TIGO YATOA KOMPYUTA 20 ZILIZOUNGANISHWA NA INTANETI KWA SEKONDARI 3 MTWARA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego(katikati) akikata utepe katika makabidhiano ya kompyuta ishirini zenye thamani ya 33m/- zikiwa na huduma ya intaneti ya bure iliyo gharimu 22m/- katika Shule ya Sekondari Sino,mkoani Mtwara, kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwana Goodluck Charles, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatuma 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego(katikati) akitoa hotuba kwa wakazi wa mtwara na wanafunzi  katika makabidhiano ya kompyuta ishirini zenye thamani ya 33m/- zikiwa na huduma ya intaneti ya bure iliyo gharimu 22m/- katika Shule ya Sekondari Sino,mkoani Mtwara, kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwana Goodluck Charles, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatuma A

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sino,mkoani Mtwara wakimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego, vipi wanavotumia kompyuta katika masomo yao ya sayansi, kompyuta hizo 20 zenye thamani ya 33m/- zilizounganishwa na intaneti ya bure yenye thamani ya 22m/- zimetolewa na Tigo
Wanafunzi wakishuhudia makabidhiano hayo
 Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania leo imetoa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 33 zikiwa na huduma ya bure ya intaneti iliyogharimu 22m/- kwa shule  tatu za sekondari mkoani
Mtwara. Msaada huo uko katika mkondo wa malengo ya kampuni  ya kuleta mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini.
 
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika Shule ya Sekondari Sino mkoani Mtwara Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles alisema, “Msaada huu kwa shule hizi tatu ni sehemu ya
mkakati wa kampuni wa kuleta mageuzi katika mtindo wa maisha ya kidijitali. Msaada huu wa leo umekuja baada ya kukabidhi kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Chuda mkoani Tanga  na kompyuta 25 zilizounganishwa na intaneti kwa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure mkoani Mwanza mwaka jana.
 
“Msaada kwa shule ya Sekondari ya Masasi, Tandahimba na Sino ni kielelezo cha kweli cha uwekezaji wa Tigo katika miradi tofauti yenye mchango kijamii kupitia mkakati wetu wa kuwekeza kijamii unaowezesha jamii kupokea zana za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katikanyanja zote za kijamii ikiwemo sekta ya elimu,” alisema Charles.
 
Tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego ambaye alizitaka sekta binafsi kuisaidia serikali katika mikakati yake katika kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zilizopo nchini.
 
Dendego alisema, “Naipongeza Tigo  kwa ukarimu wao wa kuzisaidia shule hizi natoa wito kwa watu binafsi kampuni za biashara na wadau wengine kujitokeza katika kuunga mkono juhudi za kuboresha
sekta ya elimu.”
 
Akipokea msaada huo kwa niaba ya wakuu wenzake wa shule za sekondari, Mkuu wa Shule ya Sekondari Sino Riyadh Kadhi alisema kwamba kompyuta hizo zitawawezesha wanafunzi kuwa na uelewa wa kiteknolojia na kuwawezesha  kuipata teknolojia ya habari mapema katika elimu yao. “Tunafurahi kwa hatua hii ya Tigo; tuna
matumaini kwamba  kompyuta hizi zitawaweka wanafunzi wetu katika ngazi moja na wenzao katika mashule mengine yaliyo maeneo ya mjini na duniani kwa ujumla,” alisema Kadhi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.