Thursday, June 23, 2016

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAJANE UWANJA WA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM


Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya siku ya wajene Tnzania ambaye alikuwa SIHABA MKINGA – KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII YA JINSIA WAZEE NA WATOTO.akikagua shughuli mbalimbali zilizokuwa zinaonyeshwa na wakina mama hao wajane katika uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam

 Leo ni siku ya tarehe 23 mwezi june ambako duniani kote uadhimishwa siku ya wajane duniani na kwa mara ya pili Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku hiyo. Leo wajane zaidi ya 500 walikuwa katika uwanja wa mnazi mmoja kwa kuadhimisha siku yao chini ya chama chao cha wajane (TAWIA) wajane hao wameweza kuadhimisha siku hiyo kwa tafrija fupi iliyo udhuriwa na vyama mbalimbali vinavyotetea haki za wanawake na nyinginezo kama  WLAC,ISF,LHRC,UN  na vyama vingine vingi vinayosaidia kupatikana kwa haki za wajane.
SIHABA MKINGA – KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII YA JINSIA WAZEE NA WATOTO. akizngumza katika maadhimisho hayo
Siku hiyo iliyopambwa na mambo mbalimbali yaliyofanyika uwanjani hapo kama maigizo yaliyofanywa na wajane wenyewe wakiweza kuonyesha jinsi gani wanavyoweza kupata manyanyaso baada ya wanaume wao kuweza kufariki dunia na ndugu wa mwanaume kusahau kuwa ndugu yao ameacha mjane na watoto na hivyo kuchukua mali zote bila kufikiria mjane na watoto walioachwa wataishi vipi pia kuliweza kuwa na nyimbo mbalimbali walizoziimba kwa majonzi wakielezea upatikanaji wa haki zao.

Sherehe hiyo iliyoudhuliwa na wageni toka sehemu mbalimbali akiwemo SIHABA MKINGA – KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII YA JINSIA WAZEE NA WATOTO.  Muwakilishi wa bilal Tanzania ,mwakilishi wa mstahiki meya wa kinondoni ,mama kairuki kutoka hospitali ya kairuki, diwani mama Msofe kutoka kipunguni na wengine toka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa wanawake wajane nchini Tanzania TAWIA Bi ROSE SARWAT akitoa maelezo mbele ya wakina mama hao
Mgeni rasmi mama SIHABA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo akizungumza katika shughuli hiyo amesema kwamba serikali ipo makini na inamipango mingi kuhusu wajane na kwamba wanajaribu kufanya marekebisho ya sheria kandamizi zinazoweza kumkandamiza mwanamke mjane.pia alisema kuhusu kuwasaidia anawashauri wanawake hao kuweza kujiunga kwenye vikundi mbalimbali vya mikopo kuweza kijiinua kiuchumi..
Mgeni toka umoja wa mataifa ambae ana asili ya kihindi amesema kuwa  amefurahishwa kuona wajane wamekusanyika pamoja na wanaweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili.huku akiisema kuwa amefurahishwa na maneno ya mjane toka shinyanga ambaye aliyeweza kuishi na hali hiyo ya ujane ndani ya miaka19 mpaka sasa, na ndugu wa mumewe waliweza kuleta vizingiti vingi kwenye mali lakini alikuwa thabiti na kuweza kuvishinda vizingiti hivyo hatimaye leo ameweza kupata haki yake,amesema kuwa umoja wa mataifa uko sambamba na wajane wote duniani na kuhakikish wanapata haki zao kupitia shirika lao linalo fuatlia haki za wajane duniani kote.pia amesisitiza wahakikishe wanawapatia watoto wao elimu kwa maana ni funguo kwenye maisha yao na ndio kitu pekee kitakachoweza kuwakomboa katika maisha yao.

Maadhimisho hayo yalifanyika ndani ya uwanjua wa mnazi mmoja ambapo wanawake hao waliweza kuweka kambi hapo huku wakipewa huduma mbalimbali zikiwemo za upimaji wa magonjwa mbalimbali huduma iliyokuwa inasimamiwa na wataalam kutoka Hospitali ya KAIRUKI

No comments: