Wednesday, April 13, 2016

WAZIRI NAPE NA MAKONDA WAONGOZA MAZIKO YA NDANDA KOSOVO DAR ES SALAAM


085A9851

WAZIRI wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda wamewaongoza mamia ya waombolezaji katika shughuli ya mazishi ya staa wa Muziki aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar,
Mwanamuziki huyo Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ amezikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya Ubalozi wa Congo DRC iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo alisema wameamua kumzika marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake alioutoa mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika kikao hicho Ndanda alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko Lubumbashi alikozaliwa

IMG_6672
IMG_6702
IMG_6704
IMG_6697
IMG_6626
IMG_6633
IMG_6381
IMG_6443
IMG_6491
IMG_6544
IMG_6589

No comments: