Saturday, May 7, 2016

CHADEMA WAENDELEA KULAANI WABUNGE WAO KUITWA BABY BUNGENI


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) Dar es Salaam Kuu kimesema Chama cha Mapinduzi CCM kimejitukana chenyewe kupitia kauli iliyotolewa na Mbunge wake wa Ulanga Mashariki, Godluck Mlinga kwa kuwaita 'baby' wabunge wa viti maalum wa upinzani.

Kauli ya Mlinga aliitoa juzi bungeni akiwataja wahunge hao wanaotoka vyama vinavyounda Ukawa kwamba sifa yao ya kupata ubunge wa Viti Maaalum ni lazima aitwe 'baby.' 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa (Chadema) mkoani hapa, Henry Kilewo alisema kauli hiyo ni ya kiiuni na haipaswi kufumbia macho.


"Tunasema hakuna kitu kama hicho, isipokuwa CCM imejitukana yenyewe kwani uenda vitendo hivyo wanafanyiana wao, sasa wanadhani kila chama kinafanya" alisema.
Kilewo alibainisha kuwa wabunge wao wanawake wanatokana na Baraza la wanawake ( Bavicha) ambapo wanapitia katika hatua takribani nne.


"Kila siku tunapambana na mfumo dume lakini inasikitisha kuona watu wachache wanawadhalilisha wanawake," alisema
Naye mbunge Ruth Mollel alisema akiwa kama mama mwenye taalum maneno yaliyotolewa bungeni ni matusi makubwa kwa wanawake.
Alisema wabunge wanawake wanaiwakikisha jamii nzima, hivyo haipaswi watanzania wakafumbia macho kashfa za namna hiyo.


"Kutokana na udhalilishaji huo moja ya hatua tuliyochukua ni kususia vikao vya bunge, pia kwa sasa tupo kwenye mpango wa kujiengua kwenye Chama cha wabunge wanawake TWPG," alisema.
Juzi mbunge huyo wa Ulanga Mashariki (CCM) Godluck Mlinga alitibua hali ya hewa bungeni kwa kutoa lugha ya kejeli, matusi na vijembe dhidi wabunge wa viti maalum wa upande wa upinzani.


Kutokana na kauli hizo za kijeli ikiwemo kuwaita 'Baby' ikimaanisha wamepata nafasi hizo kwa njia ya uzinzi dhidi ya wanaowateuwa ilisababisha wabunge hao kutoka nje ya bunge.


Hatua hiyo ilitokana na kile kilichotafsiriwa kwamba Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson kushindwa kutoa miongozo na kutoridhishwa kwa majibu yake.

No comments: