KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI HOLILI

ban1Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye ni  mfanyabiashara aliyekua akipita kutoka nchini Kenya  kupitia mpaka uliopo katika  kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban2Mfanyabiashara John Evarist aliyekua akipita kutoka nchini Kenya  kupitia mpaka uliopo katika  kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro, akijibu maswali aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea(wa kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban3Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea ( aliyenyoosha mkono), akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban4Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipanda Mlima   kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo  mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
ban5Ujumbe ulioongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(), ukishuka kutoka mlimani   baada ya ukaguzi wa mpaka uliopo Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo  mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.