CHAMA CHA ADC WAVUNA WANACHAMA WAPYA 250,WAPO WANAOTOKA CCM,CHADEMA NA CUF. NI HUKO TANGA

Moja ya mafanikio makubwa ya Chama chochote cha siasa ukiachana na kushika Dola ni kuwa na rasilimali watu ambayo ndiyo chachu kubwa inayowapa nguvu kuyafikia malengo yao kirahisi.

Hivi karibuni chama cha Allience for Democratic Change (ADC) kilitangaza kuanza ziara nchi nzima ambapo walitangaza kuanza na mkoa wa Tanga kwa malengo ya kujitambulisha kwa wakazi wa mkoa huo, kutoa shukrani kwa kura walizopigiwa katika uchaguzi wa Oktoba 2010 na kushika nafasi ya nne kati ya vyama nane, halikadhalika kusajili wanachama wapya.

 Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo amesema kuwa ziara waliyoifanya siku ya jumamosi mkoani Tanga maeneo ya Mabanda, Misima, Chanika, Konje na Vibaoni ya wilayani Handeni imekuwa ya mafanikio kwao tofauti na matarajio yao.

Doyo amesema moja ya kitu ambacho wanajivunia ni mapokezi makubwa kwa wakazi wa Tanga, huku wakifanikiwa kusajili wanachama zaidi ya 250 katika maeneo tajwa hapo juu, ambapo kati ya wanachama hao wapya wanachama 40 wanatoka chama cha CUF, CHADEMA na CCM.

Pia ameongeza kuwa siku ya leo wataendelea na ziara hiyo maeneo ya Handeni mjini wakiambatana na viongozi waandamizi wa Chama akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Hamad Rashid ambaye pia ni waziri wa kilimo Zanzibar

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.