WATED YAWAKUTANISHA WANASHERIA KUJADILI DHANA NZIMA YA MAENDELEO ENDELEVU

Baadhi ya washiriki wa mjadala huo uliofanyika Jijini Dar es salaam Wakiongozwa na katibu wa dhirika la WATED nchini Bi MARIAM MATUI katikati pamoja na mwanasheria DAMAS NDUMBARO na pembeni ni AISHA BADE  wakifurahia jambo baada ya mjadala huo (Picha na Msaka habari)
 Na Exaud Mtei
Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na maendeleo ya wanawake na jamii kwa ujumla la WOMEN ACTION TOWARDS ECONOMIC DEVELOPMENT –WATED leo wameendesha majadiliano maalum na wanasheria mbalimbali nchini kwa lengo la kujadili kwa pamoja dhana halisi ya maendeleo endelevu ambayo yalizinduliwa na wakuu wa nchi mbalimbali mwaka jana ambayo moja kati ya malengio yake lengo ka 16 ni maswala ya uhuru wa sheria na upatikanaji wa sheria katika kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu.
Picha ya pamoja ikiwaonyesha washiriki wakuu wa mjadala huo wakiwa ni wwataalam mbalimbali hususani katika fani ya sheria kutoka katika maeneo mbalimbali wengine wakiwa ni mawakili wa kujitegemea nchini
Majadiliano hayo yalilenga kuwawezesha na kujenga uelewa mkubwa kwa wanasheria mbalimbali ili waweze kutambua wao kama wanasheria wana wajibu gani katika kuwasaidia wananchi na mtu mmoja mmoja kuweza kuyafikia hayo maendeleo endelevu yanayotajwa katika malengo hayo.
Imani Kaduma moja kati ya wanasheria waliopata nafasi ya kutoa michango yao leo 
Mariam Matui ni katibu wa shirika la WATED Tanzania na anaeleza kuwa sababu kubwa ya kuamua kufanya majadiliano hayo ni kutokana na ukweli kwamba bado kuna haja kubwa ya kuhusisha jamii hususani wanasheria waweze kufahamu kwa kina malengo hayo kwakuwa wanasheria ndio wanaosaini na kuandika na kuandaa  mikataba mbalimbali hivyo kama wanasheria wakiwa na uwezo wa kuyadadavua kwa kina hayo maendeleo endelevu itasaidia nchi zetu hususani Tanzania kuweza kuyafikia maendeleo hayo.
Damas Ndumbaro akichangia katika mjadala huo
Imani Kaduma ni moja kati ya wanasheria ambao walipata nafasi ya kuchagia mawazo yake katika mjadala huo uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo katika mchango wake ameeleza kuwa pamoja na Tanzania kuonekana kuwa ina mifumo mizuri ya kutufikisha katika malengo hayo ya maendeleo endelevu lakini bado chagamoto kubwa imebaki katika swala la uongozi ambapo swala la matumizi mabaya ya madaraka limekuwa moja kati ya vizuizi vikubwa katika mataifa mengo barani Africa likiwemo Tanzania ya kuyafikia malengo hayo.
Dr GILES DZOUSA NI MTAALAM WA GOVERNANCE KATIKA ARDHI
Sakata la rushwa pia limetajwa kama moja kati ya mambo yanayorudisha nyuma juhudi za kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu katika mataifa mengi ya kiafrika.Mwanasheria mkongwe nchini DR DAMAS NDUMBARO ameeleza kuwa nchini Tanzania maswala kama migogoro ya ardhi katika vijiji mbalimbali imekuwa ikichangiwa kwa kiasi kukubwa na  maswala ya rushwa ambapo pamoja na viongozi wa vijiji kujua kuwa wanawahujumu wananchi wamekuwa wakirubuniwa kwa pesa na wageni na kujikuta wakiwauzia maendeo ya vijiji ambayo mwishoni huzua migogoro mikubwa na isiyokwisha.
Mshauri wa serikali ya Tanzania kutoka umoja wa mataifa UN Dr CHITRALEKHA MASSEY akichangia jambo katika majadilinao hayo
Katika majadiliano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ubalozi wa Uingereza Jijini Dar es salaam yaliwakutanisha wadau mbalimbali wa maswala ya kisheria wakiwemo washauri wan chi kutoka Umoja wa mataifa,wanasheria wenye uzoefu pamoja na viongozi wa shirika hilo..PICHA NYINGINE ZA TUKIO HILO UNAWEZA KUENDELEA CHINI.asante


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.