Friday, June 17, 2016

ACT YALAANI KUFUTWA UMISETA



 NGOME YA VIJANA, ACT WAZALENDO KULAANI HATUA YA SERIKALI KUSITISHA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA.

 SIKU ya tarehe 13/06/2016  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene aliutangazia Ummma wa watanzania kuwa serikali imeamua kusitisha mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za msingi na  Sekondari Nchini (Umitashumta na Umisseta) ambayo ilipangwa kuanza  kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 13 na kumalizikia Julai 5 Mwaka huu.
Waziri  Simbachawene ameeleza kuwa sababu ya kufanya hivyo ni Kupisha zoezi la Kumalizia Ukamilishaji wa madawati ili kutimiza agizo la Rais la kuondoa Upungufu wa Madawati kwa shule za msingi na sekondari Nchini.


Kwamba fedha ambazo zingetumika katika michezo hiyo zielekezwe kwenye madawati na wadau ambao wangesimamia michezo yote kwa shule ya msingi na sekondari wajikike katika kukamilisha upatikanaji wa madawati hayo

 Sisi vijana wa Ngome ya ACT wazalendo na Taifa kwa ujumla  tunajua Kuwa Wanafunzi si Mafundi wa Madawati, Kazi hiyo ni ya Mafundi Mchundo na Kampuni mbalimbali zilizopewa zabuni ya Utengenezaji wa Madawati husika, hivyo  tunauona Umamuzi huu wa kusitisha Mashindano haya  Kuwa ni Ukiukwaji wa Haki za Mtoto kucheza na Unaondoa Msingi Muhimu wa Taaluma na Michezo Kwa Vijana wa Taifa hili.

Pia ni muendelezo wa mawaziri wa serikali ya awamu ya tano kufanya kazi kwa mihemko pasipo kutafakari athari ya kile wanachotaka kukifanya, Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Tunapinga Vikali na Kulaani Uamuzi huu wa Serikali wa Kukandamiza na Kupora Haki ya Msingi kwa Watoto wa Kitanzania ya Kucheza Bila Sababu za Msingi.
Kazi ya Usimamizi wa Mashindano hayo ni Kazi ya Maafisa Utamaduni Na Michezo wa Wilaya Na Mikoa, hivyo hao wanaoitwa Na Waziri Kuwa ni "Wadau Muhimu  katika uamuzi huo wa Utengenezaji  wa Madawati si Wasimamizi wa Mashindano Haya ya Vijana.

Vijana wa ACT Wazalendo tunajua Kuwa Bajeti ya Fedha za Kugharamia Michezo hii ilipitishwa na bunge kwenye bajeti ya Mwaka 2015/16, tunaona Utaratibu wa Kupeleka Kasma Husika kwenye Matumizi Mengine si tu umewanyima Haki ya Kucheza Vijana wa Taifa hili Lakini pia ni Ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya Serikali.

Mbali na ukiukwaji wa utaratibu katika bajeti iliyopitishwa na bunge pia uamuzi huu wa serikali unazidi kuichimbia kaburi vipaji vya vijana wenzetu ambao wangeweza kupatikana katika michezo hiyo na kuiletea sifa nchi katika siku za usoni
Pia katika uamuzi huu tunaouita kuwa usio na tija kwa Taifa ni wazi serikali imeridhia kukiuka mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto (UN Convention On Rights of The Child). Mkataba huu chini ya ibara ya 31 unahimiza haki ya Kila mtoto kucheza na kupata muda wa ukpumzika (Right to play and rest).

Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2009 lilitunga na Kupitisha Sheria ya Mtoto ambayo Kifungu Cha 8(1) (g) imesisitiza Juu ya Haki za Mtoto kucheza na kupumzika. Usitishaji wa Mashindano haya si tu unavunja Sheria  za nchi yetu na unakiuka Kabisa mkataba wa Umoja wa Mataifa, Hatua Ambayo itaipa Sifa Mbaya nchi yetu Kimataifa.

Ibara ya 3 ya Mkataba huu inataka Maamuzi yote Juu ya hatima ya Watoto na Vijana yafanyike Kwa kuangalia athari zake Kwao, Maamuzi haya ya Serikali hayajazingatia athari husika.
Vijana wa ACT Wazalendo tunaamini Kuwa Serikali ya CCM haijui na haithamini Umuhimu wa Michezo kwa Watoto na faida ya Mashindano ya Umitashumta na Umisseta Taifa.

maamuzi haya Mabaya ya Serikali ni ya kuwakatisha tamaa wadau wa Michezo Na Sanaa Nchini, Na yanabinya fursa ya Uvumbuzi wa Vipaji vya Watoto na Vijana. Ni muhimu Serikali ijue kuwa Michezo sio nyongeza, Michezo sio ziada, Michezo ni Haki ya Watoto kama zilivyo haki nyingine.

Vijana wa ACT Wazalendo tunaitaka Serikali ya Rais Magufuli, Kusitisha Mbio za Mwenge wa Uhuru ili Fedha zinazotumika kuuzungusha Nchi nzima zitumike kutengenezea madawati. Na kuwaachia Jukumu la Usimamizi wa Mashindano Haya Maafisa Utamaduni Na Michezo Kama inavyotakikana na hao "Wadau Muhimu" wa Waziri Simbachawene Waendelee Na zoezi la Utengenezaji wa Madawati.

Mwisho tunatoa Wito kwa Taasisi zote zinazopigania na kutetea Haki za Watoto kusimama pamoja katika kuhakikisha Watoto wa Kitanzania waliopo mashuleni wanaendelea kupata haki yao ya kucheza na kuitaka Serikali iwajibike katika ipasavyo kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa Watoto.

Imetolewa na 
Likapo B. Likapo
Mtaratibu Taifa Ngome ya ACT Wazalendo
17/06/2016

No comments: