Saturday, May 21, 2016

KAMA ULIPITWA NA USHINDI WA MTANZANIA MELISA JOHN KWENYE AIRTEL TRACE MUSIC STAR NIMEKUWEKEA KILA KITU KILICHOJIRI KWENYE FAINALI

Mshindi mpya wa mashindano maarufu ya AIRTEL TRACE MUSIC STAR MELISA JOHN akitumbuiza katika mashindao hayo ambayo yalifanyika Jijini Dar es salaam na kuibuka mshindi wa mashindano hayo kati ya vijana watano waliokuwa wanawania nafasi hiyo na sasa ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Africa
 Mashindano ya Airtel Trace Music Stars ya taifa  yamefikia mwisho ambapo Melisa John alitangazwa kuwa mshindi wakati wa fainalii za shindano hilo lililowashirikisha washiriki watano bora na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Saalam

Baada ya kuimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa mwanamuziki wakimarekani Mica Paris ujulikanao kama “My One Temptation” Melisa aliweza kuwaaminisha majaji kwamba hakika yeye anastahili kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars msimu wa 2
Melisa amejishindia shilingi milion 50 huku mshindi wa pili Nandi Charles akijishindia shilingi milioni 5 na mshindi wa tatu Salim Mlindila akiondoka na shilingi milioni 2
Kufatia ushindi huo Melisa sasa amepata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika yatakayoshirikisha washiriki kutoka nchi 9 zikiwemo Niger, DR Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana and Zambia yanayotegemea kufanyaka tarehe 11 Juni 2016 , Lagos nchini Nigeria.

“Nimefurahi sana kuibuka mshindi leo, pamoja na ushindi huu mashindano yalikuwa ni ya ushindani kwani kila mshiriki alikuwa na uwezo wa kuimba na mzuri kwa namna tofauti. Nashukuru Mungu kwa kunifikisha hapa na nawashukuru Airtel kwa kutuandalia jukwaa hili ambapo leo limenifanya niweze kuishi ndoto zangu. 

Wadau mbalimbali waliopata nafasi ya kushighudia fainal hizo usiku wa jana Jijini Dar es salaam

Napenda sana kuimba na napenda sana mziki naamini huu ni mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mwanamuziki nyota” alisema Mshindi wa Airtel Trace Music Stars 2016 Melisa John
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema “ Airtel inajivunia kuwa sehemu ya kuinua maisha ya vijana wengi, tunaamini kupitia program zetu za kuwawezesha vijana tutagusa maisha ya vijana wengi na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao. Tumefurahia mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto zaidi na tunampongeza Melisa kwakuibuka kuwa mshindi. Tunamtakia afanye vyema katika michuano ya Afrika nchini Nigeria.”
Katika fainali hizo Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alitoa burdani ya nyimbo yake ya “ Nice Couple”na kuweza kuzindua kibao chake na video yake ijulikanayo kama “ Please don’t go away” e inayomshirikisha mwanamuziki nguli kutoka marekani, Akon




Msanii wa music wa kizazni kipya na star wa Nyimbo ya AFRICAN DRUM KLEYAH akiwa katika fainali hizo jana



Mshindi aliyevua taji la Mashindano hayo jana MAYUNGA akitoa burudani katika fainali hizo huku akishighudia MELISA JOHN akichukua taji lake kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Africa


Furaha ya usindi
Msanii BAGDAD naye alikuwepo





No comments: