Thursday, June 23, 2016

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AWAPA TANO LHRC,AANGUSHA MKATABA MPYA NA WANAHARAKATI HAO

Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD akiwa anabadilishana mkataba na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini ;LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA baada ya kusaini mkataba mpya wa mashirikiano baina ya nchi ya Norway na LHRC mkataba ambao utadumu kwa miaka mitatu zaidi.PICHA NA EXAUD MSAKA HABARI
 Balozi wa wa Norway nchini Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD amekimwagia sifa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Nchini Tanzania LHRC kwa juhudi kubwa wanazozionyesha katika kuwasaidia watanzania kuwatetea kupata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watu kisheria.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD akiwa anasaini mkataba huo pembeni ni Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini ;LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA naye akisaini kuashiria kukua kwa ushirikiano wao
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es salaam alipotembelea kituo hicho chenye maskani yake Kijitonyama na kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu zaidi wa mashirikiano Baina ya nchi yake na Kituo hicho mkataba ambao umetajwa kuwa utawezesha wanaharakati hao kuendelea kupigania haki za watanzania kwa hari mpya.


HANNE akizungumza na wanahabari ambao walifika kushughudia tendo hilo la kusaini mkata mpya amesema kuwa Nchi ya NORWAY wamekuwa wakiwaunga mkono LHRC tangu mwaka 2004 ambapo amekiri kuwa tangu waanze kutoa ufadhili kwa wanaharakati hao wamekuwa wakiona mambo makubwa wanayofanya na hawajuti kuwa wabia wa kituo hicho.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini ;LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizngumza na wanahabari baada ya kusaini mkataba huo
Ameongeza kuwa wakati kituo hicho cha sheria na haki za binadamu kikiwa kimetimiza miaka 20 ya uwepo wake mwaka jana kimeonekana kuwa ndio shirika bora na imara la kutetea haki za binadamu nchini Tanzania jambo ambalo amesema linafaa kupongezwa na kila mtanzania ambaye anatetea haki za watu na kuahidi kuendelea kuwa nao pamoja ili kufanikisha malengo ambayo wamejiwekea.

Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD akizungumza na wanahabari waliofika kushughudia Tendo hilo.
Aidha amesema kuwa nchi yake imekuwa ni moja kati ya nchi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kushirikiana na mashirika ya kimataifa ambayo yanapigania haki za wanadamu jambo ambalo liliwapa nguvu ya kuanzisha mashirikiano na LHRC kwa kuwa wanachokifanya ni jambo jema ambalo linafaa kuungwa mkono na kila mtu.


Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA pamoja na kushukuru kwa ujio wa Balozi huyo na mkataba huo amesema kuwa mkataba huo mpya utawasaidia katika kuendeleza mapambano ya kupigania haki na kufikia malengo waliojiwekea ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kisheria maeneo mbalimbali,kuhamasisha watanzania kuzitambua haki zao na shughuli nyingine ambazo zinafanywa na kituo hicho.
Mkataba huo unatajwa kufikia pesa za Norway Prona million 17.

No comments: