Thursday, May 12, 2016

Shirika la ndege la Ethiopia Airlines kusafirisha abiria waendao tamasha la ZIFF


2Mkurugenzi Mtendaji wa Tamasha la ZIFF, Profesa Martin Mhando na Meneja Mkuu wa Shirika la ndege la Ethiopia kwa Tanzania na Comoro, Bi Milat Mekonen wakikabidhiana nyaraka baada ya kumaliza kutiliana saini za makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, mapema leo Mei 12.2016. Wengine wanaoshuhudia ni viongozi wa viongozi wa ZIFF na Ethiopia Airlines
[???????????????????????????????????? Mkurugenzi Mtendaji wa Tamasha la ZIFF, Profesa Martin Mhando (Wa pili kutoka kushoto) akitia saini makubaliano baina ya ZIFF na shirika la ndege la Ethiopia. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Shirika la ndege la Ethiopia Tanzania na Comoro, Bi Milat Mekonen. Wengine wanaoshuhudia ni viongozi wa viongozi wa ZIFF na Ethiopia Airlines.???????????????????????????????????? 

Meneja wa Tamasha la ZIFF, Dean Nyalusi (kushoto) na Afisa Masoko mwandamizi wa shirika hilo la Ethiopia, Bi. D'Silva wakiisaini mkataba huo wa ushirikiano.???????????????????????????????????? 
  Meneja wa Tamasha la ZIFF, Dean Nyalusi (kushoto) na Afisa Masoko mwandamizi wa shirika hilo la Ethiopia, Bi. D'Silva wakiisaini mkataba huo wa ushirikiano ???????????????????????????????????? Meneja Mkuu wa Shirika la ndege la Ethiopia kwa Tanzania na Comoro, Bi Milat Mekonen akielezea machache wakati wa hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam. DSC_3104Tukiohilo likiendelea leo Jijini Dar es Salaam . (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).



Shirika la ndege la Ethiopia Ethiopia Airlines limeingia mkataba wa kusafirisha abiria waendao katika tamasha la filamu la Kimataifa la Zanzibar maarufu kama (ZIFF) ndani ya mwezi Julai mwaka huu.

Uongozi wa juu ya ZIFF na Shirika hilo la ndege, mapema leo Jijiji Dar es Salaam, wamesema kuwa, usafiri wa ndege utakuwa rahisi baada ya shirika la ndege la Ethiopia kutoa punguzo la bei kwa wasafiri wote waendao kwenye tamasha hilo huko Zanzibar.

Akizungumza katika hafla za kutia saini makubaliano rasmi kati ya ZIFF na Ethiopian, Meneja Mkuu wa Ethiopian mjini Dar es Salaam, Bi Milat Mekonen, alisema kuwa shirika lake litatoa tiketi 5 kwa wageni mashuhuri wa ZIFF mwaka huu.
“Shirika liliamuwa kuwa mdhamini wa tamasha ili kuongeza kasi ya ukuwaji wa tasnia ya filamu Tanzania, na Afrika, na kuzidisha huduma zake na kujitangaza kwa wateja.

ZIFF ndio tamasha kubwa kuliko yote hapa Afrika ya Kati na ya Mashariki likiwafikia wadau zaidi ya 100,000 na kuwavutia watalii wasiopungua 6000 kila mwaka. Tamasha ni kivutio kikubwa cha watalii toka nje na ndani likichangia uchumi wa Zanzibar ambao unaotegema sana utalii. Kwa sababu hiyo kudhamini tamasha kunatoa fursa kubwa kwa mashirika kujitangaza na kutambulisha biashara zao.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa tamasha Profesa Martin Mhando alisema, “Udhamini huu ni muhimu kwa ZIFF maana misaada ya kifedha kwenye shughuli za kitamaduni imepungua sana kwa hiyo mashirika ya kibiashara yanaweza kutumia fursa za matamasha kama ZIFF kukuza biashara zao. Alisema hilo ni jambo la kawaida sana duniani na tunawashukuru Ethiopian kwa kuwa mfano kwa mashirika mengineyo”.

Tamasha litakuwepo kati ya tarehe 9 na 17 Julai Visiwani Zanzibar na filamu na muziki unatarajiwa kupamba. Pia ni miongoni mwa matamasha makubwa kwa ukanda huu wa Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo watu mbalimbali kutoka Duniani kote ukusanyika visiwani humo.

No comments: