Sunday, May 8, 2016

SERIKALI YAIPONGEZA TAASISI YA DHI NUREYN KWA KUOKOA MAISHA YA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO

DSC_3050
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation na washirika wake zilizofanikisha zoezi la kambi ya Moyo kwa watoto iliyokuwa katika Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo imemalizika juzi.
Serikali kupitia WIzara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imepongeza juhudi za Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Kiislam ya hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn Islamic Foundation kwa juhudi zake za kuunganisha nguvu na taasisi zingine za nje  katika kuokoa  maisha ya watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.
DSC_3035
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri  akiabidhi tuzo kwa mgeni rasmi, Mh. Dk. Kigwangalla kwa namna Serikali inavyothamini mchango wa taasisi binafisi hapa nchini.
Akizungumza wakati wa hafla maalum ya kufunga kambi ya Moyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali inatambua juhudi za taasisi binafsi katika kusaidiana nazo hivyo kwa hatua hiyo, suala la magonjwa ya moyo ambayo awali yalikuwa yakitibiwa nje kwa sasa yatashughulikiwa hapa hapa nchini.
“Tunaishukuru taasisi ya Dhi Nureyn na taasisi zote kwa kushirikiana na taasisi ya JKCI, kwani zimeweza kusaidia kuokoa maisha ya watanzania ikiwemo kuokoa vifo ambavyo vingetokea kwa watoto wenye matatizo ya moyo.
Zoezi hili limeweza kuvuka lengo la asilimia 70. Kwa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu hayo ya moyo.  Tunaamini mwaka huu tukaongeza malengo,  na tayari wameweza kufanya operesheni takribani 200. Hii ni misheni ya pili na kwa maana hiyo wameweza kuvuka malengo ya asilimia 70 yale tuliyowapa.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Na kuongeza kuwa, Awali kabla ya utaratibu  wa JKCI, wagonjwa 250 walikuwa wanapelekwa nje kufanyiwa operesheni hizo za magonjwa ya moyo. Lakini kwa mwaka huu hata miezi sita bado haijafika, Wagonjwa zaidi ya 200 wameshafanyiwa hapa hapa nchi operesheni hizo. Kwa hatua hiyo wameweza kuvuka lengo la asilimia 70 na wanataka wafikie angalau wagonjwa 400 hadi 500 kwa mwaka” alimalizia Dkr. Kigwangalla.
DSC_3089
Picha  ya pamoja ya madaktari na wageni waalikwa akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla wakati wa hafla hiyo ya kufunga kambi ya Moyo Muhimbili.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri  alieleza kuwa, taasisi hiyo imekuwa kiungo kuzitafuta taasisi zingine za nje ya nchi na kuleta wataalam hao wa bingwa wa magonjwa ya moyo hapa nchini ni faraja kubwa kwa taasisi hiyo na Watanzania wote kwani imeweza kuokoa maisha ya watoto hapa nchini.
Miongoni mwa taasisi hizo  zilziofanikisha kambi hiyo ya Moyo hapa nchini ni pamoja na Taasisi ya  Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktai kutoka Saud Arabia, Taasisi ya RAF kutoka Qatar, Taasisi ya Dhi Nureyn (Tanzania) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Tanzania). Zoezi hilo la kambi ya magonjwa ya moyo ni la pili kufanyika hapa nchini  likiwemo la kwanza la mwezi Mei mwaka jana (2015) na kufanikiwa kuwatibu watoto 66 wa Kitanzania ambao walipangiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na kufanya kuokoa mabilioni ya shilingi ya Serikali kwa ajili ya gharama za matibabu hayo.
“Tunaishukuru sana taasisi ya Muntada Aid, kwa kujali, kuthamini na kujitolea kufanya kazi hii iliyookoa maisha ya Watoto weyu. Pia iliyowaondoshea maumivu watoto na wazazi wao na kuwapa matumaini mapya ya maisha. Pia tunaishukuru Serikali ya Saud Arabia, Taasisi ya Jakaya Kikwete  na Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla pamoja na washirika wetu wote wakiwemo Taasisi ya Al Akhlaaq na wanahabari na wote kwa ujumla pamoja na mdaktari wa hapa ndani. Nashukuru sana” alimalizia Sheikh Said Ahmed Abri wakati wa kutoa hutuba yake hiyo kwa wageni mbalimbali pamoja na madaktari hao.
Aidha, madaktari hao pamoja na taasisi zote zilizofanikisha zoezi hilo, zilitunukiwa vyeti na tunzo maalum kwa ajili ya shukrani.
DSC_3112Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo. Kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Ahmed Abri  DSC_3128Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipiga picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa Moyo . Mwenye kanzu nyeupe  ni  Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Ahmed Abri, akifuatiwa na  Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo, Profesa Joom Joom  na mwingine ni daktari wa magonjwa ya Moyo aliyeambatana na timu hiyo ya madaktari hapa nchini. Na Andrew Chale,Modewjiblog, Dar es Salaam
DSC_3133 Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo, Profesa Joom Joom akielezea jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) namna walivyoweza kufanikisha Operesheni zilizofanyika hapa nchini hasa kwa watoto waliokuwa na matatizo ya Ugonjwa wa Moyo. Operesheni hiyo maalum ilifanyika kuazia Aprili mwaka huu na kumalizika mwezi huu wa Mei. Hafla hiyo imefanyika jana Mei 6.2016 Jijini Dar es Salaam (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

No comments: