Tuesday, May 10, 2016

UKAWA WAMALIZANA NA MKURUGENZI WA ILALA,SASA WAMACHINGA WATAKIWA KUONDOKA HARAKA SANA

MEYA NA MKURUGENZI ILALA (5)
Pichani ni Meya wa Manispaa ya Ilala,Charles Kuyeko akizungumza na Waandishi wa habari


HATIMAYE mgogoro uliopo kati ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Isaya Mnguruni kuhusu  hatua ya kuwahamishwa wafanyabiashara ndondogo wanaofanya kazi maeneo ya karikoo,mgogoro huo umefikia tamati.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Baada ya Madiwani hao  na mkurugenzi huyo kukubalina kutatua changomoto za masoko ya wafanyabisha hao ambao wanatakiwa kwenda huko.

Awali Mngurumi aliwataka wafanyabishara hao kuondoka kwenye maeneo ya katikakati ya jiji na kuwataka kuelekea masoko ya Pugu,Kivuli,Kigogofresh,Ukonga  na Tabata jijini hapa,ambapo mara baada mkurugenzi huyo kusema hivyo-

Ndipo likaibuka Baraza la Madiwani ambalo kwa kiasi kikubwa linaongozwa na Vyama vya Upinzani kupinga hatua ya wafanyabishara hao kuhama kwa kile wanachokidai kuwa maneohayo wanayokwenda yanachangamoto za maji,umeme,Barabara na huduma za choo,ambazo zitawakwamisha wafanyabishara hao.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini hapa,Meya wa Manispaa ya Ilala,Charles Kuyeko amesema madiwani kwa kauli moja wamelidhia hatua ya Mkurugenzi huyo mara baada ya kuhaidi kutatua changamoto ambazo zilizowafanya wapinga hapo awali.

“Tumekubaliana na Mkurugenzi,baada ya viongozi wa Halmashauri kukubaliana na sisi kutatua changomoto za Barabara kuelekea kwenye masoko hayo,pia wameshaweka huduma ya umeme ambayo mwanzo ilikuwa haipo kwenye masoko hayo,lakini tumeona wameweka huduma ya vyoo lakini haijakamilika,”amesema Kuyeko.

Kuyeko amesema Baraza la Madiwani alikupinga hatua ya wafanyabishara kwenda huku bali walikuwa wanataka kujilidhisha  uwepo wa miundombinu rafiki itakayowasaidia wafanyabishara,

Amesema Wafanyabishara wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo haraka ili kupisha mradi wa Mabasi ya mwendo wa haraka (DART)ambayo yanatarijia kuanza haraka hivi karibuni.

“Kwa mfano maeneo ya Kariakoo ambapo wafanyabisha hawa wanafanya shughuli zao, kuna mradi wa mabasi haya unaanza,kwahiyo nataka watii tu agizo hili,na waende kwenye maeneo tuliowambia kwani mradi huu ukianza lazima tu wanatakiwa kuondoka”amesema Kuyeko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Mngurumi amewapongeza madiwani hao kuungana kwa pamoja katika masuala ya maendeleo huku akiwahadi kutatua changomoto zilizobakia ambao zilikuwa zinatakiwa na  madiwani hao.

Amewataka Wafanyabishara kutii agizo hilo,na kwenda kwenye maeneo hayo aliyotajwa,

Hata hivyo amesema Halmashauri yake haitasita kutumia nguvu kwa wafanyabiahara ambao watakaidi agizo hilo

No comments: