Tuesday, May 10, 2016

MSIMAMO WA ACT WAZALENDO JUU YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR



Gazeti la Nipashe Toleo Na. 0578842 la tarehe 7, Mei, 2016 katika ukurasa wa 4 lina habari yenye kichwa cha habari “ACT Yatoa Msimamo Muhimu Zanzibar”. Kwenye habari hiyo iliyoandikwa na mwandishi anayetambulishwa kwa jina la Mwinyi Sadallah kutoka Zanzibar, ananukuliwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar Ndugu Ramadhan Suleiman Ramadhan kuwa Chama cha ACT Wazalendo kimemtambua Rais Shein na serikali yake baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016.

Tunapenda kuuarifa umma kuwa habari hiyo haina ukweli wowote. Msimamo wa Chama chetu kutoutambua uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 20 Machi 2016 unafahamika na umeshawasilishwa kwa umma kupitia taarifa zetu za nyuma. Chama cha ACT hakijawahi kutoa tamko lolote halali kwa mujibu wa Katiba na taratibu za Chama kumtambua au kutomtambua Dk. Shein na serikali yake.

Hivyobasi, yaliyoelezwa na Makamu Mwenyekiti Zanzibar kupitia gazeti la Nipashe ni maoni yake binafsi na wala si maoni ya Chama cha ACT Wazalendo.
Ado Shaibu,

Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
ACT Wazalendo.
Imetolewa leo Mei 10, 2016

No comments: