Hatima ya mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema )itajulikana June 30 mwaka huu

Wakili wa mjibu maombi wa kwanza,Tundu Lissu akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kufwatilia kesi hiyo

Hatima ya mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe  (Chadema )itajulikana June 30 mwaka huu baada ya jaji kusikiliza hoja za mwisho toka pande zote hapo June 17.


Kesi hiyo inayosikilizwa na jaji,Winfrida Koroso ilitegemewa kutolewa maamuzi juzi  kama mjibu maombi ana kesi ya kujibu ama hana lakini jaji aliwapa muda wajibu maombi hao kueleza kama watapeleka ama hawatapeleka mashahidi pindi mahakama itakapotoa maamuzi juu ya shauri lao la kupinga hakuna kesi ya kujibu.


Hata hivyo upande wa wajibu maombi walieleza watapeleka mashahidi wawili ambao hapo jana ushahidi wao ulisikilizwa na kupigwa tarehe hadi Juni 17 mwaka huu.
Mwambe alifunguliwa kesi ya kupingwa kwa matokeo na aliyekuwa mgombea mwenzake wa ubunge wa jimbo hilo Oktoba  2015,Mariam Kasembe (CCM) baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa mzima wa kipindi cha kampeni hadi uchaguzi wenyewe.

Katika kesi hiyo ilikuwa na aya tatu mpeleka maombi alidai kulikuwa na mapungufu mengi katika mchakato mzima wa kampeni na kupinga uhalali wa matokeo hayo. 

Aidha mleta maombi aliiomba mahakama itoe tamko uchaguzi wa jimbo hilo ni batili kwasababu haukuwa huru na haki,pia aliomba mahakama kutoa amri ya kwamba uchaguzi urudiwe na kuomba gharama za kesi nzima pia anaomba kitu chochote ambacho mahakama itatoa.

Hata hivyo katika kesi hiyo jaji Koroso alisema ieleweke wazi katika sehemu ya awali ya kesi hiyo mahakama iliweza kutupilia mbali aya mbili za madai ya mlalamikaji baada ya kuona hazina mashiko.

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa mfululizo mahakamani hapo,wakili wa mjibu maombi wa kwanza,Tundu Lissu aliieleza mahakama ushahidi uliotolewa na waleta maombi unakidhana hivyo unapaswa kuangaliwa kwa kiasi kikubwa.

"Shahidi anayetoa ushahidi unaokidhana ushahidi wake unatakiwa usikubaliwe,kwasababu ya tofauti zilizotolewa mahakamani na kwenye kiaopo kukidhana inatakiwa ushahidi wa Shahidi wake usikubalike,"alisema Lissu
Lissu katika kuendelea kumtetea mteja wake aliendelea kusema mleta maombi wala mashahidi hawajaleta ushahidi wowote  wa maana kuthibitisha ushahidi wao .

"Ushahidi pekee wa nyaraka waliowasilisha mahakamani na ukakubalika ni wa fomu za matokeo pekee,mleta maombi alisema hana nyaraka kama video au sauti hivyo ushahidi wa maneno matupu hautoshi lazima nyaraka za uthibitisho,"alisema Lissu
Kwa upande wa makili wa waleta maombi, wakili msomi Elphace Reshagura aliiambia mahakama kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wao unajenga hoja kuna kesi ya kujibu.

Aidha mjibu maombi wa pili katika kesi hiyo ni aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa jimbo la Ndanda ambaye ni mkurugenzi wa wilaya ya Masasi , Beatrice Dominick na mjibu maombi wa tatu ni mwanasheria mkuu wa serikali ambao wote wanawakilishwa na wakili wa serikali  mkuu,Angela Lushagara akisaidiwa na Hangi Chang'a wakili wa serikali.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.