponunua vifurushi vya wiki au mwezi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari  Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Intaneti wa Tigo, David Zacharia,  kuanzia sasa faida za ziada pamoja na WhatsApp ya bure vitatolewa kwa wateja wote pindi wanaponunua  kifurushi cha extreme  cha shilingi 1,000.
“Ofa hii mpya ni kwa wateja walio na simu zenye uwezo wa kutumia huduma ya Intaneti. Hili linaonesha ni jinsi gani tulivyodhamiria kuleta mabadiliko ya kidijitali katika masisha ya wateja wetu na pia tunavyoongoza kwa ubunifu,” alisema Zacharia.
Kwa mujibu wa Zacharia Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10 na Januari mwaka huu ilikuwa ni kampuni ya kwanza nchini kutangaza upatikanaji wa huduma ya WhatsApp bure klwa wateja wake pindi wanaponunua  vifurushi vya wiki au mwezi au kwa kununua kadi mpya ya simu. Mtandao huo wa kijamii unaopatikana kwa watumiaji wa simu za kisasa za smartphone.
WhatsApp ni mtandao dada wa kijamii kwa Facebook  ambao Tigo ilianza kushirikiana nao tangu mwaka 2014 na mwaka 2015  ilizindua Facebook ya kwanza ya kisasa  ikiwa na menyu ya Kiswahili.
WhatsApp ni  huduma maarufu ya simu ya kutuma ujumbe ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania  na watumiaji zaidi ya bilioni moja duniani. Huduma ya mitandao ya  kijamii inawawezesha wateja  kubadilishana taarifa, ujumbe, video na miito ya simu kwa sauti.
Hata hivyo, ili kuifurahia huduma hiyo  kwa mujibu wa Zakaria wateja wote wa Tigo wanatakiwa  kwa kadi ya simu ya 3G au 4G kwa ajili ya kununua kifurushi cha etreme cha shilingi 1,000 kwa kupitia *148*00#  ambayo itakupatia maelekezo Tigo-Tigo ExtremeDaily=1000Ths=50min+UNLIMITED SMS+FREE WHATSAPP.
 

No comments: