Thursday, June 16, 2016

HAPA SIO KAZI TU NI KATIBA MPYA TU-JUKATA WAIBUKA KWA KISHINDO TENA,SASA KUZUNGUKA KUDAI MCHAKATO WA KATIBA MPYA


 Baada ya ukimya wa muda mrefu nchini Tanzania kuhusu upatikanaji wa katiba mpya ambayo mchakato wake ulitelekezwa na serikali ya awamu ya nne hatimaye Jukwaa la katiba nchini Tanzania JUKATA wameamua kufufua upya mchakato huo huku wakimtaka Rais wa Sasa DR JOHN POMBE MAGUFULI kutangaza haraka kuanza kwa mchakato wa katiba mpya na kuacha kuona ugumu katika swala hilo nyeti kwa wananchi.

Mchakato wa katiba mpya nchini Tanzania uliasisiwa na Aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne Mh Dr JAKAYA KIKWETE ambapo pamoja na changamoto nyingi kujitokeza mchakato huo ulizalisha Katiba inayopendekezwa ambapo hadi leo haijulikani ni lini mchakato huo utaendelea ili kuwapatia watanzania katiba mpya.
Akizungumza na wanahabari Leo Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Tanzania Jukata  Bwana DEUS KIBAMBA amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imekuwa waoga kuhusu mchakato huo huku Rais akishindwa wapi pa kuanzia kutokana na jinsi mchakato huo ulivyoendeshwa hapo awali jambo ambalo limewasukuma wao kama JUKATA kauamua kuingia Rasmi katika kufufua mchakato huo ambao umetafuna mabillioni mengi ya watanzania.

Bwana KIBAMBA ameeleza kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifwatilia kwa ukaribu swala la katiba mpya na kuishia kuwahoji wao kuwa umeishia wapi hivyo wameamua kuwasaidia wananchi kufufua mchakato wao ambao umetafuna pesa zao ili kuwasaidia kupata katiba mpya.
“Tunatangaza Rasmi kuwa leo kwa upande wa wananchi tumezindua Rasmi mchakato wa kudai katiba mpya nchini Tanzania na tunaitaka serikali kupitia kwa waziri wa Sheria na Rais kwa ujumla warejeshe mchakato wa katiba mpya ili watanzania wapate katiba ambayo iliwapotezea muda katika kutoa maoni.

Ameendelea kueleza kuwa Rais wa awamu ya Tano amesikika akitaja neno katiba mpya mara mbili tu tangu alipoingia madarakani jambo ambalo amedai ni hatari sana kwa mchakatro huo kutokana na uhitaji wa katiba kwa wananchi na gharama zilizotumika.

Aidha Jukwaa la katiba Tanzania limeitaka serikali kupitia kwa wizara ya katiba na sheria kupeleka bungeni mishwada ya kurekebisha sheria zinazosimamia mchakato wa katiba kwa ajili ya kuhuisha katika tarehe zake zote zilizopitwa na wakati hii ni kutokana na sheria ya mabailiko ya katiba ya mwaka 2011 na ile ya kura ya maoni ya 2013 kupitwa na wakati na haziwezi kutumika tena bila marekebisho na kwa vile bunge la bajeti linaelekea kumalizika bila mishwada ya marekebisho ya sheria hizo kupelekwa bungeni na hakuna pesa iliyotengwa kwa ajili ya swala la katiba mpya katika bajeti ya mwaka huu.
Aidha Jukata wamependekeza kuitishwa kwa mkutano mkuu wa kitaifa wa katiba maarufu kama NATIONAL CONSTITUTION CONFERENCE ambao utatumika kupitia maudhui ya katiba iliyopendekezwa ilinganishwa na Rasimu ya tume ya warioba lengo likiwa ni kuainisha maeneo makuu yanayolalamimikiwa na watanzania kiasi cha kuligawa Taifa kama nilivyo sasa.

Jukwaa la katiba Tanzania JUKATA wamekuwa kimya tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya tano ambapo sasa wameibuka na kudai kuwa wamegundua serikali hii imekuwa waoga wa kuendeleza mchakato wa katiba na wao wameamua kuamsha watanzania na sasa wataingia mtaani kutoa elimu na kuamsha hari ya watanzania kudai katiba yao ambayo imetumia mabilion katika ukusanyaji wa maoni yake.

No comments: