Thursday, June 9, 2016

VIDEO-Baada ya Bajeti ya Jana kusomwa Hili limetokea TGNP asubuhi ya leo

Wanaharakati ngazi ya jamii kutoka mikoa mbalimbali ambayo ni Dar es salaam,shinynga,morogoro,mbeya na washiriki wa semina ya Jinsia na maendeleo GDSS ,kikundi kazi cha uchambuzi wa bajeti BATT,na asasi nyingine za kiraia wakiwa katika maandamano madogo ya kuonyesha kutokubvaliana na bajeti ya nchi iliyosomwa jana Bungeni Dodoma ambapo shuguli hiyo imefanyika katika Ofisi za makao makuu ya Mtandao wa Jinsia TGNP Dar es salaam leo
 Na Vicent Macha-Dar es-salaam

Wakati ikiwa ni siku moja baada ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka 2016/2017 ikiwa imesomwa na kuanza kujadiliwa Bungeni wadau mbalimbali wameanza kutoa maoni kuhusu bajeti hiyo ambapo wanaharakati mbalimbali wakiongozwa na mtandao wa jinsia TGNP wakipinga vikali bajeti hiyo kwa kile wanachodai kuwa bajeti hiyo imelenga Zaidi kwa secta binafsi na wafanyabiashara na kuwasahau wananchi wa kawaida ambao ni wazalishaji wakuwa na walipa kodi wakubwa.
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa Taifa ambaye pia ni mwenyekiti maarifa  wa kata ya makumbusho Bi JANETH MAWIZA amesema kuwa vipaumbele ambavyo vimewekwa kwa bajeti ya mwaka huu ni wazi kuwa havimlengi mtu wa pembezoni na badala yake vinawalenga wawekezaji wakubwa na kuwaacha masikini pembeni ambapo ameeleza kuwa kutokjana na hali hiyo haitamuwezesha mtanzania masikini kuwa na masha bora hata kama uchumi nutakuwa

Ameongeza kuwa bajeti ya mwaka huu iliyosomwa jana bungeni Jana  wao kama wanaharakati wanadai uwajibikaji wa serikali katika kusimamia ukusanyaji wa mapato na kutafuta vyanzo mbadala vya mapato endelevu ili kudhibiti kuendelea kukopa.

Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa Taifa ambaye pia ni mwenyekiti maarifa  wa kata ya makumbusho Bi JANETH MAWIZAakisoma Tamko la wanaharakati hao juu ya Bajeti ya nchi Iliyosomwa jana Bungeni Dodoma na Kugusa Hisia za watanzania wengi.
Aidha mambo mengine ambayo wanaharakati hao wanadai ni pamoja na kuwepo mfumo shirikishi na endelevu katika kutengeneza na kufwatilia utekelezaji wa bajeti.kuongezwa kwa bajeti ya maji,na afya ambazo wamedai ni ndogo sana na haziwezi kutimiza malengo mazuri hasa kwa wanawake wa Tanzania.

Nimekuwekea Video Kuhusu Tukio hilo

No comments: