Sunday, May 8, 2016

HATIMAYE CHAMA CHA ADC WAINGIA KATIKA MKUTANO MKUU LEO,MSAJILI AWAMWAGIA PONGEZI

Waziri wa kilimo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar amnbaye ni mlezi wa chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE -ADC nchini Tanzania Mh HAMAD RASHID akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika Jijini Dar es salaam leo(Picha na EXAUD MTEI)
 Baada ya chama cha ALIANCE FOR DEMOCTARIC CHANGE  –ADC kuingia katika migogoro ya kiuongozi ndani ya chama hicho siku za hivi karibuni Hatimaye hali ya Amani imerejea ambapo chama hicho leo kimeingia katika mkutano mkuu uliowakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka kila kona ya nchi.

Katika mkutano ambao umehudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo waziri wa kilimo wa serikali ya Zanzibar ambaye alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho ambaye pia ndiye mlezi wa chama  Mh HAMAD Rashid,viongozi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na wajumbe mbalimbali wa chama hicho.
Makamu mwenyekiti wa ADC Mama ADELA STOLIC akihutubia wakati akifungua mkutano huo Mkuu mapema leo
Akizngumza wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo HAMAD RASHID amesema kuwa chama cha ADC ni chama ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia watanzania,kikiwa na itikadi zake,sera zake na mipango yake hivyo hakipo tayari kufwata sera za chama kingine chochote nchini na swala la kushiriki chaguzi mbalimbali ni moja kati ya sera zao hivyo hawapo tayari kususia uchaguzi wa aina yoyote kwani ndio njia pekee ya kupata viongozi wa nchi.
Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini A SISTY LEORNAD NYAHOZI akitoa hotuba fupi kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa nchini 
Ameleza kuwa chama chake kimeanza mipango kabambe ya kujiimarisha Zaidi kwa lengo la kuwaletea mabadiliko ya kweli watanzania baada ya wapinzani wao waliokuwa wakiongoza serikali iliyopita na sasa hawapo kushindwa kufanya hivyo kwa miaka yote iliyopita hivyo amewataka watanzania kuanza kukiamini chama cha ADC kwani ndio dira pekee ya mabadiliko kwa watanzania kwa sasa.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa viongozi wa chama hicho mara baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama kiongozi huyo amewataka wanachama wa chama hicho wakae tayari kwa kuwa siku yoyote chama kitaitisha uchaguzi wa kupata viongozi wapya.

Naye msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Mh SISTY LEORNAD NYAHOZI akizungumza katika mkutano huo amekipongeza chama hicho kwa kukubali kuingia katika uchaguzi wa marudio Visiwani Zanzibar ambapo walishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 3 jambo ambalo amesema ni ukomavu wa kisiasa kwa chama kichanga kama hicho kushiriki uchaguzi mkubwa kama ule na kupata mafanikio hayo.

Aidha amesema kuwa chama hicho kimeonyesha ukomavu Zaidi baada ya kutokea mtafaruku na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho na kufanikiwa kulimaliza kidemocrasia jambo ambalo amesema linafaa kuigwa na vyama vingine vya siasa nchini.
Chama hicho kilijikuta katika migogoro iliyosababisha hadi kutimuliwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wake SAID MIRAAJ kwa kile kiliichoitwa kukiuka matakwa katiba ya chama ambapo ilielezwa kuwa mwenyekiti huyo alipinga kitendo cha viongozi wa chama  kuingia katika uchaguzi wa Zanzibar wa marudio jambo ambalo alilipinga na kusababisha mtafaruku baina yake na aliyekuwa mgombea wa chama hicho visiwani Zanzibar ambaye kwa sasa ni waziri HAMAD RASHID.

No comments: