Tuesday, June 21, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

MHA1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo Bungeni leo kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali dhidi ya  waajiri wote wanaoshindwa kuwasilisha michango ya waajiriwa wao katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ambapo tayari Serikali iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kuunda kikosi kazi kitakachoshughulikia swala hilo.
MHA3
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. George Masaju leo Bungeni Mjini Dodoma.
MHA4Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrisom Mwakyembe akijibu moja ya hoja zilizotolewa Bungeni  leo na Mbunge wa Nchemba Mhe. Juma Nkamia aliyetaka kujua uhalali wa mtuhumiwa aliyetenda kosa la jinai la kumtukana Rais kuachiwa huru na kwenda kutafuta fedha za kulipa faini ilihali kosa alilotenda limemdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli.
MHA5
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira, Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde leo Bungeni Mjini Dodoma.
MHA6Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo iliyoombwa na wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma kabla ya Kuahirisha shughuli za  Bunge leo Mjini Dodoma.
MHA7Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisasa  ya mjini Dodoma wakiwa katika ukumbi wa Bunge kwa lengo la kujifunza majukumu ya Bunge leo Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
kol1Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Susan Kolimba akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa ili kuimarisha Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwa ni moja ya hatua za kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali.
kol2Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu maswali yaliyoulizwa na Wabunge  leo Bungeni juu ya mikakati ya Serikali kuwawezesha wanawake kupitia Benki ya wanawake kwa kufungua madirisha maalum  Katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini yatakayosaidia kuwasogezea wanawake huduma za Benki hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
kol3Wanafunzi wa chuo Kikuu Dodoma  (UDOM) Wakiwasili katika ukumbi wa Msekwa Bungeni  Mjini Dodoma leo kwa lengo la kujifunza jinsi Bunge linavyotekeleza majukumu yake

No comments: