HABARI KUBWA LEO TANZANIA-ALICHOKIFANYA LOWASA KWENYE MAHAFALI YA VIJANA WA CHADEMA DAR ES SALAAM KIPO HAPA


IMG-20160618-WA0015.jpg
Ni maafali ya CHASO mkoa wa Dar es salaam ambayo yamefanyika katika kumbi wa Karimjee na kuhudhuriwa na viongozi wakubwa wa chama hicho akiwemo mgeni Rasmi EDWARD LOWASA pamoja na wahitimu kutoka vyuo mbalimbali mkoa wa Dar es salaam

IMG-20160618-WA0038.jpgMratibu wa CHASO mkoa wa DSM Yuda Guti akitoa utambulisho sasa mbele ya mgeni rasmi amewapongeza na kuwashukuru wanachama wa CHASO kwa uvumilivu wao pamoja na vikwazo mbalimbali wanavyopata wakiwa vyuoni kutokana na itikadi yao ya kuipenda Chadema.Amewataka huko wanakokwenda baada ya kumaliza vyuo wajue kwamba ndiyo wanatakiwa wakajipambanue zaidi kuipigania Chadema na Taifa

Meya wa jiji la DSM Mstahiki Isaya Mwita ambapo amewapongeza vijana wa Chadema waliopigana kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa DSM na kumtoa Meya na Naibu wake kutoka mshirika wetu wa Ukawa.Meya anasema hata kuwepo ndani ya ukumbi wa Karimjee ulioko chini yake ni matunda ya kazi yao.

IMG-20160618-WA0033.jpgMeya Issaya anawaasa vijana wasiogope kuingia kwenye soko la ushindani.Anasema yeye alipomaliza chuo alikataa kuajiriwa na akahakikisha anapambana mpaka akafanikiwa.Amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na wabadilishe mentality ya watu huko wanakokwenda kuhusu kufanya kazi kwa bidii.

Lowassa anazungumza
Mgeni Rasmi waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ameanza kuwashukuru vijana kwa kumwamini na kumwalika katika mahafali hayo.

Lowassa anasema akiona umati huo wa wanafunzi wenye bashasha unamkumbusha mbali sana katika mapambano ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

IMG-20160618-WA0013.jpgAnasema hakuna asiyejua kwamba alishinda na kutokana na sababu hiyo wakawakamata vijana wa Chadema na kuwafunga ili wafute ushahidi.

Huku akishangiliwa Rais...Rais.Rais kiongozi huyo amewataka watanzania kupigania Tume huru ya uchaguzi kama Kenya wanavyofanya kwani tume iliyopo ni kama kitengo cha CCM.

Pia Lowassa amewataka wahitimu hao kuhakikisha kwamba wanaongoza watanzania kudai katiba mpya vinginevyo itakuwa vigumu sana kupambana na watu wanaotumia katiba mbovu kama kichaka cha kuminya demokrasia.

Lowassa amesema kwa hali yoyote ni lazima tume hii ya uchaguzi yenye mafungamano na CCM iondoke.Amesema haiwezekani tume inayoshindwa kutangaza mtu aliyeshinda uchaguzi.

Waziri mkuu huyo mstaafu amesema kamwe hawezi kukubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana hata kama itabidi kufa.

Lowassa amesema baada ya uchaguzi mkuu walimleta Nabii Joshua ili amshawishi akubali matokeo lakini alimjibu Nabii huyo kama atakubaliana na matokeo yale basi ajue heshima yake itashuka.Lowassa amesema Nabii Joshua aliondoka kwenye hoteli aliyopangiwa na alikataa kushiriki kuapishwa kwa Rais mpya

Kwa mara ya kwanza Lowassa amezungumzia kuhusu Bunge kutokuwa Live na kusema kuzuiwa matangazo ya moja kwa moja ni aibu kubwa kwa watawala na heshima yao imeshuka kupitiliza.

Lowassa ameendelea kusema vijana wengi hawana ajira na ni bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote kuanzia sasa.

IMG-20160618-WA0011.jpgKuhusu elimu Lowassa amesema haoni mpango wowote madhubuti wa kukwamua elimu yetu.Amesema inatakiwa kuwe na mpango madhubuti wa muda mfupi na mrefu kuhusu elimu kama ilivyo katika ilani ya uchaguzi ya Chadema.

Lowassa anesema watawala hawana raha kwa sababu Chadema na Ukawa wameshinda maeneo mengi sana kote nchini.Amewataka wote walioshinda kuhakikisha wanafanya kazi kubwa na nzuri kuwatumikia watu ili uchaguzi wa 2020 washinde kwa urahisi.Lowassa ameapa mwamko anaoona sasa wa watanzania na mateso makubwa wanayopata chini ya CCM basi ni dhahiri mwaka 2020 Chadema na Ukawa watapata ushindi mkubwa sana.Anasema watanzania wamekata tamaa chini ya utawala huu na hawana matumaini tena

IMG-20160618-WA0017.jpgLowassa amemaliza kuhutubia na kuwashukuru tena vijana wa Chaso kwa jinsi wanavyopigania Chadema.Lowassa anashangiliwa sana kwa shangwe kuu huku mamia ya vijana hawa wakiimba...Rais...Rais...Rais.Kwa hali inayojionyesha hapa ukumbini ni wazi Edward Lowassa ndiye mwanasiasa maarufu zaidi Tanzania na anayependwa kupitiliza.

Sasa inafuatia kula kiapo kwa viongozi wapya wa matawi na kisha utafuatia ugawaji wa vyeti kwa wahotimu......

Habari kwa msaada wa http://www.furahianewz.com/


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.